Siri ya white house

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
SIRI YA WHITE HOUSE MAREKANI.

Karibia siku nzima nilikuwa nimekaa mbele ya televisheni kushuhidia hatua kwa hatua tukio la kihistoria la kuapishwa kwa Rais wa 45 wa Marekani ambaye anakuwa ndiye Rais wa kwanza wa nchi ambaye hana historia ya kuwa mwanasiasa hata kuwa "mwenyekiti wa mtaa" au kutumikia jeshi la Marekani.

Baada ya Rais Donald John Trump kumaliza kutamka maneno 35 ya kiapo cha kushika ofisi ya Urais maneno ambayo yanaishia na sentensi inayosema "... so help me God!" Karibia watu laki tisa waliokusanyika Capitol Hill kushuhudia tukio hili la kihistoria walilipuka kwa shangwe na vifijo kuwa sasa ni rasmi Trump amekuwa Rais.

Lakini binafsi yangu, mara baada ya Trump kumaliza kutamka maneno hayo ya kiapo, wazo moja tu likanipitia kichwani mwangu; "kwahiyo now Trump has the nuclear codes"!!

Katika kipindi chote cha kampeni watu kadhaa wazito akiwemo mama Clinton na hata Rais Obama wamekuwa wakikaririwa wakisema kuwa "Trump hana utashi, busara wala utulivu wa ndani wa kumfanya aaminiwe kupewa 'nuclear codes'".
Maneno hayo yalikuwa yakirudiwa mara kwa mara kiasi kwamba yakawa kama wimbo kwamba "Trump sio mtu wa kuaminika na kuuweka ulimwengu wote rehani kwa kumkabidhi nuclear codes"

Sasa swali la kujiuliza, je hofu hii yote ni kwasababu gani?? Na je, baada ya kuapa ameshapewa hizo 'codes' au bado?? Na je hizo 'codes' ni kitu gani haswa??

Ni kwamba, wakati ambapo jana watu wote akili yao ilikuwa ikisubiria tukio kubwa la kuapishwa kwa Trump na labda wale wenye kupenda kufuatilia habari walifurahia kuangalia jinsi Familia ya Trump ilivyowasili Washington, walivyohudhuria ibada kanisani pale DC, na baadae kujumuika na familia ya Obama kupata kifungua kinywa Whitehouse lakini watu wengi hawafahamu moja ya tukio muhimu zaidi lililofanyika jana ambalo hili haliwezi kurushwa CNN, BBC, Fox au chombo chochote kile cha habari ingawa naamini walikuwa wanajua.

Mnamo majira ya saa tatu asubuhi ndani ya ikulu ya Marekani kilifanyika kikao maalumu amabacho kilihudhuriwa na Rais Barack Obama, Rais Mteule Donald Trump, Makamu wa Rais Joe Biden na Makamu wa Rais Mteule Mike Pence na kikao hiki kilisimamiwa na kamandi maalumu ya jeshi la marekani inayoitwa Strategic Command ambao ndio wanaosimamia sehemu zote za siri zenye kuhifadhi silaha za Nuclear (Strategic Nuclear Arsenal). Pia kikao hiki kilikuwa na muwakilishi wa ofisi ya jeshi ndani ya White House (Whitehouse Military Office).

Kikao hiki kilihusu makabidhiano ya "nuclear codes" kutoka kwa Obama kwenda kwa Trump.

Miaka ya nyuma Rais mpya alikuwa anapewa hizi codes Mara baada ya kuapishwa lakini mwaka 1973 utaratibu huu ukabadilishwa ambapo kabla ya Rais mpya kula kiapo kinafanyika kikao cha siri ambacho Rais Mteule anakabidhiwa nuclear codes.

Swali, je hizi codes ni kitu gani?? Ni kama namba ya mpesa au tigo pesa au atm ambayo unakuwa umeikariri kichwani??

Jibu ni kwamba, hizi tunazozisikia zikizungumzwa kila siku "nuclear codes" ni msululu wa vifaa maalumu vya kijeshi vinavyomuwezesha Rais wa Marekani kutumia uwezo wake kama Amiri Jeshi mkuu kufanya shambulio la kinyuklia pale anapoona inafaa kufanya hivyo.
Na ukisikia wanaongelea "nuclear codes" ni kwamba wanaongelea mkoba maalumu ambao mda wote unakuwa umebebwa na Mwanajeshi wa Marine sehemu yoyote ile ambayo Rais wa Marekani anakuwepo.

Sehemu yoyote ile ambako Rais wa marekani anakuwepo ndani ya nchi yake au nje ya nchi.. Mtaani au whitehouse, yaani popote pale alipo..
Watu wengi huwa wanaelekeza akili yao kushangaa wale 'secret service', but next time jaribu kupepesa macho (hata kama unaangalia kwenye TV) utaona kuna Mwanajeshi amevaa sare za Marine (au mara chache sana anavaa suti) amebeba mkoba mweusi uliotuna. Huu mkoba wenyewe wanauita "The Football" na ndani yake ndimo kuna "nuclear codes" na nyenzo nyingine muhimu za kumuwezesha Rais kufanya shambulio la nyuklia.

Ndani ya huu mkoba unaoitwa "The Football" au kama unavyojulikama kwa jina rasmi la kiofisi "The Presidential Emergency Satchel" kuna vifuatavyo;

- kuna kifaa kinafanana kama na laptop
- kuna simu ya kijeshi ya satelaiti
- kijitabu kama kipeperushi chenye maelezo ya namna ya kutumia vifaa vyote ndani ya The Football
- kuna kijitabu chenye maelezo ya hatua za kijeshi na sehemu za kuzilenga kwa mashambulio (retaliatory options)
- kuna kadi ya pembe nne kama kadi ya benki yenye namba za siri. Hii kadi maarufu inaitwa "The Biscuit".

Sasa ikitokea Rais anataka kutumia nyuklia kushambulia mahali fulani.. Huu mkoba unafunguliwa kisha kitufe maalumu kinabonyezwa ambacho inatuma taarifa maalumu inayoitwa "watch alert" kwenda kwa kamati ya Majemedari wa Vikosi vya majeshi ya Marekani (Joint Chiefs of Staff). Na wao wanamshauri Rais namna bora ya kutekeleza shambulio hilo.

Hapa niseme kwamba huu ushauri wa hawa Joint Chief of Staff ni protokali tu kwani Marekani inao mpango maalumu wa kijeshi unaoonyesha namna ya kufanya shambulizi lolote la nyuklia kutegemea na lengo lolote ambalo Rais atakuwa nalo. Mpango huu unaitwa OPLAN 8010 (zamani ilikuwa inaitwa Single Integrated Operational Plan) ndio hii ipo kwenye kile kijitabu kimoja wapo nilichoeleza hapo juu kuwa kipo ndani ya The Football.

Baada ya hapo The Football inatuma signal kwenda National Military Command Center ambayo itampa Rais 'access' ya mizinga yote ya nyuklia ipatayo 4,500.

Baada ya hapo kwa kutumia kile kifaa kama laptop ndani ya The Football atachagua 'location' anayotaka kuishambulia na kisha ataingiza 'codes' zilizopo kwenye kile kikadi kinachoitwa The Biscuit. Na baada ya hapo, booooommb.!! Shambulio linakuwa limetekelezwa.

Nchi nyingine pia zenye nguvu kubwa za kijeshi kama Urusi na China pia wameiga mfumo huu.

Hiki nilichoeleza ndizo "nuclear codes" ambazo walikuwa wanapiga kelele Trump asipewe. Lakini mpaka hivi tunavyoogea tayari anazo na mwanajeshi wa Marine anambebea huo mkoba kila Trump alipo, kwa sababu yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu kwa sasa.

Mizinga hii 4,500 ya nyuklia ina uwezo wa kuisambaratisha dunia yote kama ikirushwa sehemu tofauti tofauti za dunia, na ndio maana mara baada ya Trump kumaliza kile kiapo cha Urais cha maneno yale 35 pekee.. Na kumaliza kwa ile sentensi maarufu ya kwenye kiapo "…. so help me God!", Trump amekuwa ndiye binadamu mwenye nguvu zaidi kwa sasa juu ya huu uso wa dunia.
ANGALIZO
Makala hii ni copy kama ilivyo kutoka katika ukurasa wa fb wa bwana Petro Magoti
 
Hahaa!..Hii ishaletwa bwana.. Subiri ulete nyingine kutoka huko kwenye group lenu la whatsapp.
 
na kwanin achukue story ya mtu mwingine kwenye group na kuileta jf..ni umbumbumbu tu..tengeneza yako mkuu
 
na kwanin achukue story ya mtu mwingine kwenye group na kuileta jf..ni umbumbumbu tu..tengeneza yako mkuu

Mkuu dhumuni la forum ni kuelimishana kwa hoja na si vinginevyo

Nimeiona makala hiyo sehemu
Nikaipenda, na kuamua kuileta humu
Iweze kusomwa na wengine pia,
Waweze kuchangia wanachokijua zaidi ya hapo

Ndio maana mwisho kabisa nimeeleza nilipoitoa
Badilisha mindset yako
Great thinkers hawana mtazamo kama wako
 
Asante kwa taaluma, binafsi naona kina Hilary kumshambulia kwa kupewa urais Trump ni siasa tu lakini ukweli ni kwamba sasa yeye ndio Amiri jeshi.

Kiduku naona watakula nae Burger pamoja badala ya vita.
Trump yupo kibiashara zaidi
 
Back
Top Bottom