KING COBRA
JF-Expert Member
- Nov 10, 2011
- 2,782
- 877
Shetani ana watu wengi kuliko LowasaKitendo Cha Wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kumdhamini Lowasa imetusaidia sisi Watanzania kujua kumbe CCM ni chama kinachounga mkono vitendo vya UFISADI. Somo zuri sana
Sasa kama hawajirudii mbona kuna watu kila mtangaza nia akipita mkoani kwao ni lazima utawaona tu wapo mstari wa mbele...???Hapana
Udhamini ni kwa mgombea mmoja tu. Hao 50,000 ni kuhakikisha wengine wanakosa wa kuwadhamini.....
Sasa kama hawajirudii mbona kuna watu kila mtangaza nia akipita mkoani kwao ni lazima utawaona tu wapo mstari wa mbele...???
Sawa kabisa, na hiyo ndo nia halisi.. Wapige kelele jamaa atawakosesha wadhaminiKama mgombea mmoja ana wadhamini 50,000 na mkoa una CCM kama 200,000 sasa hao wagombea wengine si watakosa wadhamini?
Acha kupotosha Makatibu wa Mkoa wanatafuta wadhamini kwa kadi zao na kuzirudisha haina haja hata ya kuonana na unayemdhamini hiyo ni Rushwa tu. Akina Bilali hawajetembea hata hiyo mikoa yote zaidi ya kutafutiwa wadhamini na kurudisha fomu hao wanaozunguka kila Mkoa na wilaya wanatafuta kuhonga tu na kampeni hawana linginekwani kuna kosa gani wakilipwa? umemuweka mtu saa tano anakusubiri, je ni kosa kumlipa muda wake alioupoteza kukusubiri?
acheni mawazo ya kifukara.
kwani kuna kosa gani wakilipwa? umemuweka mtu saa tano anakusubiri, je ni kosa kumlipa muda wake alioupoteza kukusubiri?
acheni mawazo ya kifukara.
wagombea wote 30+ hawaendi mkoa mmoja.
Chama cha Mapinduzi kilifungua dirisha lake la watia nia kwa ngazi ya urais. Wanachama wengi wamejitokeza hadi sasa wanakaribia kufikia 40. Miongoni mwao wameshakamilisha zoezi la kutafuta wadhamini wasiopungua 450 kwa mikoa isiyopungua 15 ya Tanzania. Katika mchakato huo, baadhi wametumia fursa hiyo kujiuza toka mkoa mmoja hadi mwingine huku wapambe wao wakisherehesha mikutano ya kusaka saini za wadhamini kwa mikutano mikubwa sana. Na baadhi yao wamefanya na kukamilisha mchakato huo kimya kimya.
Aidha, kwa watia nia wengine miongoni mwa waliojitokeza inaonesha kuwa fursa hii ya kusaka wadhamini waliisubiri kwa kwa shauku kubwa. Ni fursa ambayo ilikusudiwa kujiuza kwa taifa kwa maana kabla ya hapo hawakuwa na wala wasingeipata fursa kama hii. Hii ni fursa adimu ya kuzunguka nchi nzima ukisema makusudio yako ni nini kwa umma. Fursa adimu iliyotumika kuvuka mipaka ya zoezi hata kufikia kuitangulia NEC ya Jaji mstaafu Lubuva.
Inavyoelekea, kuna watia nia hao waliokuwa wamepanga kimkakati kabisa kutumia mchakato huo kuanza kampeni za kuusaka urais mapema. Na kwa mujibu wa Katibu Mwenezi wa CCM ndugu Nape Nnauye mchakato wa kutia nia na kusaka wadhamini sio muda wa kampeni. Hata hivyo, kwa sisi tulio wengi mchakato huu kwa baadhi ya watia nia umegeuzwa muda na msimu wa kampeni kiaina. Kampeni ambazo si kwa wanachama tu, bali sasa ni kwa taifa zima.
Tunapenda kuelewa, kwa mujibu wa kanuni za CCM. Je! Ni sahihi kwa mwenendo kuwa hivi?