Sio kila kitu kinafaa kuigwa Hollywood

Sio kila kitu kinafaa kuigwa Hollywood

Makini

Senior Member
Joined
Dec 23, 2014
Posts
154
Reaction score
59
rihana.jpg

Katika harakati za kufatilia kinachoendelea Hollywood Marekani, nimegundua kuwa Mastaa wengi katika tasnia za filamu na muziki wamekua sehemu ya maisha yetu hasa kwa vijana waliopo katika mashule ya sekondari na vyuo. Vijana wengi wanawachukulia hawa ‘celebs' kama ni Miungu watu, wanawaamini sana na kuona hawawezi kukosea.

Tunachoshindwa kugundua ni kwamba mastaa hawa wanatuletea hasara zaidi ya faida kwenye jamii zetu. Mitindo ya mavazi wanayokuja nayo, yaani kila kukicha afadhali ya jana, ni kama wanashindana nani ataonesha mwili zaidi ya mwingine au nani atatoa video chafu zaidi ya muziki.

Kingine ambacho hivi sasa nimegundua kuwa ni tatizo kubwa, ni movie za hollywood zinazotufundisha mbinu za ujambazi na ubabe huku zikijificha chini ya mwavuli wa ‘Action'. Vijana wengi wa kike na wa kiume wanawatizama mastaa kama mashujaa na watu wa kuigwa.

Rihanna aliwahi kusema yeye si mfano wa kuigwa kutokana na yale anayoyafanya. Mtazamo wangu ni kwamba si yeye tu bali mastaa wengi wanafanya mambo yasiyostahili kuigwa kabisa. Nahisi huu ni muda wa kubadilika na kuhakikisha vijana tunakuwa makini na vitu tunayotizama na tunayoamua kuiga kutoka kwa mastaa.
 
Makini Kila mtu na rollmdl wake wengine huwaambii kitu kwa rihana xo aina hii ya mawazo imechelewa sana, kunabinadamu ukiwacheki utasema Rihana ndio anaiga Bongo ha ha ha ha....
 
Watu wameshakuwa adicted. Tena wanaoendekeza mchezo huu ni wasanii, wao badala ya kudumisha utamaduni wetu wanakuwa mstari wa mbele kufata tamaduni za watu, inahitaji nguvu ya ziada kuwaelimisha watu katika hili.
 
Wanashindwa kuelewa kwamba yeye huyo(Rihana) biashara yake ya muziki ndiyo inamfanya awe hivyo alivyo.
 
Katika harakati za kufatilia kinachoendelea Hollywood Marekani, nimegundua kuwa Mastaa wengi katika tasnia za filamu na muziki wamekua sehemu ya maisha yetu hasa kwa vijana waliopo katika mashule ya sekondari na vyuo. Vijana wengi wanawachukulia hawa ‘celebs' kama ni Miungu watu, wanawaamini sana na kuona hawawezi kukosea.

Tunachoshindwa kugundua ni kwamba mastaa hawa wanatuletea hasara zaidi ya faida kwenye jamii zetu. Mitindo ya mavazi wanayokuja nayo, yaani kila kukicha afadhali ya jana, ni kama wanashindana nani ataonesha mwili zaidi ya mwingine au nani atatoa video chafu zaidi ya muziki.

Kingine ambacho hivi sasa nimegundua kuwa ni tatizo kubwa, ni movie za hollywood zinazotufundisha mbinu za ujambazi na ubabe huku zikijificha chini ya mwavuli wa ‘Action'. Vijana wengi wa kike na wa kiume wanawatizama mastaa kama mashujaa na watu wa kuigwa.

Rihanna aliwahi kusema yeye si mfano wa kuigwa kutokana na yale anayoyafanya. Mtazamo wangu ni kwamba si yeye tu bali mastaa wengi wanafanya mambo yasiyostahili kuigwa kabisa. Nahisi huu ni muda wa kubadilika na kuhakikisha vijana tunakuwa makini na vitu tunayotizama na tunayoamua kuiga kutoka kwa mastaa.

Kwa hiyo tufanyeje sasa, mbona hujatoa suluhisho la hili tatizo?
 
suluhisho liko hapo, tuache kutumia muda mwingi kuwafuatilia na kuiga vitu wanavyofanya visivyo vya kistaarabu
 
Hili swala haliwezi kua solved kwa simply ushauri.. Hadi mtu yamkute ndo anajua kua alikua anapoteza muda, tatizo wanakuja kugundua when its already too late life lishawapiga chenga hawana direction.. ni ka mtu anajipanga mwaka mzima afikishe milioni ili anunue simu flani akitembea kila mtu amuone yuko juu, plain stupid.. bongo wamejaa sana design hii
 
Back
Top Bottom