kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,423
- 13,935
Walioimba "tuna imani na Lowassa" siku ile kwenye mkutano ule ni karibu robo tatu ya wajumbe wote mkutanoni, wajumbe hawa bado wamevaa magwanda ya kijani hadi leo na wamo humohumo ndani ya CCM wao pamoja na wafuasi wao mgongoni, kuwatimua wote hawa ni sawa na kuamua kuanzisha CCM nyingine. Itakuwa na ilivyoanzishwa timu ya Pan African kutoka Yanga na Nyota Nyekundu kutoka Simba. Kuwatimua akina Sophia Simba chamani ni sawa na kutatua tatizo la wasaliti kwenye chama kwa 0.00025% tu. Nijuavyo mimi 97.99% ya mashina ya wakereketwa nchini ni wanachama fake waliojificha mule kwa maslahi yao maalumu tena ya kihalifu kama vile kuuza na kusambaza madawa ya kulevya, kupokea na kusambaza pesa za rushwa za wagombea wakati wa kura za maoni na kuchagua wagombea nyakati za kura za maoni. Ukifuta matawi ya wakereketwa, kupiga vita madawa ya kulevya na kuimaliza rushwa ya kwenye uchaguzi chama kwa vyovyote vile hakiwezi kuwa na wanachama 8m hata kidogo, wengi watatimka na kuanza siasa za kuchagua mgombea badala ya chama.