Siri Kali Chumbani Mwangu
Serikali iko ndani mwangu,
Inapanga jinsi ya kulea wana wangu,
Vijiko vya sukari jikoni kwangu,
Hata aina ya fikra za mke wangu.
Sera kali zote dhidi yangu,
Hakuna tena faragha ya kuwa mtu wangu.
Uhuru sasa si wangu,
Bali kauli mbiu moja,
Hakuna kosa dhidi ya kiongozi wangu.
Hata sala sasa si kwa Mola wangu,
Maana woga wa moyo umeandikwa kwenye Katiba yangu.
Suruali kali lazima iwe na rangi ya chama changu,
Hakuna tena “mimi” bali “watu wangu.”
Watawala wapaa juu zaidi ya haki zangu,
Wananchi ni watumwa wa wenye nchi yangu,
Wameteka hata uhuru wa majonzi yangu.
Maana Serikali ni mimi limbukeni wa nchi yangu.
Watawala wanataka kufunga moyo wangu,
Wakifundisha jinsi ya kupenda nchi yangu,
Ukoloni sasa unakaa machoni mwangu.
Aisee, aibu kali…
Siri za chumbani mwangu,
Zimekuwa sera za serikali yangu.
Serikali iko ndani mwangu,
Inapanga jinsi ya kulea wana wangu,
Vijiko vya sukari jikoni kwangu,
Hata aina ya fikra za mke wangu.
Sera kali zote dhidi yangu,
Hakuna tena faragha ya kuwa mtu wangu.
Uhuru sasa si wangu,
Bali kauli mbiu moja,
Hakuna kosa dhidi ya kiongozi wangu.
Hata sala sasa si kwa Mola wangu,
Maana woga wa moyo umeandikwa kwenye Katiba yangu.
Suruali kali lazima iwe na rangi ya chama changu,
Hakuna tena “mimi” bali “watu wangu.”
Watawala wapaa juu zaidi ya haki zangu,
Wananchi ni watumwa wa wenye nchi yangu,
Wameteka hata uhuru wa majonzi yangu.
Maana Serikali ni mimi limbukeni wa nchi yangu.
Watawala wanataka kufunga moyo wangu,
Wakifundisha jinsi ya kupenda nchi yangu,
Ukoloni sasa unakaa machoni mwangu.
Aisee, aibu kali…
Siri za chumbani mwangu,
Zimekuwa sera za serikali yangu.