Duniani kote serikali huwa zinatengeneza mfumo wa kuwa na siri kwa dhana kwamba siri ndiyo huendesha kwa ufanisi masuala yahusuyo tawi la utawala (Executive Branch). Wakati Bunge hupenda kuendesha mambo yake kwa uwazi ama nusu uwazi (Behind the closed door) mfumo unaotumiwa pia na mahakama, tawi la utawala (Serikali) wao hupenda kuwa na siri.
Waziri wa utumishi wa umma Angela Kairuki amewahi kusema kwamba mtumishi wa umma (Serikali?) atakayetoa siri atakiona cha mtema kuni. Lakini Siri kwa serikali na ukomo wa siri hizo hutofautiana kati ya nchi na nchi kutokana na mtizamo wa nini hasa ni siri kwa serikali husika.
Kuna nchi kadhaa zimeweka sheria na miongozo inayotumika kutambua siri za serikali, na sheria na miongozo hiyo inafahamika kwa wananchi wengi kama sio wote.Hapa Tanzania nadhani siri ni Mhuri unaokuwa kwenye ofisi husika na wala si muongozo wa kuweka siri. Hakuna muongozo wa nini hasa ni siri badala yake kila ofisa mwenye mhuri ulioandikwa "SIRI" anagonga kwenye nyaraka mbali mbali na kuzigeuza kuwa ni siri.
Matokeo yake jamii inaamini kila nyaraka iliyoko kwenye ofisi za Serikali ni siri na haitakiwi itumike kwa manufaa ya umma. Nimewahi kuona hotuba ya Mkuu wa Mkoa mmoja ikiwa imegongwa mhuri wa siri, ni kashangaa sana!! Ni kawaida wanasiasa kupenda kila jambo walifanyalo liwe siri lakini ni kweli kwamba kila wayafanyayo ni siri? Leo ukiuliza mshahara wa rais unaambiwa ni siri!