Sitawatenga kwa itikadi za siasa-Pinda

tibwilitibwili

Senior Member
Sep 12, 2006
184
10
Na Reuben Kagaruki,
Rukwa

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda amewataka wakazi wa Rukwa wasitarajie kuteuliwa kwake kuwa ni kunyooka kwa mambo yao bali wachape kazi kwa nguvu ili kujiletea maendeleo na kuwaahidi kwamba hatawatenga wananchi kwa itikadi za vyama.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo mkoani hapa juzi katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku nane. "Rukwa bado iko nyuma kimaendeleo, si kweli kwamba mmepata Waziri Mkuu mambo yote yatanyooka, itawezekana iwapo mtafanya kazi kwa nguvu," alisisitiza Bw. Pinda na kusema kuwa huu ndio wakati muafaka wa kushirikiana kuleta amaendeleo.

Mbali na kutoa rai hiyo Bw. Pinda aliwataka wananchi wa Mkoa huo kujenga utamaduni wa kusameheana. "Wananchi wa Rukwa nawaombeni mshirikiane, msivutane bila sababu za msingi," alisena.

Alisema kuwa kazi aliyopewa ni nzito inahitaji ushirikiano na atakuwa tayari kulifanyia kazi jambo lolote hata kama litapelekwa kwake na mtu wa CHADEMA kwani lengo ni kuifikisha nchi pale panapotakiwa.

Akielezea vipaumbele vyake kwa mkoa wa Rukwa, Bw. Pinda alisema ni pamoja na barabara na kuongeza kuwa anashukuru Mungu ameteuliwa wakati Rais wa Marekani Bw. Bush akiwa amemwaga fedha nyingi za ujenzi wa barabara ikiwemo ya Tunduma- Sumbawanga.

Alisema ana uhakika kwamba katika kipindi cha miaka miwili hali ya miundombinu itakuwa imeanza kuboreka kutokana na eneo hilo kupewa kipaumbele na Serikali katika fedha zinazotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Alisema ana ugomvi na hilo, kwakuwa fedha zinazotolewa na mfuko huo hazikutumika ipasavyo kwa wananchi wakati zilitengwa kwa ajili ya miradi iliyoibuliwa na wananchi.

"Kuna fedha Mkoa huu tumeambia tuirejeshe makao makuu (TASAF) kwa sababu haikufanya kazi ya miradi iliyoibuliwa na wananchi," alisema.

Waziri Mkuu huyo alisema fedha hiyo inafikia sh milioni 178 na atawabembeleza TASAF ili kuona namna ya kuondoa kasoro hiyo.


_______________________________________________
 
Back
Top Bottom