Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
Kwa ufupi
CCM, ambayo hufanya chaguzi zake kila baada ya miaka mitano, imeanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wapya kutokea ngazi ya shina, lakini mabadiliko ya katiba yaliyofanywa hivi karibuni na sera za uongozi wa sasa yameufanya uchaguzi huo kukumbwa na changamoto, hasa ya wanachama kugombea nafasi za ngazi ya chini.
Uchaguzi wa viongozi wa CCM katika ngazi ya shina na matawi umekumbwa na tatizo la wanachama kutojitokeza kugombea, hali ambayo baadhi ya wadau wamesema imesababishwa na nafasi hizo kutokuwa na umuhimu na kutokuwa na posho.
Awali ngazi ya kwanza ilikuwa ya mjumbe wa nyumba kumi, lakini sasa imekuwa shina ambalo kila moja linatakiwa kuwa na watu angalau 50. Pia, sera ya sasa ya uongozi inataka mwanachama kuwa na nafasi moja ya kiutendaji badala ya kofia mbili. Licha ya mchakato wa uchukuaji wa fomu kuanza wiki kadhaa katika ngazi ya shina na kata, ni wanachama wachache waliojitokeza kiasi cha kuwafanya baadhi ya viongozi kuwafuata watu wanaoamini kuwa wanafaa na kuwashawishi kujitokeza kugombea.