Cha kushangaza sasa:
Kama vazi hili linavaliwa maeneo ya siri kwa nini linawekwa marembo (hasa kwa wenzetu)/ya nini kuvaa za thamani kubwa.....kwa faida ya nani?
mitishamba, kunakovaliwa chupi si mahali pa siri, ila tu labda position viliko hivyo viungo, vinakufanya wewe uone kama ni mahali pa siri, ni kama kwapa liko ndani ndani huku lakini haimaanishi kuwa liko sehemu ya siri! otherwise ingekuwa siri usingekuwa watu beach wanaoga na vichupi
tena ikiwezekana chupi inabidi ilowekwe na sabuni ya unga na maji ya uvugu vugu then unazifua na kuanika nje kwenye jua kali kama nguo nyingine tu, sema wengi wetu unakuta chupi nyeusi, kijani , njano looh nyeupe za kuhesabu.
Hili vazi linashangaza kweli!
Dukani linauzwa hadharani.
Wakati wa kununuliwa linanunuliwa kwa siri.
Wakati wa kuvaliwa linavaliwa kwa siri na linavaliwa sirini.
Linaficha siri.
Linafuliwa na kuanikwa kwa siri.
Linapochakaa linatupwa kwa siri.
Uchafu unavyozidi, na siri inaongezeka
Ndio unakuta chupi inafichwa hadi kusikofichika -
mvunguni kama anavyosema huyo Billionaire hapo juu!
Aina ya chupi nazo huongeza siri....
chupi-kamba.... nayo ni siri?
Chupi iweke safi, anza na wewe mwenyewe kuwa msafi,
tibu mafangasi yako na zuia maambukizi mapya,
Fua na anika kwenye mwanga siyo chini ya godoro.
Hili vazi linashangaza kweli!
Dukani linauzwa hadharani.
Wakati wa kununuliwa linanunuliwa kwa siri.
Wakati wa kuvaliwa linavaliwa kwa siri na linavaliwa sirini.
Linaficha siri.
Linafuliwa na kuanikwa kwa siri.
Linapochakaa linatupwa kwa siri.