Sintofahamu KKKT siyo Kanisani tu, Benki ya Maendeleo nako kuna mambo

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Wadau salamu.

Hivi karibuni Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKKT) limekumbwa na migogoro ya kiuongozi na waumini wao, hususan Dayosisi ya Konde, lakini ukweli ni kwamba, hata Benki ya Maendeleo ambayo inatajwa kuwa mmiliki wake ni KKKT pia ina sintofahamu

Kifupi, hii benki, imefungua Center za kukopesha wajasiriamali wadogo wadogo mitaani katika maeneo mbalimbali ya nchi, Dar ikiwemo na marejesho ya mkopo ni kila wiki. Kwa hiyo kila wiki wateja wanakutana Center husika ili kutoa marejesho na maafisa huyachukua kupeleka benki.

Sasa wiki moja nyuma nilikutana na mama mmoja kutoka Center ya Ukonga ambaye alinisimulia ukiritimba ndani ya hizo Center.

Alisema: "viongozi wa kwenye hizi Center wamejifanya 'mungu watu' kiasi kwamba huwezi kuamini kuwa ni taasisi ya kidini. Kupewa mkopo 'inategemea viongozi siku hiyo wameamkaje'. Unaweza kujaza fomu na ukakataliwa kupewa pesa bila sababu ya kueleweka.

"Wapo viongozi (maafisa) wanacheza dili na baadhi ya wateja, yaani mteja anajaza fomu anataka sh. 1,000,000 afisa anamwambia atamwidhinishia sh. 2,000,000 halafu mteja akishachukua Mil. 2, Mil. 1 iliyozidi anampa afisa kwa ahadi kwamba yeye (afisa) atakuwa akilipa rejesho la hiyo milioni moja yake lakini mwisho wa siku halipi, mteja ndiyo anabeba mzigo.

"Hili jambo liliwahi kumkuta afisa mmoja wa Center ya Bonyokwa, anaitwa Adamu. Alimuidhinishia mteja pesa milioni mbili, moja ya kwake, yakamkuta mazito baada ya mteja kubumbulua, maana ilibidi marejesho ayabebe peke yake, Adamu akakamatwa na kupelekwa polisi. Sina hakika kama alitoka.

"Pia, yuko mwanamke alikataliwa kupewa mkopo eti kisa ana mimba. Mtu kuwa na mimba ni kigezo kweli? Kwani biashara anayoifanya inahusiana nini na mimba?

"Mimi mwenyewe yaliwahi kunikuta makubwa, nilichelewesha rejesho. Afisa mmoja alinicharura kama anamcharura mwanaye. Machozi yalinitoka. Wanachama wenzangu walishangaa sana maana afisa mwenyewe ni kama mwanangu wa kumzaa.

"Kifupi, Maendeleo Bank katika hizi Center zake mitaani, ina sifa mbaya sana tofauti na taasisi zingine kama ASA TANZANIA, BLACK, NETRON na nyingine ambazo zinasifika kwa utendaji bora.

"Nawaambia viongozi wa juu, kama Askofu Shoo anahusika, au mkurugenzi mkuu, Mwangalaba wapitishe fagio la chuma kuwatoa maafisa wasiojali utaratibu ili taasisi iaminike kama zamani,' Viongozi wakuu watembelee kila Center wasikie malalamiko kutoka kwa wateja kwani yapo malalamiko, leo mimi nimekwambia machache tu," alimaliza kusema mwanamke huyo.
 
Nyinyi ndio mnafanya kanisa letu lionekane la hovyo,mambo ya kufikisha sehemu husika wewe unakuja kuleta mitandaoni,kwanini usiende kukopa huko ASA TANZANIA,NETRON na BLACK?..Mtu umenyimwa mkopo na vigezo unavyo si uende kwa uongozi wa bank ukalalamike? Umechelewa kurudisha mkopo ulitaka uchekewe kisa umemzidi umri Afisa? Tuachieni KKKT yetu kasali kwingine.
 
Shoo anahusikaje na Bank inayomilikiwa na Dayosisi ya Mashariki na Pwani??

Ulivyosema Maendeleo Bank ni bank ya KKkT nchi nzima hapo tu nimeingia walakini kama kweli wewe ni muumini wa KKKT kweli! Maendeleo Bank iko chini ya DMP kama vile ambavyo Dayosisi ya Kaskazini inamiliki Uchumi Commercial Bank. Hayo malalamiko peleka kwa Malasusa..
 
Pia, yuko mwanamke alikataliwa kupewa mkopo eti kisa ana mimba. Mtu kuwa na mimba ni kigezo kweli? Kwani biashara anayoifanya inahusiana nini
Na hapa umejiona wewe una akili kuwashinda wao?
Usome ualimu huko maisha yakushinde uje ubishane na wanaojua athari ya kukopesha wajawazito kwa marejesho ya namna hiyo sio mzima wewe
 
Yaani officer anapiga nusu ya mkopo Ila marejesho anafanya mkopaji. Huu ni ufisadi mkubwa na aibu ya Bank ya Kanisa. MD Mwangalaba hebu amka uliko. Bank wataiua hiyo.
 
Shoo anahusikaje na Bank inayomilikiwa na Dayosisi ya Mashariki na Pwani??

Ulivyosema Maendeleo Bank ni bank ya KKkT nchi nzima hapo tu nimeingia walakini kama kweli wewe ni muumini wa KKKT kweli! Maendeleo Bank iko chini ya DMP kama vile ambavyo Dayosisi ya Kaskazini inamiliki Uchumi Commercial Bank. Hayo malalamiko peleka kwa Malasusa..
Safi san
 
SO wewe ndio umekuwa mtoa habari baada ya kuzinguliwa.....JITAFAKARI VEMA......
 
Kazi ya kanisa ni kueneza injili hayo mengine wamejibandika matokeo yake kanisa linageuka pango la wanyang'anyi na siyo kimbilio
 
Nyinyi ndio mnafanya kanisa letu lionekane la hovyo,mambo ya kufikisha sehemu husika wewe unakuja kuleta mitandaoni,kwanini usiende kukopa huko ASA TANZANIA,NETRON na BLACK?..Mtu umenyimwa mkopo na vigezo unavyo si uende kwa uongozi wa bank ukalalamike? Umechelewa kurudisha mkopo ulitaka uchekewe kisa umemzidi umri Afisa? Tuachieni KKKT yetu kasali kwingine.
Sasa hilo ni kanisa au kichaka cha kufanyia biashara bila kodi?
 
Back
Top Bottom