Siyo dhambi kwa wapinzani kutekeleza Ilani ya CCM - RC

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Elaston Mbwilo amewataka wanasiasa na wafanyakazi, kutambua kuwa Ilani ambayo inatakiwa kutekelezwa katika kuwaletea wananchi maendeleo ni Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ; na sio dhambi hata wapinzani kuitekeleza hiyo.

Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana, baada ya baadhi ya watu kupinga uamuzi wake wa kuwataka madiwani kutoka vyama vya upinzani, kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Mbwilo alieleza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inamtaka kila kiongozi wa chama na mtumishi wa umma kuhakikisha anatekeleza Ilani ya chama kilichoshinda kuongoza serikali bila ya kujali itikadi za vyama, dini au kabila.

Alieleza kuwa kutekeleza Ilani ya CCM siyo dhambi kwa vyama vya upinzani, bali ni kutekeleza matakwa ya kikatiba katika kuhakikisha wanawaletea maendeleo Watanzania. “Awamu hii ya tano chama kinachoongoza serikali ni CCM.

Kila mmoja kikatiba anatakiwa kutekeleza Ilani ya chama hicho kwa miaka itakayokuja mbele ikiwa vyama vya upinzani vitashinda uchaguzi kuongoza serikali, kila mtu kwa mujibu wa Katiba atalazimika kutekeleza ilani ya vyama hivyo,” alifafanua Mbwilo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom