Sioni fundi wa kuumaliza upinzani nchini!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kama kuna mafundi ndani ya CCM wa kuumaliza upinzani ilikua ni CCM ya awamu ya nne, zilitengenezwa technical teams za kila aina lakini zilikwama. Kuna wengine walitengenezewa kesi za ugaidi lakini walichemsha.

Leo tutegemee CCM isiyokua na mikutano, isiyopitia kila kona ya nchi kukagua utekelezaji wa ilani yake ndio iue upinzani? Hii itakua ni sawa na kuota ndoto huku uko barabarabni unatembea.

Wanaotegemea kuumaliza upinzani wa sasa wanategemea zaidi kutumia nguvu badala ya akili nyingi kwa kuwabana. Hoja huuawa kwa hoja na sio kuua hoja kwa mabavu, zaidi utazidi kuibua hoja mpya.

Mategemeo ya wengi yalikua ni kwamba upinzani ungekwwisha kwa kumalizwa na kutatua shida za wanamchi, inamaana serikali nchini ya CCM wakitatua matatizo ya wananchi ndio wananchi watawakataa wapinzani na ndio utakua mwisho wao.

Ona sasa kila Mwananchi analalamika, maisha magumu, bei za vyakula zinapaa kila kukicha zimebaki kua taabu tupu. Kila anayelia leo anskwambia ni bora ya jana.


Imefikia mahali wananchi wanalalamika kwamba hawatokaa kufanya makosa tena, hawatadanganyika tena. Walikua wakiamua hivi kuliko vile hali ingeweza kutengamaa Lakini bado wakajikuta wameangukia kugumu zaidi kuliko walikotoka.

Bado watanzania wanaamini hata hawajachungulia walikopataka.
 
Umeliona jambo moja zito sana ambalo wachumia tumbo wengi hawakuliona .

CCM hiii ni nyepesi kuliko toilet paper , Hivi ya Dimani umeyaona ? Hatari !
 
Kwa Tume hii ya uchaguzi na Katiba hii ya kale ni sawa tu na kutokuwa na upinzani! Upinzani gani wakati mgombea uraisi wa CCM atatangazwa mshindi na hamna pa kulalamika? Kwa nini CCM ipoteze muda na rasilimali eti kuzunguka kila kona kujieleza? Atakayetangazwa na tume ndiye raisi, basi!! Vigezo na masharti kuzingatiwa!! Ni goli la mkono dakika ya mwisho ndiyo siri!
 
Mkuu weka akiba ya maneno, haina haja ya kuumaliza upinzani, lengo lililopo ni kuudhoofisha tu. Na hakuna kipindi kigumu kwa upinzani kama kuelekea 2020, wapinzani wanatakiwa kucheza karata vema sana, la sivyo ukawa inaweza kuwa vipande vipande kabla ya 2020. Refer Lipumba's movie.
 
Naomba ieleweke kua hakuna mtu anayetaka kuumaliza upinzani nchini!
 
Naomba ieleweke kua hakuna mtu anayetaka kuumaliza upinzani nchini!
Ccm wanafikiri kummaliza upinzani ni kuwatisha hata kuwaua na pia watu na kesi za hovyo hovyo kupitia policcm,lakini wameshindwa pamoja na hivi vyote upinzani bado utasimama
 
CCM wanahangaika bure kutaka kuumaliza upinzani wakati kuna wapinzani wamejitolea uhai wao kuwapigania wanyonge wanaokandamizwa na CCM,hawako tayari kuisaidia CCM na maovu yake.
 
Raisi huku kwetu hapatikani kama matokeo ya kuchaguliwa na wengi. Anapatikana kwa kutangazwa na tume! Tume ile inapoteuliwa na Mwenyekiti wa CCM inapewa vigezo na masharti ambayo lazima kuyazingatia. Upinzani hata ungekua na nguvu kiasi gani huku kwetu, kwa sheria hizi za uchaguzi, na tume ya namna hii, hawataingia ikulu! Hili la kudai Katiba mpya na tume huru isiyoteuliwa na mwenyekiti wa CCM ni la kupewa kipaumbele na vyama vya upinzani.
 
Mimi mwenyewe nilijua tumeumia alipoingia Faru John, maana allianza kwa mikwara ambayo niliamini ilikuwa na nia thabiti kumkwamua mwananchi kwenye lindi la umasikini lakini na hivyo kutupa wakati mgumu wapinzani kwenye kujenga hoja za kuwashawishi wananchi maana tulifikia hata kusema kuwa anatekeleza sera zetu.Lakini kila siku zinavyosonga tumegundua kuwa hana njia mbadala ya kuwasaidia wananchi na kuwezesha nchi kukua kiuchumi, badala yake kaamua kuongoza kwa chuki na kutumia mabavu kuua upinzani kitu ambacho hakiwezekani,upinzania kwa sasa upo imara kuliko wakati mwingine wowote ule.
 
Back
Top Bottom