Sitasahau Sekou Toure Mwanza: Dada yangu alijifungua mapacha bila msaada wa wauguzi

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Wakuu katika waathirika wa hii Hospital ni dada yangu anayeishi Mwanza eneo la Ghana. Mwaka 2013 alipoteza mapacha wawili na yeye kuponea bahati kama si kudra za mwenyezi Mungu baada ya kumhamishia bugando. SITOSAHAU.

MKASA:
Dada yangu alikuwa mjamzito na maendeleo ya watoto kulingana na clinic yalikuwa mazuri na hapakuwa na tatizo lolote, ilipofika wakati wa kujifungua alipelekwa Hospitali ya SEKOU TOURE kwa ajiri ya kujifungua, alipokelewa vizuri akiwa na uchungu km kawaida alipewa kitanda chumba cha kujifungulia huko ndiyo masaibu haya yote yalitokea.

Baada ya muda alijiskia kujifungua akawaita nurses lakini hawakujari kwaani walikuwa kwenye story zao ndefu hapo nje, baada ya kelele walifika na kumlamba vibao kuwa anawapigia kelele.

Aliwambia anataka kujifungua lakini hawakujari, baada ya nurse kutoka nje tu mtoto alitoka na kuteleza kwenye mipira iliyopo kitandani na kudondoka chini, na dada alijitahidi lakini hali yake ilikuwa tete kwani alikuwa bado anahangaika na mtoto wa pili, mtoto wa kwanza alipoteza maisha akiwa anaona huku akipambana na maisha yake na ya mtoto wa pili.

Bbaada ya muda alijifungua mtoto wa pili huku akiwa na uchovu sana alikosa msaada pia mtoto wa pili nae akafariki dunia huku akiwa amezaliwa salama.

Baada ya mama wa watoto kujifungua alitokwa na damu nyingi, na yeye kuwa katika hali mbaya, kwa kuwa hatukuruhusiwa kuingia huko chumba cha kujifungulia hatukujua yaliyokuwa yanaendelea.

Baadae tulimwagiza mama mmoja ajitahidi kujua kinachoendelea, mama mja mzito mmoja aliyekuwa ward ya wazazi alimwambia mama huyo kuwa inaonekana dada ana shida kubwa huko lab.

Akawatafuta nurses waliokuwa wakipiga story zao na vicheko na kuwaomba wamwangalie mzazi ndiyo kuinuka, loooh tuliletewa taarifa kuwa alijifungua mapacha lakini walipoteza maisha na mama yao alikuwa hali mbaya.

Tulifanya jitihada kumhamisha pale na kumpeleka Bugando ambako tulimfikisha akiwa hajitambui, tulipata huduma nzuri Bugando, baada ya siku tatu mgonjwa alipata nafuu na kutueleza tukio na SEKOU TOURE.

Tulipata uchungu na vilio tuliumia sana, ukweli Serikali ya awamu ya tano inatakiwa kuombewa sana, kuna watu wanabeza kazi ya mkuu wa mkoa Mwanza Bw Magesa Mulongo, ukweli hawajui uzembe uliopo kwenye hii Hospitali.

MUNGU AWABARIKI WOTE WANAOTENDA HAKI, MUNGU AMBARIKI RAIS WETU JPM
 
AKSANTE MODE LKN WALIFARIKI UNGEWEKA VIZURI HAPO.
 
Jamani msiwalaumu manesi kwa kila kitu. kwa sababu hata mtu anapobeba mimba manesi hawapo
Ningekuwa karibu na wewe makofi yangekuhusu! Ndo upumbavu mnaojiiifariji mkiwa kazini? Haise mshukuru Mungu umejificha nyuma ya ID feki ningependa kujua unafanya kazi gani na uwajibikaji wako katika shughuli unazofanya

Inawezana kabisa we ni Nesi lakini badilika vifo vya kizembe vinauma sana
 
duh poleni sana kwa huo mkasa dah mwenyewe roho imeniuma mbaya baada yakusoma
 
Back
Top Bottom