Ingawaje hatua alizochukua mwakilishi huyu dhidi ya mchhuzi wa samaki hazistahili kuungwa mkono, mimi nafikiri kupanda daladala kunategemea sana mazingira ya wakati huo kwani posho ya mafuta pekee siyo inayoendesha gari. Inawezekana alipata breakdown akajikwamua kwa kupanda daladala ili afike aendako na baadaye afanye mpango wa matengenezo ya gari. Wakati mwingine inawezekana alikuwa anakwenda gereji.
La msingi hapo ni kwamba anapopanda daladala ajue kuna adha atakutana nazo na awe tayari kuzikabili bila jazba wala kuleta rabsha zitakazompa usumbufu, kuaibika na hata kuzua maswali kama haya yanayojitokeza sasa ya yeye kupanda daladala ilhali yeye ni mtu mkubwa sana.