Hebu funguka zaidi. Una Cathode za Shaba yaani 99% Pure? Kama ndiyo basi tuwasiliane kwa email SSAMBALI@hotmail.com. Ila ufunguke zaidi kwenye uuzaji. Wauzaji wengi hutaka PESA kwanza au sijui kutanguliza kabla ya mzigo kuchukuliwa. Kuna kampuni hapa wananunua maana wana kiwanda ila tu hawatakupa hata senti tano kabla ya kuwa na uhakika wa Shaba na shaba hiyo kufika kwa Agent wao ili aisafirishe.
Kama utaweza masharti hayo basi niandikie.
WARNING: Kama unafuatilia soko la vyuma la London, LME basi utakuwa umeshaona jinsi Shaba inavyoporomoka bei kwa sasa. Hivyo kuwa macho huko unakoinunua maana usije ukanunua na ukashindwa kuuza. Mchina kapunguza ununuzi wa Shaba kwa sasa kwa sababu wameshapunguza uzalishaji wao wa fujo na sasa vitu vinaanza au kupanda au kushuka. Bahati mbaya, mara nyingi ni Mali ghafi zinashuka bei ila bidhaa zao tayarii, bei inapanda na waumiaji tunabaki sisi Waafrica.