Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Na Ahadi Mtweve
Barua ya wazi kwa Mh. Rais John Pombe Magufuli
.......Nchi hii ni tajiri sana na mwenyewe umekiri kuwa ni tajiri. Iweje tena utoe pesa zako za mfukoni,halafu ukate na za wenzako ili kununua madawati ya mkoa wa Dar es Salaam peke yake? Nchi nzima inahitaji madawati. Umetumia kigezo gani kuichagua Dar es Salaam? Kwa nini isiwe Mtwara au Manyara, au Njombe?
Kama kweli hoja ya kuchangia kwa kutoa pesa za mfukoni ni muhimu kwako Mh Rais John Magufuli, mbona umechangia kiasi kidogo sana? Yaani mshahara wako wa tsh mil 400 ukichangia mil 6 ambayo ni sawa na asilimia 1.5 ya mshahara wako mbona ni pesa kidogo sana? Na kwanini uchangie na ulazimishe wenzako kuchangia kwa nguvu wakati Tanzania ina kila kitu?
Mh Rais wangu kama ulivyojitambulisha kuwa wewe ni mpambanaji nakushauri tengeneza mfumowa serikali kufanya kwa kujitegemea kwa pesa za makusanyonya kodi na tozo nyinginezo lakini sio kwa kuchangia toka mfukoni mwako.
Kitakachotokea hapa ni wananchi walalahoi kuchangishwa mpaka hela ya kununua bomba la sindano maana watasema umechagia!
Nakushauri hizo pesa kiduchu unazotoa ungezielekeza kwa makundi maalum ya kijamii kama masaada binafsi kwa asasi zinazowasaidia hao wahitaji.........