Sitta mzoefu wa kuvuruga Bunge?

Sitta sio malaika, ila anaweza kuwa mtu mwema japo kwa kipindi kifupi cha maisha yake. Ni yupi kiongozi aliye mwema? Mh! Majungu bwana! Mtu asitende chema, mnang'ang'ania historia. Mtu akiwa mdokozi utotoni, tumhalalishie sifa ya wizi?
 

Najibu hoja nyekundu lakini nianze kusema hivi, Mimi ningekuwa kundi la mafisadi ningewaambia wenzangu tubadili mbinu za mapambano maana kutumia magazeti ni mbinu iliyokwishagudnulika mwaka 2005. Huwezi kupigana vita yoyote kwa mbinu ileile ambayo adui yako kaishaijua.

Kwa nini Sitta hakujiuzulu uwaziri wa Sheria kuhusu G55 na suala la utanganyika? Kosa la magazeti ya mafisadi wanadhani watu hawasomi vitabu na hawana kumbukumbu.

Suala la Tanganyika na G55 lilimfanya Mwl. Nyerere aandike kitabu kiitwacho UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA. Ni kweli Nyerere aliiponda serikali na bunge kwa kukubali hoja ya Tanganyika na wale wabunge 55 (G55).

Lakini Nyerere alimsifia mtu mmoja tu ndani ya kitabu hicho naye ni Samwel Sitta, waziri wa sheria na katiba wakati huo. Kwa nini Nyerere alimsifia Samwel Sitta? Ninamnukuu Nyerere kwenye kitabu chake hapa chini kwenye aya ya kwanza alipoanza chapter ya USUGU WA VIONGOZI :

..."Jukumu la kueleza taarifa hii ya Serikali katika Halmashauri Kuu ya Taifa aliachiwa Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mheshimiwa Samuel Sitta. Baadaye, baada ya kikao, nilimtafutaNdugu Sitta, nikampa pole kwa kupewa jukumu la kueleza jambo ambalo halielezeki".

"Mapema nilikuwa nimeambiwa kwamba (Samwel Sitta) alikuwa ametamka bungeni kwamba hapo hoja ya kudai Selikali Tatu itakapoanza kujadiliwa, yeye ataipinga, maana jimbo lake la uchaguzi, Urambo, halikuwa limemtuma kwenda bungeni kudai Serikali ya Tanganyika. Wabunge wote wakweli wangeweza kusema hivyo hivyo. Hata Waziri Mkuu na katibu Mkuu wangeweza kusema hivyo hivyo. Wao ni wateuliwa na Rais, ambaye alikwisha kwenda bungeni siku chache tu zilizopita, na kupinga hoja ya Serikali Tatu. Katika kikao cha usiku wa jana yake nilikuwa nimewakumbusha hivyo viongozi wetu waheshimiwa".....Mwisho wa kunukuu.

Hivyo katika sakata zima la suala la Tanganyika Sitta anabaki kuwa waziri pekee aliyeonyesha msimamo huo ambao umetajwa na Nyerere.

Spika wa wakati huo Pius Msekwa hakusifiwa kwa msimamo ndani ya bunge au NEC. Msekwa alitajwa tu na Nyerere kwamba ndiye aliyetoboa mpango mzima wa bunge ambapo bunge lilijifanya limefunga hoja ya serkali tatu lakini kumbe kimyakimya na kijanja limeipitisha hoja hiyo kwa siri ambayo Msekwa aliitoboa kwenye vyombo vya habari. Ninamnukuu Nyerere tena hapa chini:

...Kwa sababu uamuzi wa kutaka Serikali ya Tanganyika ‘ndani ya muungano' ulifanywa na viongozi wetu kwa hila, na kupitishwa bungeni bila mjadala, sisi wengine hatukujua lililotokea. Baadaye tulifahamishwa kuwa huo ndiyo ulikuwa uamuzi wa ‘bunge zima" kutokana na kauli ya Pius Msekwa aliyekuwa msimamizi wa kikao cha Bunge kilichofikia uamuzi huo....Nadhani viongozi wetu walitaka kuendelea kuficha na kuuvuga vuga, lakini yeye akatoboa. Nasikia baadaye aliitwa akakemewa. Sijui kwa nini...".....Mwisho wa kunukuu.

Hivyo tunaona kuwa ushujaa wa Samwel Sitta hata Nyerere aliujua na aliuandika. Mwandishi wa makala hii hana kumbukumbu ya kitabu hiki kwa sababu full time anasubiri kuneemeshwa na mafisadi. Na kama hakununua kitabu hiki mwaka 1994 basi aende kwenye makumbusho pale Butiama kuna vitabu zaidi ya 8000 vya iliyokuwa library ya Baba wa Taifa Julius Nyerere.
 
Zina sound kama Siasa za maji taka hivi!!!!!!!!!!
 
Asante sana Kieleweke kuna wengi wanafikiri mbinu ya magazeti bado ina nguvu sawa kama miaka ya 80s na 90s wakati sources za habari zimekuwa nyingi na uelewa wa watu umeongezeka hicho kitabu nafikiri ni muhimu maana kuna watu humo waliitwa wahuni Nyerere aliwajua lakini bado wanang'ang'ania madaraka kwa udi na uvumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…