Songombingo la Kibiti

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,207
4,405
SONGOMBINGO LA KIBITI.

1)Nilisema sitosema,ila sasa tumechoka
Nitasema nayosema,hata kwa kuja ropoka
Yalosemwa ndo nasema,leo yaje kujulika
Songombingo la Kibiti,washenzi mnahusika.

2)Hivi mna roho gani,enyi wana wa shetani
Huu upuuzi gani,mnautenda nchini
Nahisi mwala majani,na yamewajaa kichwani.
Songombingo la kibiti,washenzi wanahusika.

3)Ni siasa ama dini,mbona eti inafanywa siri
Wakulisema ni nani,jambo hili la hatari
Twahofia hayawani,walojawa na viburi
Songombingo la Kibiti,washenzi wanahusika.

4)Mkuranga wakatenda,wakaruka na mabawa
Wakaua wakaenda,hawa mashetani hawa
Hivi hakuna magwanda,wakutokomeza hawa
Songombingo la Kibiti,washenzi wanahusika.

5)Iwapi intejensia,wakuyagundua haya
Kabla hayajatokea,na kutendeka mabaya
Mapigo ya kuotea,yafanyika bila haya
Songombingo la kibiti,washenzi wanahusika.

6)Taifa letu ni dogo,hakuna pakujificha
Kama tungekuwa mbogo,wasingetoa makucha
Tuwapige kwa vipigo,wanotenda wangeacha
Songombingo la Kibiti,washenzi wanahusika.

Shairi-SONGOMBINGO LA KIBITI
Mtunzi-Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
[HASHTAG]#mimimalenga[/HASHTAG]
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom