Hello wana Jamii,
Ninashukuru kuona kupitia Forum hii nimeweza kupata wateja wa Consultancy services zetu chini ya KIMI DEVELOPMENT CONSULT LTD. Sio wote wanaotambua umuhimu wa BDS (Business Development Services) kwakuwa bado watanzania wengi tunategemea kupata ushauri wa kirafiki na katika Forum kama hizi. Ukiangalia kwenye Forum yetu hakika watu wanatoa mawazo mazuri ya kujenga, japo kuna wengine wanakatisha tamaa wenzao, pale wanapohitaji msaada na ufafanuzi fulani.
Ningependa kushauri kuwa ili Forum iwe nzuri hasa kwenye THREADS zenye kwajenga watu wengi kusiwepo watu wa kukakatisha tamaa wenzao, kama lengo ni kusaidiana basi litimie. Naamini kupitia humu watu wana nufaika sana. Kama mtu ana jambo lake mfano Mizaha basi apeleke katika Jukwaa husika.
Katika kutangaza kwangu kupitia Forum hii, watu niliowapata kama wateja wangu ni watu SERIOUS kwakuwa unakuta HAJACOMMENT ila anatafuta CONTACTS moja kwa moja na tuna ongea, tunajadili na tunafanya.
MTEJA mmoja amenipa RUKSA ya kusema ushuhuda wake kwakuwa sisi kama kampuni tumefanya vile alivyo tarajia kulingana na Hitaji lake. Mteja huyu wa Makete, ana shamba la ekari 6 huko kwao Makete, alihitaji afanyiwe Upembuzi Yakinifu (Feasibility study) na hatimaye tumwandalie Mpango wa biashara yake hiyo (Business plan) YA kilimo cha matunda aina ya PEASI kama zinazotoka Africa kusini, kwa lengo la kujipatia UWEZESHWAJI KIFEDHA kutoka chanzo kimoja cha shirika la kifedha la kimataifa ( OIKO CREDIT), sisi KIMI DEVELOPMENT CONSULT LTD ( tembelea hapa
KIMI DEVELOPMENT CONSULT LIMITED) tulikubaliana na MTEJA huyu tukafanya kazi zote, na ndani ya miezi 6 akapata HITAJI LAKE la mkopo wa masharti nafuu (kiasi kama 85m hivi). HIVI sasa yuko kwenye utekelezaji wa mradi wake kwa kadri ya PHASES zake. Na kimsingi amekubali kuwa kampuni yetu tumejitahidi kufanya kazi yake vizuri kwakuwa hakutarajia kama ingewezekana.
Mteja wa pili ni kwenye upande wetu wa pili wa shughuli za kampuni yaani Sourcing, supplying and/or selling various local or imported Goods. Huyu yuko Ifakara alihitaji kutafutiwa used Laptops ili aanzishe chuo cha mafunzo ya kompyuta, Kama kampuni tunakafuta link na makampuni ya nje, tukafanikiwa kupata laptops nzuri kwa bei nzuri, kiasi cha yeye kutoamini kuwa mzigo wake tulimfikishia hadi mahali alipo (ifakara) kwa mkataba wetu tuliokubaliana. Mtu huyu pia tuko katika kumwandalia Documents Mhimu za kusajili taasisi yake na Business plan (sisi tuna amini a right business must have an organised way throught its life).
Ni vema nikakumbusha kuwa tatizo la ajira nchini linahitaji sisi wasomi kujipanga vema ili tuwe msaada kwa ambao hawajafikia elimu husika lakini pia kuajiri wengine. Kupitia kazi za ofisi yetu huwatumia part time consultants kama assistants katika level ya diploma na degree ili kufanya hizi kazi, hivyo kuwa sehemu ya kutatua tatizo la ajira lakini pia vijana husika kupata Uzoefu utakao hitajika wanapojitafutia kazi.
Nirudie kusema tena kama kuna watu wamejiajiri humu JF ni vema tukatiana moyo, na nitoe wito kuwa WALE wanaojitangaza humu kufanya haya na yale BASI wajitahidi kuwa wakweli(inasemekana wapo matepeli) kwa wateja wao ili FORUM hii iwe ni market source na sehemu kubwa katika kuleta maendeleo ya members na non members.
In the next thread nitaendelea kutoa ushahidi wa kazi zetu, ili kwamba MHITAJI WA KWELI ajue wapo watu walio serious. Kama unataka undani zaidi ni vema ukaongea nasi kiofisi (usiishie kusoma comments za humu ndani).
Tutembelee;
KIMI DEVELOPMENT CONSULT LIMITED
SIMU: 0754 734009/0652 656565
EMAIL:
kimiconsultancy@gmail.com
OFISI (PRIMARY): MBEYA mjini
OFISI (secondary): to be opened soon- Sinza Mugabe.