Slaa atangaza 2013 mwaka mtakatifu

Slaa atangaza 2013 mwaka mtakatifu

nice 2

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Posts
747
Reaction score
520
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeufananisha mwaka huu kama mtakatifu, kwa wanachama wake kujiandaa na chaguzi za mwaka 2014 na 2015.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alipokuwa akizindua ofisi za kata na matawi maeneo tofauti ya Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Dk Slaa alisema mwaka huu ni mtakatifu kwa chama hicho, kwa sababu ni pekee uliobaki katika harakati za ukombozi wa Watanzania kabla hawajafikia mwaka 2014.

Aliwataka wanachama na viongozi wa Chadema kufanya kazi zenye kuleta tija kwa wananchi, ikiwamo kufungua ofisi kwa wingi, kuhamasisha wananchi kujiunga kwa wingi na chama hicho.

Alisema lengo ifikapo mwaka wa 2014 ambao ni wa uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka 2015 Uchaguzi Mkuu, kiweze kushika dola.

Dk Slaa ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya kuimarisha chama, kufanya mikutano ya hadahara, alisema licha ya ufunguzi wa ofisi hizo za kata, viongozi na wanachama wahakikishe zinafanya kazi ya kuhudumia wanachama na wananchi siyo kugeuzwa mazalio ya popo au vijiwe. Ili kufanikisha kazi za chama, Dk Slaa aliwataka viongozi hasa madiwani katika siku 365 za mwaka huu, kuhakikisha wanawafikia wananchi kwa njia mbalimbali na kuwaelezea sera za Chadema.

Katika hatua nyingine, Dk Slaa aliwakingia kifua madiwani wa Manispaa ya Moshi kwa kueleza kuwa mara nyingi watu wengi wamejenga tabia ya kulaumu madiwani kila kitu kibaya.

Alisema diwani hashiki fedha, hatoi zabuni na kazi yake ni kuhamasisha maendeleo ya kata husika, ili kuhakikisha miradi iliyopangwa inatekelezwa.

Dk Slaa aliwataka madiwani wa Chadema nchini kuwa mstari wa mbele kusimamia maendeleo ya halmashauri zao.Alisema itakuwa rahisi kwa Chadema kupata ushindi na kumpatia ukombozi wa kweli mwananchi.

Source: Mwananchi
 
Huu ni mwaka muhimu sana katika harakati za kusaka mabadiliko ya kweli na yenye mafaa kwa taifa hili.Ni mwaka ambao CHADEMA inapaswa kuutumia vizuri kwa kuandaa mipango kabambe ambayo itahakikisha inawafikia na kuwafikishia watanzania wengi kzaidi habari njema za ukombozi.
Pia kuzidi kuwajulisha wote wamfahamu zaidi adui namba moja wa uhai wa maisha yao kiuchumi, kijamii na taifa lao kwa ujumla.

LAKINI hili sijukumu la chama peke yake , bali ni ka wote wenye mapenzi mema na taifa hili, waliotambua na kufunguka macho hata kuweza kuujua umuhimu wa kufanya mabadiliko tunapaswa kuifanya kazi hii ya kuufikisha ujumbe huo kwa ndugu,jamaa na marafiki zetu na tuwahamasishe wajiunge nasi kulifikia lengo la kukomboa nchi yetu toka kwenye mikono ya wanyonyaji weusi.

KWA PAMOJA TUTASHINDA!
 
maneno kuntu haya kutoka kwa mtu ambaye probably ni mwanasiasa bora katika bara letu hili la Africa baada ya N.Mandela.
 
Ni mapambano ya kweli mwaka huu mpaka kieleweke,Shoza kaa kule na mipasho yako ya kianalogia.
 
Safi dk kwa kuchapa kz makamanda tumejiandaa vilivyo kushika hatam.
 
Safi Dr mpaka kitaeleweka tu! Mungu akulinde na atulinde sote'
 
hili gazeti la mwananchi naliangalia kwa macho manne,habari zao siku hizi ni kama limenunuliwa na nape,subiri kesho watakavyofyatuka..
 
..
Dk Slaa aliwataka madiwani wa Chadema nchini kuwa mstari wa mbele kusimamia maendeleo ya halmashauri zao.Alisema itakuwa rahisi kwa Chadema kupata ushindi na kumpatia ukombozi wa kweli mwananchi.

Source: Mwananchi
RED:Chezea CHADEMA wewe uone cha moto....
 
Pamoja sana dr. Mbowe keshasema huu ni mwaka wa nguvu ya umma. Local participation ndio ngao ya maendeleo ya umma wetu.
 
hao ndio viongozi wa chama sio wahuni wengine wanaokesha mitandaoni kuwatukana wenzao.pumba na mchele vinajitenga.
 
Back
Top Bottom