SMZ waongezewa mishahara

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,773
3,471
Habari za kuamka wakubwa na wadogo,

Ni habari ambayo ni ya kweli na ya uhakika kama kichwa cha habari kinavyosema.
Mshahara huo umeongezeka kwa ahadi ya mheshimiwa rais wa Zanzibar ambayo aliitoa katika kipindi chake cha kampeni ambapo aliahidi ifikapo mwezi wa nne mwaka huu ataongeza mishahara kwa wafanyakazi wake wote wa SMZ.

Kutendo kimewapa hamasa sana hasa kwa wale wa vikosi vya ulinzi ambapo walikua wakidharaulika mitaani, na hata kwa wafanyakazi wengine waliokuwa na kipato kuwazidi wao.

Nimpongeze sana rais wa Zanzibar kwa ahadi zake za kweli na kuwatia hamasa wafanyakazi wake kufanya kazi kwa bidii.

Nitoe rai kwa serikali ya SMZ ikitaka kuendelea kuimarika zaidi iachane kabisa na ubabaishaji uliopo SMT maana serikali hii iliweka ahadi nyingi wakati wa kampeni ila hakuna hata kimoja kilichotekelezwa, kila siku ni kuondoa wenye vyeti feki ila wenye wenye hivyo hawaishi na bado wanaendelea kula mishahara ndani ya serikali ya ahadi bila utekelezaji.
 
Kama mambo yake mazuri mkumbusheni atulipe lile deni letu la Umeme wa Tanesco huku Tanganyika,huko zenji jiandaeni kwa kula ubwabwa naona watu wataongeza wake sio mchezo
 
Back
Top Bottom