Sio kwamba Mimi ni mariaoo, ila

Live circuit

Senior Member
Joined
Mar 11, 2023
Posts
124
Reaction score
366
Habarini Wana janamvi ,
Nimeona nianze na heading ili mjue sio kwamba nataka kulelewa Ila najiuliza Kuna upendo kweli apa, ?

Mim nilikua nafanya kazi kwa miaka minne nikaacha nikaja chuo kusoma course niipendayo by that time mtarajiwa wangu yeye anafanya kazi na analipwa pesa nyingi Zaid yangu, almost take home 800k ,
Lakin 3yr now sijawah muomba ela na hajawah hata ni jaribu kama naweza pokea ela yake ,
Ingawa nilishapanga kuwa siku akinipa ntanunua vitu vya thamani Ile Ile nimtumie,

Najiuliza kama ni Mimi ningekua kwenye nafasi yake na yeye yupo kwenye nafasi hii ya masomo nilio nayo si angeishi kama malkia chuoni?

Thanks God Mungu ananijaria najiteoshelesha kwenye Ada, mavazi chakula (nipo chuo Cha kati)

Lakin hajawah ata jistua kuwa ebu Leo nimetumie just a little,
Ingawa kiukweli akinipa ntanunua vitu kama nguo namtumia ,

Ninacho jua mkiwa wapenzi vyote ni vyenu ingawa as a men siwez tegemea ela yake Ila naweza tumia njia hiyo kama kipimo Cha upendo,
Hivi Kuna upendo kweli apa,
 
Hapo huyo ni mchoyo au hajawahi kukupenda kabisa.......
 
Ela, apa etc jifunze matumizi ya h ili akuone kweli ni Dume la mbegu
 
........mkuu nikutoe wasiwasi tu kwamba huyo mke wako sijui mchunba anakupenda vizuri kabisa.....anachokosa hapo ni akili ya kujiongeza kidogo afanye hicho unachosema hata kwa kuzuga tu.......Sasa Hilo wewe hupaswi kumuhukumu coz anaendeshwa zaidi na asili ya jinsia ya kike ambayo huwa inaamini mwanaume ni mpambanaji hakosi hela Kwa vyovyote vile.....so yeye haoni kama unashida licha ya kujua hauna kazi, ndo maana hata kwenye familia masikini ambapo watoto wote me na ke mnakuwa hamana kazi lakini utaona mtoto wa kiume unaombwa pesa na dada zako, yaani wanaamini we una hela kwa sababu mwanaume.....hiyo ishu ingeletwa na mwanamke kwamba mumewe hamuhudumii chuoni ndo ingekua query......
 
Zingatia masomo yako ndio kitu muhimu kwako kwa sasa.
Kama umeamua kupima upendo wake kwako kwa njia ya wewe kupewa hela na huyo mwenzako,basi hapo hakuna upendo,

Pia jaribu kujifundisha kuandika Kiswahili fasaha,huleta heshima pia,

Apa___Hapa
Ela___Hela
Ananijaria___Ananijalia
Ata____Hata
Jistua___Jishtua,

Umesema upo Chuo Eee!
 
[emoji6][emoji6] error
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…