Soma mtoto wa kike

Soma mtoto wa kike

Joined
Jan 4, 2012
Posts
61
Reaction score
23
SOMA MTOTO WA KIKE

Soma mtoto wa kike, soma usitetereke,
Soma usishawishike, hadi mwishoni ufike,
Soma nyadhifa ushike, Nchi hii utumike,
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Soma usibabaike, mafundisho uyashike,
Soma usidanganyike, vishawishi uepuke,
Soma kisha utumike,katu usiangaike,
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Soma na ufundishike, na vikwazo uvivuke,
Soma nami niridhike,moyo nisisononeke,
Soma kesho unizike, mahali pema niweke,
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Soma usirukeruke,bongo zako zichemke,
Soma yote ukumbuke,masomo yasiponyoke,
Soma usirubunike,mwanangu usipotoke!
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Soma usipaparike, raha zina muda wake,
Soma nisifedheheke,wenzangu wasinicheke,
Soma nami nitukuke, unasi niheshimike,
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Soma nisinyanyasike,wenye wivu watapike,
Soma nami ninyanyuke,jina langu lisifike,
Soma nisiwe mpweke, tamati nitamatike!
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Lambert Chialo(Mhadhiri wa Malenga)
Magogoni, Dar es Salaam
0713 961860
 
^^
Hivi si niliambiwa eti wanaume wanawasomea? Ya Kweli haya Munkari na mimi49
^^
 
Last edited by a moderator:
SOMA MTOTO WA KIKE

Soma mtoto wa kike, soma usitetereke,
Soma usishawishike, hadi mwishoni ufike,
Soma nyadhifa ushike, Nchi hii utumike,
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Soma usibabaike, mafundisho uyashike,
Soma usidanganyike, vishawishi uepuke,
Soma kisha utumike,katu usiangaike,
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Soma na ufundishike, na vikwazo uvivuke,
Soma nami niridhike,moyo nisisononeke,
Soma kesho unizike, mahali pema niweke,
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Soma usirukeruke,bongo zako zichemke,
Soma yote ukumbuke,masomo yasiponyoke,
Soma usirubunike,mwanangu usipotoke!
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Soma usipaparike, raha zina muda wake,
Soma nisifedheheke,wenzangu wasinicheke,
Soma nami nitukuke, unasi niheshimike,
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Soma nisinyanyasike,wenye wivu watapike,
Soma nami ninyanyuke,jina langu lisifike,
Soma nisiwe mpweke, tamati nitamatike!
Soma nakutegemea, soma mtoto wa kike.

Lambert Chialo(Mhadhiri wa Malenga)
Magogoni, Dar es Salaam
0713 961860


CC: Paloma,,,,, Madame B,,,,, Heaven on earth,,,,, Paloma, ,,,,, Preta Evelyn Salt,,,,, heaven on desert na gfsonwin mmesikia ujumbe?? someni muwe na jeuri yenu na nyonyi
 
Last edited by a moderator:
ukweli mtupu wasome sana!
ila mke wangu asinizidi mshahara tu!
 
Back
Top Bottom