Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,275
Katika pitia pitia yangu nimekutana na mandiko haya katika kitabu Kilichoandikwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Chenye jina "UJAMAA"toleo la1968 ukurasa wa 14 ambao ni mwendelezo wa Sehemu ya kwanza(IMANI YA TANU) kipengele(i)Kinachosomeka.
"Kwamba ni wajibu wa Serikali ambayo ni watu wenyewe kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi wa Taifa ili kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani na siasa ya watu wote kwa kuwa sawa."
Kuna mambo ya msingi sana ya kujifunza hapo hasa hasa juu ya wajibu na uzuri wa maandiko hayo yametaja ni nani anapaswa kuwajibika kwa ustawi wa Taifa kwa kuitaja Serikali lakini bado maandiko hayo niliyonukuu yameifasiri serikali kama"watu wenyewe"ambao ni mimi na wewe na yule.
Maandiko hayo pia yametaja kingezo"siasa ya watu wote"kumbe kuna sifa au vigezo vya kuwa mwanajamii anayeendana na ustawi wa Taifa lake na yule anayekuwa kinyume na kigezo hicho.
Na Serikali sharti iingilie kati kwa vitendo ili kusimami ustawi wa Taifa na juu ya hili hakuna wa kumlaumu juu ya hali ilivyo na kumyooshea vidole wote kana kwamba yeye ndiyo sababu kuu ya hali ilivyo ila tutambue hali ipo ilivyo kutokana na Sisi kuwa tulivyo"SISI NI SABABU YA HALI ILIVYO NA TUNA WAJIBU KATIKA KUIBADILI KAMA HATUITAKI.
Bado nasoma kurasa nyingine.