SITUATIONAL STRESS

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
766
Reaction score
1,536
Jana tulianza kuangalia aina nne za stress kwa mujibu wa Dr.Karl Albrecht na naamini umeanza kufanya kitu kuhusiana na aina ya kwanza ya stress.

AINA YA PILI YA STRESS inaitwa “SITUATIONAL STRESS”(Stress inayosababishwa na matukio fulani maalumu katika maisha yako).Matukio haya yanaweza kuwa ni yale ambayo yako juu ya uwezo wako,emergency,kupoteza hadhi fulani,kuachishwa kazi au kusemwa vibaya mbele ya watu wengi.

Mara nyingi aina hii ya stress unaweza usiijue kama hauko makini sana.Njia nzuri ya kuigundua ni kuangalia dalili za KIHISIA na KIBAILOJIA ambazo hukutokea.Kwa mfano:Wengine wakiwa katika hali hii huwa na MASHAKA ya hali ya juu sana(ANXIETY),kuna wengine hupenda KUJITENGA na HAWATAKI kuongea na MTU na wengine hata hupata MAUMIVU ya ghalfa ya TUMBO au KICHWA.

Watu wengi wanaosumbuliwa na stress za namna hii ni wale ambao huwa wana changamoto kubwa MBILI:Moja ni kuwa wana VIWANGO VIDOGO vya ujuzi wa kutatua migogoro.Wakijikuta kwenye mgogoro badala ya kutatua huwa WANAUKIMBIA na hawatafuti SULUHISHO.

Mbili watu hawa huwa wana changamoto ya KUWASILISHA MAWAZO YAO(Communication).Wengi uwezo wao wa kujieleza ni mdogo na husababisha waendelee kukaa kimya huku WANANUN’GUNIKA moyoni kila siku badala ya Kuongea.Kujitoa katika stress hii ni kujifunza mbinu za kutatua migogoro na kujifunza kuongea kwa utulivu badala ya KUKASIRIKA hovyohovyo na kupaza sauti kila wakati (SHOUTING)..

Je,umeshawahi kukutana na stress ya Namna hii?.Angalia video kwenye link kujifunza zaidi somo hili ili leo usiishi kwa stress.


#Nanauka
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…