mkuuwakaya
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 1,063
- 1,456
Heroin ni nini?
Heroin ni dawa inayotengenezwa kutokana na dawa nyingine aina ya morphine inayovunwa kutoka mbegu za mimea inayopatikana nchi za Asia. Heroin huonekana kama unga mweupe, kijivu au kama nta nyeusi kwa namna ilivyoandaliwa. Dawa hizi zina uwezo wa kuondoa maumivu makali kwa kuzuia ubongo kupokea taarifa kutoka sehemu ya mwili inayouma.
Heroin pia iliwahi kutumika kutibu wanajeshi wa marekani waliokuwa na magonjwa ya msongo wa mawazo (Post Traumatic Stress Disorder), kutokana na kumbukumbu za matukio ya kutisha walioshuhudua vitani – Vietnam. Magonjwa haya huambatana na ndoto za kutisha na hata kuyaona upya matukio yale yaliyopita (visual hallucinations).
Ni kweli kuwa heroine humfanya MTU kusikia raha!
Ni kweli tupu. Heroine hustua seli za ubongo kuzalisha homoni aina ya Dopamine ambayo humfanya mtu kusikia raha. Homoni hii hutolewa kwa kiasi cha unit 1200- 1800 baada ya kutumia heroine kulinganisha na unit 150 – 200 tu zitolewazo wakati mtu anaposhiriki ngono. Ndio kusema Heroin inaleta raha karibu mara tisa ya ile itokanayo na ngono, tena kwa muda wa takribani dakika 30- 45.
Uvumilivu /Tolerance
Matumizi ya Heroin hufanya akili kupumbaa na hivyo kuhitaji kiasi kikubwa zaidi kwa mara nyingine. Seli za ubongo huongeza vipokezi vya homoni ya Dopamine ili kupokea homoni nyingi inayozalishwa, Hali hiyo hupelekea ubongo kuhitaji Heroin zaidi ili kujikidhi. Kwa hiyo mtumiaji huongeza kiasi kila wakati.
Arosto /withdraw symptoms
Wakati Heroin inapoisha mwilini, mwili hutamani zaidi. Hapo ndipo hutokea “arosto”, ambapo mtumiaji hutaabika kwa kukosa raha isiyo kifani. Maumivu makali ya tumbo, viungo na kichwa, baridi kali, mapigo ya moyo kwenda kasi, mwili kutetemeka, kujisikia vibaya sana, kuchoka, kushindwa kula na dalili nyingine mbaya humpata. Hali hiyo humlazimu kwa haraka sana kutafuta namna ya kuipata Heroin iwe kwa njia halali au haramu.
Acknowlegment goes to AfyaNjema