Don't get me wrong hukufanya kosa kujenga maana kwa wengi wetu hela ya kujenga huwa tunaidunduliza kidogo kidogo ba kupandisha jengo hadi limeisha..
Lakini kosa ni kwa sasa ambapo mjengo wako umekamilika halafu umechacha...
Maana unaishi humo ndani na familia yako ama hata kama huishi humo haipangishiki ukapata hela nzuri..
SIO VIBAYA KUUZA...
1.kama huishi humo ndani una nyumba ya thamani ya shs milioni 500 lakini hupati mpanaji wa kukulipa kodi ya shs 1.5m kwa mwezi UZA...
KISHA 500M kawekeze kwenye Government bonds za muda wa miaka 20
Kisha anza kulipwa shs 6,245,000/= kila mwezi kama riba yako kwa miaka 20 ijayo huku 500M yako imetulia tu ni Mali yako lakini kwa sasa utakuwa unapata hela kila mwezi mara 4 na kodi ya 1.5m ambayo hata kupata mpangaji ni shida..
Huna kodi ya jengo..
Huna kodi ya kiwanja ni wewe na 6.2M yako kila mwezi unakula maisha...
2.Kama ni nyumba unaishi humo na familia....wala usijali wala kuogopa...UZA
halafu wekezeza kwa bonds...kisha ile riba yako unavuta kila mwezi ya 6,245,000/= toa hapo 1.2M kapangishe bonge la jumba Mbezi beach ama Kawe Beach ..na mbweni...
Kisha bakiwa na 5M ya kula maisha wewe na familia yako...
Wanao waambie umewawekea 500M yao bank watakutana nayo miaka 20.ijayo kwa sasa waambie tule mkate kwa siagi wanangu maana mimi ndio wakati wangu huu wa kula raha.
Maana nikifa tu nyumba mtaiuza ndani ya mwezi tu mgawane hela...
Kama vipi haya wanao katika hiyo 5M inayobaki kama wako wanne kila mwezi walipe mshahara wa 500,000/= weeee watakaaa kimyaaaa chezea hela weyeeee
USIISHI DAR KWENYE NYUMBA YAKO HALAFU UMECHACHA....ni kosa la dhahabu sana...
DAR HAKUNA NYUMBA CHINI YA SHS MILIONI 200 ya mtu
Uza kisha kaziweke hata kwa GREEN BOND YA MIAKA 10 YA CRDB kisha vuta riba ya 10.25% kila mwezi
Hapo kwa 200M yako utakula riba kila mwezi shs 2,050,000/=
Kapange nyumba ya shs 500,000/= iliyo sawa na nyumba yako uliyouza kisha bakiwa na 1,550,000 ya kula maisha yako ....
Na kama una tatizo la mtaji na una uhakika na biashara unayotaka kufanya....
Bonds zako ni dhamana ya kukupa mkopo hadi wa 80% ya thamani ya bonds zako straight away no longo longo banks wanapenda saana dhamana za bond maana wanajua hela inakuja kiuhakika..
Hivyo kama una bonds za sha milioni 500 unakopeshwa milioni 400 chap chap....
Kama una za milioni 200 unakopeshwa 160M chap chap..
Unalipa mkopo ndani ya miaka mitano kisha umemaliza unaendelea kula riba zako zote tena hazilipii mkopo
Ila nakushauri kama una za 200M kopa hata milioni 100 tu ili zile 100 nyingine aendelee kuwa na hala ya kula kila mwezi maana biashara bwana hazitabiriki
Wasalaam
Jungle economist.