Jitu la-Mtumba
Senior Member
- Mar 20, 2025
- 151
- 349
Habarini wanajukwaa. Najua mpo salama mmepumzika na familia weekend tulivu kabisa, changamoto za hapa na pale ni kawaida na sitaki kuzijua.
Basi bwana siku ya leo nimeona niwape kisa cha ukweli niliyowahi kuyapotia kwa mama wa kambo miaka ya nyuma.
Nikiwa darasa la kwanza mzee alipata mchepuko uliokuja kusababisha mama na baba wakatengana mkoa wa kusini mwa Tanzania.
Mama ikabidi ametuacha kwenye nyumba sisi wawili,mimi na mdogo wangu wote wa kiume. Baba ikabidi ametupeleka kwa baba mdogo,mimi nikiwa nishaanza shule mdogo wangu bado,huku anaangalia muda wa kutuchukua tuende kuishi naye kwa mama wa kambo.
Muda haukupita sana ikabidi twende kwa baba. Mwanzo ilikuwa nyumba ya kupanga baada kama ya mwaka mmoja mzee akajenga huko tukahamia kwenye nyumba yetu. Yule mama alikuwa na watoto wawili wa nje,jumla na wa mzee wadada wa4 wanafika watoto 6,jumlisha sisi 2 tunakuwa 8.
Mwanzo maisha yalikuwa mazuri tu na yule mama akawa anatufurahia,si unajua watoto wa kusini kazi kazi,na isitoshe sisi ndiyo tulikuwa wakubwa kuliko wale wa yule mama.,
Kumbe ilikuwa mwanzo tu! Kama penzi jipya alipatavyo mtoto wa kiume zile care zisizochosha. Mimi nikawa naendelea na shule ya msingi nipo darasa la tatu yule mama akawa anatupa kazi za kukomoa mpaka majirani wanashituka. Upendeleo ukawa unaonekana,watoto wake wanavaa vizuri sisi nguo zimechanika chanika balaa,mtu akifika home lazima ajionee utofauti.
Malezi yasiyo na haki yaliendelea,mnafanya kazi zote yeye na watoto wake wamepumzika,masimango wakati wa kula,vipigo visiyoisha tena vipigo kweli!,mara ubinywe maskio na mkasi akisema hausikii anakukata sikio. Baadaye yule mama akawa anatunyima chakula asubuhi na mchana- usiku mzee akiwepo ndiyo mnakula. Tumendelea hivyo mpaka mwisho yule mama akamwambia mzee kuwa hawezi kuishi na sisi na kwakuwa tushakuwa wakubwa na tushajua kupika atupangishie nyumba. Hapo mkubwa nayesemwa ni mimi nikiwa darasa la tano na mdogo wangu akiwa la kwanza.
Kunakipindi dogo aliumwa sana,huduma ikawa ni mimi kumuogesha,kumbadilishia nguo,kumpeleka chooni na kila kitu. Baba alikuwa mtu busy anayeonekana usiku tu,habari nyingi za nyumbani akawa hazijui. Nahisi alipokea taarifa kutoka kwa majirani.
Ilipofikia sehemu ya kutupangishia nyumba mzee sasa ikabidi awasiliane na mama yetu mzazi ikibidi twende kule[sjui mzee alipigwa juju hata sielewi].
Mama kwa kuwa sisi ni wanae hakukataa,akakubali-tukapandishwa bus haoo mpaka Morogoro. Tumeendelea na shule mzee hana habari na sisi,hatoi huduma wala salamu,mpaka secondary. Nlipofika advance ndiyo nikawa nawasiliana tena na mzee na akaanza kutoa malezi kidogo,mzigo mkubwa ulikuwa upande wa mama na Babu mzaa mama. Nisiwe muongo ilifikia hatua nikawa namchukia mzee kwa kututelekeza! Toka ule muda tumetoka kwa baba hakuweza hata kuja kutusalimia mpaka nimefika chuo.
Nikiwa chuoni nikapata taarifa mzee wangu kafariki!nliumia sana,siku hiyo hiyo ikabidi nijiandae kwenda msibani sababu mimi ndiyo nlikuwa mtoto mkubwa wa kiume upande wa mzee,hapo hatujaonana toka nikiwa darasa la tano shule ya msingi.
Kufika kule nikaambiwa mzee ashazikwa! Kumbe alitengana tena na yule mama,yule mama akabeba watoto wote mzee akawa anakaa peke yake kwenye nyumba! Wale watoto wa mzee upande wa mama wa kambo wakawa wanampelekea chakula sababu yule mama alipanga siyo mbali. Baba aliumwa peke yake kwenye ile nyumba na tetesi zinavyodai ni kwamba yaweza kuwa kile chakula alichopelekewa kiliwekwa sumu maana hazikupita siku akafariki. Watu wakaja kujua baada ya siku zimepita na mwili ukawa ushaanza kuharibika.
Niikatishie hapa hii story sababu inasikitisha,
Kama mwanaume jitahidi mama wa watoto wako ndiyo anawalea,wapo mama wa kambo wazuri pia. Hii hali huwa nikiikumbuka naona wanawake ni makatili sana na nakuwa sina huruma na mwanamke yeyote