Sio lazima waziri wa afya na naibu wake kujiuzulu, ishu yenyewe ndogo tuu

Mi huwa namchukia sana mtu anayetumia udhaifu wa mwingine naye kujihararishia udhaifu wake, sitaki kuungana hoja hii kwa sababu hiyo tu
 
Mi huwa namchukia sana mtu anayetumia udhaifu wa mwingine naye kujihararishia udhaifu wake, sitaki kuungana hoja hii kwa sababu hiyo tu

Kama serikali yetu ingekua makini mawaziri wengi walitakiwa kustep down kwa uzembe na kutowajibika ipasavyo. 1.Celina Kombani na mwanasheria mkuu kwa kusema katiba iliyopo inafaa nk 2. Mwinyi, milipuko ya mabomu mbagala na gongo la mboto. 3. Ngeleja sakata la uchangishaji fedha aka jairo skendo. 4. Waziri wa elimu; wizi wa mitihani na kufeli kwa 80%. 5. Waziri wa uchukuzi zanzibar kuzama kwa meli. 6. Waziri wa mali asili wizi wa wanyama hai wakiwamo twiga. Hawa niwachache nilioweza kuwakumbuka list inaweza kuwa ndefu. Hawa wote wanatakiwa kuwajibishwa na mteuzi wao au kujiuzulu wenyewe kwa kuisababishia nchi hasara na upotevu wa rasilimali za nchi. Nikisema serikali ni dhaifu, hoi, legelege, hovyo, na chovu ktk kushughulikia mambo yamsingi nitakua nakosea!!?
 
Hebu tuache kuwatetea Mponda na Nkya kwa sababu wao ndo walifanya mgogoro ukalazimu madokta kugoma. Tukumbuke Dr Nkya alitafutwa kabla mgomo haujaanza matokeo yake akachagua kwenda kuongea na waandishi wa habari, hata alipofuatwa ofisini kwake na viongozi wa MAT aliishia kuwatolea maneno ya kejeli eti madokta hawana umoja hata kugoma hawawezi na serikali haitishiki. Dr Mponda naye alifuata mtindo wa msaidizi wake kwa kuita waandishi wa habari ndiyo maana pale starlight madokta waligoma kumsikiliza Mponda badala yake ikabidi Hawa Ghasia aongee kwa niaba ya wizara ya afya. Hivyo hawa ni kati ya vilaza wengi ndani ya Serikali ya JK ambao wanatakiwa kung'oka
 

Ndugu yangu Ibrah kwenye serikali ya awamu hii hakuna mtu atakayejiuzulu kwa sababu wote wanajua hata wasipojiuzulu hawatawajibishwa. Waziri Mkuu ameshafanya wajibu wake wa kuwaondoa wale walioko kwenye level yake ya kazi na ni wajibu wa raisi kuwasimamisha kazi wa kwake ili uchunguzi ufanyike, la sivyo atamfanya Waziri Mkuu wake aonekane hana maana. Kuna scandal nyingi sana zinazongojea Raisi achukue hatua nafikiri hata wahusika wanashangaa wana-survive namna gani. Issue kama ya Jairo bado imepigwa tarehe, scandal nyingine zote watu wote wamejitahidi kuchukua hatua zao za kuwajibisha wahusika lakini inavyofika kwa Raisi anakaa kimya. Mimi nina uhakika kuwa Raisi wetu amedhoofishwa sana na vitu viwili: kwanza, amehusika kwenye scandal nyingi sana katika hizi scandal ambazo tunasubiria decision, na pili, huyu Raisi ameweka dhamana sana kwenye kupendwa na watu hasa wazungu, kiasi kwamba anaogopa kama ukweli wa madudu yake utaanikwa, wale wanaomheshimu ndani na nje ya nchi wataujua ukweli na heshima yote waliyokuwa wanampa itaisha. What he doesn't know ni kwamba wale wanaojidai kumpenda hasa huku nje wanamchekea tu kidplomasia lakini nyuma wanamwona hana maana, the same way they laughed with Mobutu au wengine kama Mugabe. They know what they want and as long as they are getting it, why rock the boat? Unfortunately, Watanzania wenyewe ndio wanaoweza kufanya maamuzi ifikapo muda wa kura.
 
ifike hatua tukubali udhaifu wa mfumo tuliona lakini pia viongozi wetu kwa upande mwingine,dr.mponda hatakiwi kumsubiri mh.rais amuwajibishe bali awajibike mwenyewe pamoja na naibu wake,tatizo la mgomo wa madaktari viongozi hawa wenye dhamana ya kisiasa wamechangia kwa kiasi kikubwa kwa kutotimiza wajibu wao kama wasimamizi wa sera na kutafuta majawabu sahihi kwa muda muafaka,wao kwanza walilala pili wakaja na vitisho kwa madaktari,walipaswa wao wawili wakae na madaktari wajadili kwa kina na kukubaliana sidhani kama mgomo ungefika ulipofikia.madhara yanayotokana na mgomo hasa madaktari athari zake zinaanza kuoneka mara tu daktari anapoweka vifaa chini,watu wanakosa huduma,watu wanazidiwa watu wanapoteza maisha mara tu daktari napoweka tools down,mgomo umechukua takribani wiki tatu waziri anataka kuendelea kuwa ofisini sio sahihi kuendelea kuwepo kwakuwa tafsiri ya mawaziri wa afya kushindwa kutatua matatizo ya madaktari hawawezi kupikika chungu kimoja kwa kuwa lazima mmoja ampishe mwingine aidha daktari au viongozi wawapishe,so pale ktk ile wizara kuna matatzo ya msingi zaidi kuliko tunavyofikiria.waziri,naibu wazir wawafuate wasaidiz wao ili pia uchunguz uweze kuwa huru na wa haki na pia walete taarifa ni ndg zetu wangapi wamepoteza maisha kutokana na mgomo huu.tuache kulinganisha mambo yaliyopita na tuliyonayo hasa kama tuna nia njema kwa taifa letu lazima tuwe na viongozi wanaowajibika kwa wananchi na si kwa mambo yao binafsi.
 
Wewe unatakiwa damu ya mpenzi wako ipimwe na vile vifaa feki vya ukimwi uambiwe hana ukimwi wakati anao.
 
al Saaf ametumia METAPHOR! anataka kuonesha kuwa uozo upo kwenye Jamii nzima ya utawala wetu. Hivyo ishu si waziri wa afya na naibu wake pekee bali uongozi mzima una tatizo na unapaswa kupigwa out!
lakini kwa sababu nchi yetu hawa viongozi ni wagumu kutoka wenyewe pale tunapowabamba readyhanded ndo hapohapo tukomae nao kama tunavyofanya kwa mawaziri wa afya!
 
Kweli wewe ni profound kilaza.Madhara ya shule za kata haya.

Moderators tusitoe adhabu kali sana kuwabann watu kwanza ni kwa muda mrefu sana halafu ikiwezekana wapewe warnings kwanza kabla ya kuwabann kwani tunawapoteza great thinkers humu kama my friend mabolio!
 
Hivi nyie wote mnaosema utendaji wa Haji Mponda ni mbovu au uwezo wake ni mdogo, mnamlinganisha na waziri yupi aliyewahi kuongoza hiyo Wizara ya Afya? Au mnamlinganisha na yupi atakayekuja kuongoza? Tusifanye ushabiki tu, tuje na comparisons au facts zitakazotusaidia kujenga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…