Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,041
- 1,294
Wasiseme sikuumwa.
Usiku wa saa nane ,imepigwa hii simu
Ni kwasababu ya mane, nimeridhi kunywa sumu
Nimeishi kama bene , sikuwa na umuhimu
Wasiseme sikuumwa, Abuu hili liseme
Sikulala miezi sita, mawazo yaniumiza
Hadi macho yalisita, yalivyo nisheheneza
Chakula hakikupita, hata ningajiliwaza
Wasiseme sikuumwa, Abuu hili liseme
Nje 'likuwa mzima, kwa ndani kulishakufa
Nikabakia hamuma, bongo likapata ufa
Isitokee husuma, Abuu andaa dhifa
Wasiseme sikuumwa, Abuu hili liseme
Waambie niliumwa, sonona imeniua
Hakika sijasukumwa, meafiki kujiua
Nimezidi mkaumwa, munifanyie adua
Wasiseme sikuumwa, Abuu hili liseme
✍️Abuuabdillah
Usiku wa saa nane ,imepigwa hii simu
Ni kwasababu ya mane, nimeridhi kunywa sumu
Nimeishi kama bene , sikuwa na umuhimu
Wasiseme sikuumwa, Abuu hili liseme
Sikulala miezi sita, mawazo yaniumiza
Hadi macho yalisita, yalivyo nisheheneza
Chakula hakikupita, hata ningajiliwaza
Wasiseme sikuumwa, Abuu hili liseme
Nje 'likuwa mzima, kwa ndani kulishakufa
Nikabakia hamuma, bongo likapata ufa
Isitokee husuma, Abuu andaa dhifa
Wasiseme sikuumwa, Abuu hili liseme
Waambie niliumwa, sonona imeniua
Hakika sijasukumwa, meafiki kujiua
Nimezidi mkaumwa, munifanyie adua
Wasiseme sikuumwa, Abuu hili liseme
✍️Abuuabdillah