GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Kama kawaida yangu penye kupongeza napongeza hasa bila kujali kama linahusu Chama changu cha CCM au Wapinzani CHADEMA, CUF na ACT na vile vile huwa sibakishi au simkawizi Mtu au Taasisi pale inapofanya jambo baya ao bovu.
Kwa takribani wiki moja sasa kumekuwa kuna TAASISI fulani ambazo zimekuwa zikirudisha Chenji zao kwa Msubi ili pengine kuonyesha uwajibikaji wao Kwake na labda asiwatumbue na wao.
Cha kushangaza, kusikitisha kama pia siyo kupandisha hasira hizo taasisi za mwanzo ambazo zimerudisha hizo Chenji kwa Msubi ndiyo TAASISI ambazo zinalalamikiwa mno na Wananchi katika suala zima la RUSHWA na UONGOZI / USIMAMIZI mbovu.
Hivi ni nani asiyejua kuwa TAKUKURU na MAHAKAMANI kuna matatizo ambayo hadi leo hayajatafutiwa UFUMBUZI? Kuna KESI ngapi ambazo tayari zina USHAHIDI wa kutosha lakini TAKUKURU " wameuchuna " tu? Kuna SHUTUMA ngapi za unyimwaji wa HAKI na KESI nyingi kupigwa tu Kalenda bila hata sababu za msingi huko MAHAKAMANI?
Jamani Watanzania tusitake kutafuta UMAARUFU wa kujifanya ni WATENDAJI WAZURI na MAKINI kwa Kipenzi chetu Msubi kwani mnaweza mkadhani mnamlaghai kwa USANII na UJANJA UJANJA wenu lakini kumbe mkawa mnampoteza katika mikakati yake ya kuiletea maendeleo nchi hii.
Nilikuwa na wazo kwenu TAKUKURU na MAHAKAMA ambao kimsingi tayari mmesharudisha Chenji zenu kwa Msubi. Hivi kwa mfano mngerudisha zile Chenji zenu kwa Msubi kimya kimya isingetosha? Kama lilikuwa ni suala tu la Taasisi zenu na Msubi kulikuwa na haja au ulazima gani wa kutaka publicity?
Hivi TAKUKURU na MAHAKAMA hizo bidii zenu za kuhakikisha kuwa matumizi yenu ya Pesa yanaenda sawa sawa mngezihamishia katika kuwakamata WALA RUSHWA na KUHUKUMU leo isingekuwa mmetoa msaada mkubwa wa Kiutendaji kwa Msubi na Wananchi kwa ujumla?
Natambua sana na naunga mkono mno juhudi na jitihada za Msubi katika campaign yake ya " anti - corruption drive " ila binafsi sioni TIJA ya kutafuta UMAARUFU au SIFA kwake kwa maslahi ya kulinda ajira zenu.
Nadhani TAKUKURU mngeenda kwa Msubi kumpelekea majina ya WALA RUSHWA wakubwa wa nchi hii na Wahalifu wengine wa KIUCHUMI wa nchi yetu lingekuwa ni jambo jema mno huku pia MAHAKAMA nanyi badala ya kwenda kwa Madaha kama ya Twiga kurudisha Chenji yenu kwa Msubi basi mngetumia fursa ile kumpelekea Mheshimiwa majina ya Mahakimu au Majaji walarushwa na wabadhirufu wanaochelewesha Haki kwa wanaostahili na kupendelea wasiostahili kwani kwa kufanya hivi hamtakuwa mnamsaidia tu Msubi bali Taifa kwa ujumla na Wananchi watakuwa na imani kubwa nanyi huku nchi ikienda.
Mwisho kabisa nitoe RAI kwa wale wasaidizi wote wa Msubi kuwa jitahidini kwanza KUJIRIDHISHA KIITIFAKI katika matukio ambayo huwa mnamuandalia kwani kusema ukweli kuna mengine huwa kama vile " mnamchoresha " na kumfanya aonekane tofauti Kiutendaji na wale waliokuwa na imani na matumaini nae.
Nawalaumu nyie Watu wa ITIFAKI kwakuwa nyie ndiyo mnaratibu taratibu zote za Kiratiba za Msubi na matukio yake na nadhani inawezekana tukawa pengine tunamlaumu Msubi kumbe kiuhalisia nyie wana Protocal ndiyo TATIZO kama siyo JIPU kabisa. Kwa Mtu mwenye AKILI kubwa, nyingi na pana ni jambo la aibu kama siyo la kuudhi kwa TAASISI tena KUU ambazo zinaharakisha kutaka SIFA wakati huku nyuma katika hizo hizo TAASISI zao hali ya Kiutendaji ni mbaya na inasikitisha.
Nina mengi ya " kutiririka " ila kwa sasa naomba nianze na haya. Hata hivyo naunga mkono jitihada ambazo kwa sasa zinafanywa na TAKUKURU na MAHAKAMA katika kuleta UFANISI katika taasisi zao ukilinganisha na huko nyuma lakini bado mna majukumu makubwa mno mbele yenu kwani HAKI na MASLAHI ya Watanzania yapo kwenu na nimwombe pia Msubi kuwa asipende sana publicity katika utendaji wake na badala yake publicity yake itakuja tu automatically pale ambapo atakuwa anatenda yale ambayo aliwaahidi Watanzania kwani sisi Watanzania tukiridhika na anayotufanyia kitendo tu kile cha kuhadithiana basi hiyo inatosha kuwa publicity Kwake na wala haitaji kuita press mara kwa mara. Bado nina imani na Msubi na sijajutia kumpa KURA yangu ila niliyoyasema hapo ayatizame kwa jicho la tatu na niliowasema msichukie badala yake nishukuruni kwani nina " Jicho " la dhahabu ambalo mkilitumia vizuri litawasaidieni sana.
HAPA KAZI TU na MBELE KWA MBELE!