Sipendi ingawa ni mrembo na anapesa

Sipendi ingawa ni mrembo na anapesa

Panthera 1

Member
Joined
Dec 30, 2014
Posts
50
Reaction score
9
Habari zenu ndugu zangu,

Ashukuriwe Mungu muumba mpaka hapa tulipofika. Mimi ni kijana wa miaka 26 ambae leo nimeamua kuja kuomba ushauri kwenu kwani nipo njia panda na sielewi kipi cha kufanya. Nilikuwa na mpenzi wangu mmoja ambae nilimpenda kwa moyo wote, nilimuonyesha mapenzi yote lakini leo hii ameamua kunisaliti na kwenda upande mwingine huku tayari tulikuwa katika ahadi za kuoana.Siku chache zilizopita kuna rafiki yangu ambae alinieleza kuhusu mambo ya mpenzi kuwa ni msaliti.

Lakini sikutaka kumkubalia hilo. Rafiki huyo aliendelea kunisisitizia kuwa mpenzi wangu siyo muaminifu lakini nami nilikataa ila leo nimeamini baada ya kushuhudia hayo niloelezwa. Mpaka sasa moyo wangu unauma, najihisi kuwa mgonjwa kabisa kwa kuwaza kilinitokea, sina raha na ninaona dunia nzima ni chungu. Ila nako katika hali ya kushangaza sikuchache baada ya mpenzi wangu kunisaliti, alitokea msichana mwingine mzuri tu na kudai ananipenda.

Ukweli mimi simpendi ingawa ni mrembo na anapesa. Mpaka muda huu sijampenda msichana huyo wala sikuwahi kumpenda. Je nimpende kwa sababu nimesalitiwa au nimpende kwa ajili ni msichana mwenye hela? Kweli sijampenda wala sitaki kutumia pesa zake hata kidogo, ila yeye ananipenda.
Nipo njia panda, nakumbuka hata familia yangu iliwahi kunambia kuwa mpenzi wangu hafai lakini mimi nilimng'ang'ania kwa kuwa tulipendana tangu utoto.

Nifanyaje ndugu zangu?

Aonywaye akashupaza shingo...............

Sawa ndugu ila sababu ambayo iliifanya familia yangu kumkataa mpenzi wangu ni tofauti ya dini tu,kitu ambacho nilitumia muda mwingi kuwaelewesha.
Sikuona kama hiyo ilikuwa sababu ya kuvunjika mahusiano yangu na mpenzi wangu.
 
Kwanza hakuna kitu kinachoitwa usaliti kwa watu wenye mahusiano yasiyo ya uchumba au ndoa.

Je mtu kama wewe umesalitiwa kwa mkataba upi ulio rasmi baina yenu?

Mwenzako katafakari na kugundua kuwa kwake huna nafasi na kachukua hamsini zake...

Pili, unatuambia kuna mwanamke mpya akupendaye lakini wewe moyo wako upo kwingine...

Sikiza kijana mapenzi ni ya wawili ingawaje dunia ya sasa wapo wanaodai kuna kujifunza kupenda...

Wahenga wanasema penda unapopendwa, hivyo hata wewe una jukumu la kupenda pia...
 
Panthera 1

Umesema humpendi ingawa ni mrembo na ana pesa. At the same time unatuuliza UMPENDE kwa vile anapesa?! Inaonyesha upendo wako ni kama bulb ya umeme,unaamua tu unawasha na kuzima!

Nafikiri swali lako lingekuwa 'je niwe naye kwasababu ya pesa zake'? Kama pesa ndio kila kitu kwako go ahead.
 
Last edited by a moderator:
Angalia sana kijana usije ukaishia kuwa mtumwa wa mapenzi umbu achana nayo fanya mambo yatayo kusaidi maisha yako tafuta mwanamke mwenye mapenzi ya kweli nasio utafutwe utaumia tene weshobokea besa uone radha yake
 
angalia sana kijana usije ukaishia kuwa mtumwa wa mapenzi umbu achana nayo fanya mambo yatayo kusaidi maisha yako tafuta mwanamke mwenye mapenzi ya kweli nasio utafutwe utaumia tene weshobokea besa uone radha yake

Nimekuelewa sana ndugu.
 
Nipe namba za uyo aliyekusaliti nimchambe hapa hadi akome
 
  • Thanks
Reactions: amu
sawa ndugu ila sababu ambayo iliifanya familia yangu kumkataa mpenzi wangu ni tofauti ya dini tu,kitu ambacho nilitumia muda mwingi kuwaelewesha.
Sikuona kama hiyo ilikuwa sababu ya kuvunjika mahusiano yangu na mpenzi wangu.

Pole sana
 
Panthera 1

soma tution kwanza na maliza shule mtu uko form three unaleta ujinga humu
 
Last edited by a moderator:
Alafu umepewa sadaka hujaenda ibadani umenunua bundle. Em kazania tuition dogo.
 
Kama umesalitiwa ni vizuri kujipa muda ili uweze kurudi hali ya kawaida. Maamuzi yoyote yenye lengo la kulipiza ni sawa na kunywa sumu ukifikiri itamuua mbaya wako. Kaa tulia. With time utapata mwingine. La kujiuliza ni kwamba kabla ya kumpenda huyo alikusaliti hamkuwa mnajuana na vivyo hivyo upo uwezo wa kumpata mwingine ambaye kwasasa hamjuani.
Ikitokea ukapata mwingine usisharau ushauri unaopewa kuhusu mienendo ya mpenzi wako. Mara nyingi kwenye mahusiano ukiona watu wanafikia hatua ya kukueleza mwenendo wa mpenzio inakuwa imefika hatua mbaya ingawa wewe unaweza usijue. Mara nyingi watu huwa hawataki kuwa chanzo cha ugomvi ndani ya mahusiano.
 
Kwanza hakuna kitu kinachoitwa usaliti kwa watu wenye mahusiano yasiyo ya uchumba au ndoa.

Je mtu kama wewe umesalitiwa kwa mkataba upi ulio rasmi baina yenu?

Mwenzako katafakari na kugundua kuwa kwake huna nafasi na kachukua hamsini zake...

Pili, unatuambia kuna mwanamke mpya akupendaye lakini wewe moyo wako upo kwingine...

Sikiza kijana mapenzi ni ya wawili ingawaje dunia ya sasa wapo wanaodai kuna kujifunza kupenda...

Wahenga wanasema penda unapopendwa, hivyo hata wewe una jukumu la kupenda pia...

Eeee mie nimependa hapo aliposema mzuri na ana pesa....
Labda anisaidie mtoto wa kiume kusema anapendwa na mdada mwenye pesa inamsaidia nini?
 
Kama umesalitiwa ni vizuri kujipa muda ili uweze kurudi hali ya kawaida. Maamuzi yoyote yenye lengo la kulipiza ni sawa na kunywa sumu ukifikiri itamuua mbaya wako. Kaa tulia. With time utapata mwingine. La kujiuliza ni kwamba kabla ya kumpenda huyo alikusaliti hamkuwa mnajuana na vivyo hivyo upo uwezo wa kumpata mwingine ambaye kwasasa hamjuani.
Ikitokea ukapata mwingine usisharau ushauri unaopewa kuhusu mienendo ya mpenzi wako. Mara nyingi kwenye mahusiano ukiona watu wanafikia hatua ya kukueleza mwenendo wa mpenzio inakuwa imefika hatua mbaya ingawa wewe unaweza usijue. Mara nyingi watu huwa hawataki kuwa chanzo cha ugomvi ndani ya mahusiano.

Asante sana,nitauzingatia sana ushauri huu.
 
Umesema humpendi hunanhaja ya kuwa naye kama unataka basi itakuwa kwa ajili ya pesa zake utajiongezea tatizo badala ya kuondoa.......kwa sasa endelea kuuguza moyo hayo mengine baadae
 
Back
Top Bottom