Sio lazima waziri wa afya na naibu wake kujiuzulu, ishu yenyewe ndogo tuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sio lazima waziri wa afya na naibu wake kujiuzulu, ishu yenyewe ndogo tuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Seif al Islam, Feb 11, 2012.

 1. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  mimi nawashangaa watu na taasisi zinazomkomalia waziri wa afya na naibu wake wajiuzulu kwa hako kamgomo ka wiki tatu.jaman mbona watu wengi tu wamevurunda hatuwaulizi?kwanza mwaka jana tuu,matokeo ya form 4 watoto 80% walifeli na kupata zero,waziri wa elimu anapeta hadi leo inakuwaje mumkomalie waziri wa afya ilhali waziri wa elimu hadi leo anapeta?,hata mwaka huu udanganyifu kwenye mitihani ya darasa la saba umekuwa mkubwa na unaotisha lakini hatujasikia waziri akiambiwa ajiuzulu iweje basi mgomo huu mdogo tuu ulete balaa.kwani waliokufa ni wengi kuliko wale waliokufa kwenye ajali ya meli kule zanzibar?.najua pia mtatkumbuka kuwa mabomu ya gongolamboto yalilipuka na kuleta maafa makubwa.ule ulikuwa mwendelezo wa maafa na uaribifun uliotokea mbagala na waziri husika aliyeahidi kujiuzulu kama ingebainika kulikuwa na uzembe yupo hadi leo na anapeta huku akifunika ripoti ya uchunguzi iliyomtia hatiani akiusaka uraisi kishkaji,sasa inakuwaje leo mnakomaan waziri wa afya atoke?au ndo anamzibia mgombea wenu?watanzania tuazche unafiki,kama ni kuwajibishana iwe kwa wote na katika yote yanayostahili sio kuwachagua watu fulani tu na kuwakomalia.Naomba niwasilishe
   
 2. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Jamani tutenganishe utendaji wa kiserikali na kisiasa.
  Mgogoro umesababishwa na Blandina Nyoni na mhauri
  wake mkuu Dr Deo Mtasiwa. Waziri ni mtu anayeandikiwa
  hotuba na taarifa mbalimbali. Jamani tuwe wakweli
  tusipende tu kukurupuka rumuonee hurunma Dt Haji
  Mponda na naibu wake Dr Nkya walikuwa wanafanya kazi
  na KM ambaye yuko corrupt vibaya sana na ambaye
  ungeshisi kama vile analindwa na mfumo wa usalama wa
  nchi. Ukizisoma tuhuma za Blandina unaona zimejaa
  ufisadi, ukabila na wizi wa moja kwa moja. Tuhuma hizi
  ziko muda mrefu lakini Dr Haji Mponda na naibu wake
  Nkya hawana tuhuma yeyote ya matumizi ya madaraka
  wala ufisadi. Maamuzi mengi ambayo yamewakwaza
  madaktari yamefanyika mwaka 2010 na 2011 na Blandina
  Nyoni aliyekuwapo hapo tangu 2008 na Dr Mtesiwa
  aliyekuwapo tangu 2006.
  Mtanzania yeyote angeweza kupatwa na situation
  iliyompata Dr Haji Mponda kwenye utendaji wa Nyoni.
  Naomba turejee hata kwenye utawLa wa Profesa
  Mwakyusa, mutakumbuka kuwa hata yeye alikuwa
  anafunikwa na huyu mama. Kwa mtazamo wangu mimi
  tatizo ni la mfumo wa utendaji wa serikali, kwa hiyo
  napendekeza tumpe muda Dr Haji Mponda
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Yaani wewe unachezea roho za watu! Nadhani wewe ni IDIOT kama JK
   
 4. D

  DATOGA Member

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Pumbaaaaaaaaaaaaafu kabisa wewe
   
 5. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kama wewe ni great thinker njoo kwa hoja, matusi hayasaidii kitu
   
 6. K

  Kitorondo Member

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Ni lazima wajiuzuru na wakichelewa Rais awatimue mara moja.mbona Mzee Ali Hassani Mwinyi alijiuzuru uwaziri wa mambo ya ndani kwa kosa ambalo walifanya wasaidizi wake? kwenye law of torts(sheria za madhara kuna kitu kinaitwa vicorious liability master will be liable for the offence of his servant.tatu,uwezo wao wa kuongoza wizara umeonyesha ni mdogo sana
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Issue kubwa ni ipi na issue ndogo ni ipi? Tunaongozwa na vilaza kila upande wanaojificha kwenye Phd za kudesa na kugawana kama njugu!
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jina lako lanikumbusha mtoto wa Muammar Gadaffi!
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kweli wewe ni profound kilaza.Madhara ya shule za kata haya.
   
 10. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na mimi nakushangaa "Seif al Islam". Mawazo yako yangekuwa mazuri kama ungejadili positively kwamba ni vema waziri wa afya kujiuzuru kama mfano mzuri kwa hao ambao hawakujiuzuru huko nyuma kwa mifano uliyotoa ya (1) mwaka jana matokeo ya form 4 watoto 80% walifeli na kupata zero (2) mwaka huu udanganyifu kwenye mitihani ya darasa la saba umekuwa mkubwa (3) wale waliokufa kwenye ajali ya meli kule zanzibar na (4) mabomu ya gongolamboto/Ukonga baada ya fundisho kutokana na mabomu yalilipuka Mbagala. Ni kama wewe unaona yaliyofanywa huko nyuma ni sawa! Tusipime usahihi wa maamuzi yetu kwa kutumia maamuzi mabaya yaliyopita.
   
 11. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kuna madudu kibao yamefanyika hapa Tanzania katika utawala wa JK lakini hakuna lililofanyika ila inabidi ifike wakati tuanze kuwa na uongozi unaowajibika. Waziri wa afya anaweza kuwa wa kwanza na kuanzia sasa mawaziri wajue kuwa kuna kitu kinaitwa kuwajibika. Ni aibu sana jinsi mambo yanavyoendeshwa hapa kwetu
   
 12. k

  kimambosr Member

  #12
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kujiuzuru sio adhabu, ni na dalili nzuri ya uwajibikaji. Tatizo watanzania wakishapewa madaraka wanataka wafie hapohapo. kwani ukijiuluzu ukarudia kazi ya ya zamani kuna tatizo gani? kwani ulizaliwa kuwa waziri? uongozi ni dhamana tu. Wenzetu china waziri mapato yake kwa mwezi anazidiwa na mshahara wa engineer hapa kwetu. china hakuna mianya ya kuiba. Ukiiba wanakula shingo. Huku kwenye ukishapewa madaraka unaona ndio sehemu ya kufanya ufirahuni. ndio maana mkiambiwa kujiuzulu mnapaniki kwani mnakua na ndoto za kifasadi.
   
 13. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,659
  Trophy Points: 280
  1. Umekwisha iona job description ya waziri?
  2. Hujui kuwa ni waziri pekee anayeweza kumshauri rais kuhusu udhaifu katika wizara yake?
  3. Hujui kuwa waziri ana wajibu wa kisiasa katika wizara yake?
  4. Hujui kuwa Mawaziri hawa wa afya kwa kiwango kikubwa wamehusika kusababisha na kurefusha mgomo wa madaktari?
  5. Hujui kuwa kutokana na uzembe wa mawaziri hawa serikali imedhalilika?
   
 14. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  kwahiyo unataka kusema waziri hapaswi kutumia akili yake?yaani yeye kusoma tu speech alizoandaliwa regardless ya ukweli wa anayoyasoma?inawezekana wewe ni mwanaasha
   
 15. The Mockingjay

  The Mockingjay JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mawaziri ni reflection ya rais.
  Na ndio wanaopeleka siasa wizarani.
   
 16. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  WANABODI
  hawa waheshimiwa Dk mponda na naibu wake wanapaswa kuwajibika kwa kustep down na hiyo ndo tafsiri sahihi ya collective responsibility kama alishauriwa vibaya na hakugundua kuwa anapotoswa sasa yeye wanini pale kama hana mchango wowote akishauriwa vibaya nae anatenda vibaya hawa ndo wanaotusababishia matatizo ya kiuchumi tuliyo nayo tunawalipa watu wasiona mchango wowote kwetu...
   
 17. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Al islam, nasikitika kwa utetezi unaoufanya kwa hao Mawaziri. Nchi za wenzetu Mawaziri huwajibika kujiuzuluhata kwa makosa yaliyofanya na subordinates wao, hata kwetu Rais Mst Mwiniyi aliwahikufanya hivyo kwa makosa ya Askari (sio yeye binafsi) wa Wizara yake. Huyu Dk Mponda na Nkya wao wenyewe personally wanahusika na matatizi haya kufika hapo, naamini hata PM Pinda alipaswa kujiuzulu kwa kusababisha maisha ya watu kupotea maana mwanzo hakufanya jitihada za dhati kumaliza tatizo hilo bali alichochea.
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa kawaida katika nchi za kistaarabu kama kumetokea uzembe au uoza kwenye wizara, hata kama waziri hahusiki, anapaswa kujiuzulu ili kumpa rais clean slate na kurejesha imani ya raia katika serikali. Lakini sisi Tz kwa sababu mawaziri wameingia kwa ajili ya ulaji, kujiuzulu inakuwa ni ngumu sana. Mwinyi bado yupo licha ya kwamba watu walipoteza mali na maisha Gongo la Mboto. Ndio maana imani katika serikali ya Kikwete imepotea.
   
 19. oba

  oba JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  unajua mama Nkya alivyowadharau madokta? au unaropoka tu, si ndo huyu huyu ambaye aliitwa ukumbi wa Donbosco yeye akaenda kuongea uongo na waandishi wa habari ukumbi wa Anatoglo? jamani tuache utetezi wa kihuni!
   
 20. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  [​IMG]
   
Loading...