Sisi waoga

Pasta Joshua

Member
Joined
Aug 2, 2020
Posts
23
Reaction score
131
#Tukubaliane
Sisi watanzania ni waoga
Sisi watanzania tukitishwa tunakimbia,
Sisi watanzania tunataka amani,
Sisi watanzania maswala ya kuvutana hatuyajui,
Sisi watanzania kipaumbele chetu maelewano.

Yes nakubali,
Ila round hii watanzania lazima tuelewane, iwe ni mwanasiasa mkongwe, msani, blogger, mwandishi wa habari, mwanamichezo na shabiki TANZANIA IKIOZA, HUTAKUWA NA MAHALI SALAMA PAKUISHI.
#Tunajua ni chungu ila bora ifike

Tunachotakiwa ni kufanya maamzi ya kuwa na sauti moja tu, TUNATAKA UCHAGUZI HURU sisi wananchi ndio tuwe na power ya kuchangua viongozi tunaotaka.
#Tunajua ni chungu ila bora ifike

Tumechoka polisi kubeba kura fake,
Tumechoka kupigwa mabome ili kupitisha mgombea kwa nguvu.
Tumechoka fujo hizi zote,
Tumechoka vurugu hizi zote, #Tunajua ni chungu ila bora ifike

Kama nchi,
Sisi ndio wananachi,
Kama ni bandari ni zetu,
Kama ni mali zote ni zetu na vituku zetu, polisi , raisi, majeshi, mahakama zote ni mali yetu na sisi ndio maboss zao.
#Tunajua ni chungu ila bora ifike

Tunataka tume huru,
Bila tume huru, hakuna haja ya sisi kuita uchaguzi, ili linawezekana kama wote bila kujari vyama vyetu tutasema #NO REFORM #NO ELECTION
 
Wabongo ukiwaambia no election hawakueelewi ila sema no erection uone utakavyo pata engagement 🤣

Wabongo ni comedians na wacheza pono mkuu🤣
 
Sawa, ujumbe murua!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…