Tumesoma habari za Samwel Six,masurufu yake na wanawake wake.Nchi yeyote yenye morals ,tayari angeisha ondoka
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Arusha;
Tarehe: 29th September 2009
Habari Leo
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, ametangaza rasmi kuwa amejitoa mhanga kupambana na ufisadi ili nchi isiangamie.
Sitta amesema, ufisadi nchini ni wa kiwango cha juu hivyo yeye na baadhi ya wabunge wameamua kujitoa mhanga kupambana nao, na hawafanyi mzaha.
Amesema, ufisadi unatisha Tanzania, na kwamba, mafisadi wanaiangamiza nchi.
Nyinyi vijana mnakua wakati wa mikataba hii mibovu mimi naweza kuwa nimeshakufa kwa wakati huo, ndio maana baadhi ya watu wakiwemo baadhi ya wabunge wanachukia rushwa, Sitta amewaeleza waandishi wa habari leo mjini Arusha.
Rais huyo wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola amesema, gharama za ufisadi nchini zinaweza kuambukiza vizazi vijavyo.
Rushwa ni tatizo kubwa katika bara letu la Afrika, wala rushwa wanatumia utajiri wao kuingia kwenye siasa huku wakiwa na nguvu kubwa ya kiuchumi, amesema Sitta.
Ametoa mfano wa ufisadi huo nchini kuwa ni viongozi wa Serikali kusaini mikataba feki itakayoliingiza taifa kwenye gharama kubwa siku zijazo. Amesema,Tanzania itaonja machungu ya gharama hizo kupitia madeni.
Sasa tunatumia kama asilimia 35 ya bajeti kwa ajili ya kulipia madeni ya nje; lakini kuna uwezekano wa kufikia asilimia 50 kama tutaendelea kuingia mikataba feki na ikifikia hapo tumekwisha.
Ufisadi umefikia hatua ya juu ndio baadhi yetu hatufanyi utani na tumeamua kujitoa mhanga kupambana dhidi ya wahusika wa ufisadi huo.
Kwa mujibu wa Sitta, mwaka jana Afrika ilipoteza takribani dola za marekani bilioni 20 kutokana na vitendo vya ufisadi. Kiasi hiki ni kikubwa kwani ni zaidi ya msaada ambao bara hili linapata, hii ni hatari kubwa.
Sitta amesema, mkutano huo wa CPA utalijadili suala hilo la ufisadi wakati watakapokuwa wanajadili moja ya mada zitakazowasilishwa.
Amesema, rushwa ni chanzo cha migogoro mingi Afrika kwa kuwa watu wachache wana utajiri walioupata kwa njia ya rushwa, wananchi wengi ni masikini.
Kwa mujibu wa Sitta, watu wamekuwa wanakasirishwa na ustawi huo kwa watu wachache na hivyo kuwa chanzo cha mapigano na migogoro isiyokwisha katika baadhi ya nchi.
Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo, kitendo cha watu wachache kumiliki uchumi na kuwa na nguvu kubwa ya kisiasa kunasababisha watu wengi wawe masikini.
Katika mkutano huo baadhi ya mada zitakazojadiliwa ni Serikali ya mseto, majukumu ya Bunge katika kutoa habari kwa jamii, na mabadiliko ya hali ya hewa.
Bla blah blah blah blah...huyu si ndio alikuwa anapigana na kina Dr Slaa waliokuwa wanasema nchi inaangamia na kumpa ushahidi wote bado akaukataa,leo mafisadi wenzake wanataka kumtoa kwenye ulaji anajidai yuko upande wa wananchi,huyu mtu sio serious anatuchezea akili tuu
Bla blah blah blah blah...huyu si ndio alikuwa anapigana na kina Dr Slaa waliokuwa wanasema nchi inaangamia na kumpa ushahidi wote bado akaukataa,leo mafisadi wenzake wanataka kumtoa kwenye ulaji anajidai yuko upande wa wananchi,huyu mtu sio serious anatuchezea akili tuu
Tumesoma habari za Samwel Six,masurufu yake na wanawake wake.Nchi yeyote yenye morals ,tayari angeisha ondoka
Kwanza Mhe. Sitta anapaswa kumuomba msamaha Dr. Slaa kwa jinsi alivyo mpiga danadana kuhusu hoja yake binafsi juu ya mafisadi mpaka Dr. Slaa akaamua kuwithdraw hoja hiyo na kuipeleka mwembe Yanga Temeke.
Mhhhh.yangu macho,,,,,,,,nasubiri nione calculation zake,hasa
wakati wa uchaguzi,na mwanzo wa bunge lijalo.uchaguzi wa spika....
Kujitolea mhanga ni pamoja na kukubali matokeo hata kama umeshindwa....
Bla blah blah blah blah...huyu si ndio alikuwa anapigana na kina Dr Slaa waliokuwa wanasema nchi inaangamia na kumpa ushahidi wote bado akaukataa,leo mafisadi wenzake wanataka kumtoa kwenye ulaji anajidai yuko upande wa wananchi,huyu mtu sio serious anatuchezea akili tuu
Bla blah blah blah blah...huyu si ndio alikuwa anapigana na kina Dr Slaa waliokuwa wanasema nchi inaangamia na kumpa ushahidi wote bado akaukataa,leo mafisadi wenzake wanataka kumtoa kwenye ulaji anajidai yuko upande wa wananchi,huyu mtu sio serious anatuchezea akili tuu
Wacha tusubiri na kuona atajitoa mhanga vipi. Lakini kama ni Sitta yule yule wa CDA na pale TIC na madudu yake yote, sioni huo uadilifu utaanza lini?
Akipewa nafasi ya kutetea wananchi au kutetea serikali, ataenda kutetea serikali.
Labda ameenda kuungama kwa mungu na kutubu ujambazi mkubwa aliofanya huko nyuma.
Lakini vijana wengi hapa ni wapumbavu tu na wanashabikia bila kusoma historia ya mhusika. Sawa wote tunataka ufisadi uishe lakini kama viongozi wetu wenyewe ni akina Sitta, hapo tusitegemee matokeo.
ndo manake ,na alipoipeleka mwembe yanga ndo moto ukawaka mpaka leo tunaona akina Mwakyembe nao eti wanapigana na ufisadi..this country bwana is very funnyKwanza Mhe. Sitta anapaswa kumuomba msamaha Dr. Slaa kwa jinsi alivyo mpiga danadana kuhusu hoja yake binafsi juu ya mafisadi mpaka Dr. Slaa akaamua kuwithdraw hoja hiyo na kuipeleka mwembe Yanga Temeke.