Ambiele Kiviele
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 15,267
- 29,906
Tofauti yetu na mbuzi (mnyama) siyo miguu
au manyoya bali kitu kingine kikubwa zaidi.
Kitu hiki kikubwa ndicho sisi sisi ni jinsi
tunavyofikiri kwa kufikiri kwetu tunakuwa kama
tulivyo ambao nsiyo sisi wenyewe. Kila
binadamu ni kamili na hana thamani kubwa
zaidi au ndogo kuliko mwangine.
Hakuna
binadamu awezaye kuwa na thamani kubwa
kuliko mwingine hata kama atajikweza vipi,
lakini hakuna pia awezaye kuwa na thamani
ndogo kuliko mwingine bila kujali anajishusha
kwa kiwango gani.
Kwa nini? Kwa kuwa kila binadamu ni namna
anavyofikiri, ni wazi thamani ya ubinadamu
wake haipo pengine popote nje yake, ambako
ni kufikiri kwake.
Yale yote yaliyo nje ya
binadamu hayana uwezo wa kupima thamani
yake, bali yeye mwenyewe anavyofikiri na
kuamini ndiyo thamani yake.
Ina maana
kwamba thamani ya kila mmoja wetu imo
ndani mwake na hakuna anayeweza kuingoza
au kuipunguza hadi pale mwenyewe
anapotaka.
Ni uongo mtupu kudhani kwamba sisi
binadamu tunaweza kufanya au kuwa vyovyote
bila kwanza hali hizo kupitia kwenye kufikiri
kwetu.
Tukifikiri kwa njia fulani tunakuwa sisi
wa aina fulani na tukifikiri kwa njia tofauti
tunakuwa sisi tofauti. Ndiyo maana huwa
inasemwa kwamba, ’Binadamu haaminiki’.
Kauli hii inatokana na ukweli kwamba sisi tuko
ndani mwetu na ni vigumu kwa mtu mwingine
kujua sisi tuko vipi kwa wakati gani hata pale
anapoona vitendo au mambo ambayo
yanatokana na kufikiri kwetu.
Lakini bila shaka sisi siyo kufikiri tu na mambo
yote kuishia hapo. Ni wazi kabisa kuwa kama
sisi ni kufikiri hatuna budi kujiuliza ni sisi wa
aina gani, kwa sababu kufikiri hakuko kwa aina
moja. Na hii ndiyo tofauti yetu binadamu.
Kila
mmoja kati yetu amezaliwa na kulelewa katika
mazingira tofauti, amekulia katika mazingira
tofauti, amepata uzoefu tofauti wa kimaisha.
Hivyo hata kufikiri kwetu ni Lazima kutakuwa
ni tofauti, kwani kufikiri kwetu kwa kiasi
kikubwa ni zao la mambo hayo.
Bahati mbaya sana hata hivyo, tulio wengi
huwa hatujui kuwa tunafikiri, kama ilivyo katika
kupepesa macho au kupumua, mambo ambayo
ni muhimu sana kwa maisha yetu, huwa
hatujui kwamba tunayafanya hadi
tukumbushwe.
Wengi wetu tunaweza kushtuka
wakati huu tunaposoma mada hii, kwamba
tunapumua au kupepesa, ndivyo ilivyo kwenye
kufikiri. Wengi wetu huwa hatuna habari
kwamba tunafikiri hadi tukumbushwe kama
sasa hivi.
Kwa kuwa sisi ni kufikiri kwetu, ina
maana basi kwamba huwa hatujijui, tunaishi
tukiwa hatujui kama tunaishi.
Matokeo ya jambo hili yamejaa kila mahali.
Kuna kujuta kwingi kila siku na kusema,
‘Ningejua’ zisizokwisha, kuna kukwaruzana
ambako hakuna maana, kuna tamaa
tunazodhani hazizuiliki, kuna kushindwa kujua
ni kwa nini tunatenda jambo fulani au
hatulitendi na kuna kulalamika kusikoisha na
hofu na mashaka makubwa.
Ni vigumu kwetu
kuishi kama tunavyotaka wakati hatujajua hasa
sisi ni akina nani.
Tunaongozwa na miili yetu
na vile vilivyo nje ya miili hiyo, kwa kudhani
kwamba sisi ni miili au vitu hivyo vingine.
Hebu sasa tufahamu na kukubali kwamba sisi
ni kufikiri kwetu, yaani tunakuwa vile
tunavyofikiri.
Kama tumekubaliana na hilo,
hebu tujiulize, kufikiri kwetu kukoje.
Tunaposema kufikiri kwetu kukoje, tunakuwa
na maana kwamba, mawazo au fikira
zinazopita vichwani mwetu hutufanya tutende
au kuhisi vipi, ambapo ndiyo tunakuwa sisi.
Jinsi unavyojiona na kuamini ulivyo ndivyo
utakavyofanya maamuzi na kuchukua hatua ya
maisha yako kwa kujiangalia hivyo.
Binadamu
ni kiumbe anayehangaika huku na kule kutaka
kuyafikia malengo fulani duniani, tangu azaliwe
mpaka atakapoondoka maisha yake yamekuwa
katika mfumo wa kutafuta kuyafikia malengo
fulani lakini kutokana na mazingira, hali, watu,
mambo anayoyasikia na kuyasoma na mifumo
ya maisha fulani humfanya akubali maisha
fulani kwa mipaka fulani anayoamini yeye na
kujiwekea yeye mwenyewe na si kuwa ndivyo
alivyo.
Hivyo basi hujikuta kuwa anayoyaamini na
kuyakubali ndiyo hayo anayoyaishi na hubaki
kama hivyo.
Lakini katika kukubali kwake
kuhusu yeye alivyo haimaanishi ndiyo hivyo au
ndivyo anavyoweza kwasababu anayoyaishi ni
yale anayoyaamini kuhusu yeye na yamekuwa
kweli kwake.
Niliwahi kuandika huko nyuma kwamba,
binadamu ni zaidi ya mwili wake ni zaidi ya
damu yake ni zaidi ya nyama yake na
hakuumbwa kuishi kwa kuangalia hivyo na
tunapoangalia uwezo wake binadamu
hatuangalii ukubwa wa mwili wake, kichwa
chake, miguu yake au hata ulemavu wake bali
tunaangalia zaidi katika mfumo wake wa
akili,vipaji na imani yake kuhusu uelewa wake
wa ndani kuhusu yeye mwenyewe.