Sokoine kweli alikuwa ni shujaa?

Mr.mzumbe

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,019
968
Kwanza niseme tu, mimi kipindi Sokoine anakuwa kiongozi mimi nilikuwa bado sijazaliwa, mimi kama watanzania wengine nimeweza kumsoma tu kwenye vitabu mbalimbali. Vitabu vinasema huyu bwana alikuwa ni Waziri mkuu wa tatu (3) na kiongozi shupavu sana, vimeenda mbali zaidi na kusema yeye ndiye alikuwa rais anayefuata baada ya Nyerere.

Lakini vitabu hivyo hivyo vinatueleza huyu bwana alikuwa mtu ambaye ameelewa sera za Mwalimu, kwa maana ya ujamaa na kujitegemea kuliko mtu yeyote yule kwa kipindi kile, yeye alikuwa anatekeleza sera za Bwana Mkubwa kwa vitendo. Kwa mfano tunaambiwa alikuwa mstari wa mbele kwenye ishu ya UHUJUMI UCHUMI. Kwangu mimi nikijaribu kupitia sera ya Mwalimu kwenye mambo ya UHUJUMI UCHUMI naona ni moja ya failure kubwa sana ambayo amefanya kwenye uwongozi wake na nafikri vitabu mbalimbali vimeeleza hata baadae Mwalimu alifikiri kama alifanya makosa makubwa sana.

Mimi nakubali alikuwa na nia njema sana kuona nchi hii inakuwa na uchumi wenye hali nzuri na kila mwananchi aweze kunufaika, lakini nia peke yake haitoshi. Leo ipo ishu kama hii kwa viongozi wetu wa leo ambao maongezi yao, vitendo vyao vinaonesha wanayo nia njema sana na nchi hii lakini tatizo lao hawajui jinsi ya kufikia hiyo nia njema waliyokuwa nayo.

Baada ya maelezo hayo mafupi, mimi nataka niuulize tu, kama sera kuu ambayo Ndugu Sokoine imemfanya awe maarufu nchi nzima ni mambo yale yale ambayo yaliharibu uchumi wa nchi yetu, na nchi kufikia hatua inakwenda kama gari bovu :-

1-je ni kweli Sokoine ni sahihi kumuweka kwenye kundi la viongozi shupavu kwenye nchi hii?
2- Au kama kweli alikuwa shupavu alikuwa shupavu kwenye nini?
3-Au na yeye awepo kwenye kundi la kiongozi wa kawaida tu ambao walikuwa na nia njema lakininhakujua jinsi ya kufikia nia njema yake?

Asante.
 
Back
Top Bottom