Single mothers na vilio vya kushangaza

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,230
116,844
Tuseme tu ukweli kuna wadada wengi au wamama siku hizi wanaamua kuzaa tu....hasa umri fulani ukifika na wengine wanaamua kuzaa kabla hata wa kuzaa nae hajatokea...

Sasa kimbembe kinaanza anaposhika mimba....au akishazaa na mtu ambae si ajabu hakuwa na mipango ya kuzaa na huyo mwanamke

Wadada wengine wanaamua kutumia mimba kulazimisha commitment au ndoa......Asipopata hiyo ndoa au hiyo commitment ni kumlaani huyo mwanaume na kutumia mimba au mtoto kama njia ya kumkomesha huyo mwanaume..

Siku hizi unakuta vilio vya wadada kuwa 'wanaume hivi na wanaume vile'
lakini ukweli sio wote walidanganywa wataolewa au waliahidiwa commitment

Wengine kupata mimba na kuzaa ilikuwa ni mipango yao binafsi..lakini wakishazaa wanaanza kubadili maneno...utasema waliahidiwa kweli kuolewa
au waliahidiwa matunzo ya mtoto in the first place kabla hawajashika mimba...

Ni busara kwa kila mwanaume kushiriki matunzo ya mimba inayomhusu
na matunzo ya mtoto wake......lakini wote tunajua busara sio kila mtu anayo
na wadada wanaojichukulia maamuzi binafsi ya kuzaa ni busara pia wakaacha kulialia.....kama vile maamuzi hayo yalikuwa ya watu wawili
na wengine husingizia kwa ndugu kuwa waliahidiwa ndoa...kumbe ni maamuzi yake binafsi kuzaa.......dunia imebadilika.... tupunguze lawama tukabili changamoto za maamuzi yetu...
 
Tuseme tu ukweli kuna wadada wengi au wamama siku hizi
wanaamua kuzaa tu.....hasa umri fulani ukifika
na wengine wanaamua kuzaa kabla hata wa kuzaa nae hajatokea...

Sasa kimbembe kinaanza anaposhika mimba....au akishazaa
na mtu ambae si ajabu hakuwa na mipango ya kuzaa na huyo mwanamke

Wadada wengine wanaamua kutumia mimba kulazimisha commitment
au ndoa......Asipopata hiyo ndoa au hiyo commitment ni kumlaani huyo
mwanaume na kutumia mimba au mtoto kama njia ya kumkomesha huyo mwanaume..

Siku hizi unakuta vilio vya wadada kuwa 'wanaume hivi na wanaume vile'
lakini ukweli sio wote walidanganywa wataolewa au waliahidiwa commitment

Wengine kupata mimba na kuzaa ilikuwa ni mipango yao binafsi..lakini wakishazaa
wanaanza kubadili maneno...utasema waliahidiwa kweli kuolewa
au waliahidiwa matunzo ya mtoto in the first place kabla hawajashika mimba...

Ni busara kwa kila mwanaume kushiriki matunzo ya mimba inayomhusu
na matunzo ya mtoto wake......lakini wote tunajua busara sio kila mtu anayo
na wadada wanaojichukulia maamuzi binafsi ya kuzaa ni busara pia wakaacha
kulialia.....kama vile maamuzi hayo yalikuwa ya watu wawili
na wengine husingizia kwa ndugu kuwa waliahidiwa ndoa...kumbe
ni maamuzi yake binafsi kuzaa.......dunia imebadilika....
tupunguze lawama tukabili changamoto za maamuzi yetu...
Kama huna mpango Wa kuzaa nae kwanini mpige kavu
 
PMU=pata mimba uolewe.Anaweza akakuoa kweli lakini hivyo vishindo huko ndani sasa.Huu ulimwengu wa contraceptive hivi unapatapataje mimba ovyoovyo?

Unakuta mdada alitoa mimba za kutosha
halafu anazaa na mtu anaanza kulalamika alirubuniwa

Hataki kusema ukweli alizaa kwa utashi wake pengine kamtegea huyo mtu
 
Hakuna mtu aliyechagua kuwa single mom, it just happens na hakuna jinsi. Hawa single moms mimi nawaheshimu sana, they're stronger than us all, they are fighers, breadwinners kwa watoto wao, mara nyingi wanakuwa bullied lkn still they keep going.

You need an iron chest kuwa single mama. Ni watu kamwe siwezi kuwasimanga.

Hats off to all single mama who are disrupting status quo. Salute!
 
Ukiamua mwenyewe kupata ujauzito... matokeo ya maamuzi yako yasijikite katika kutafuta sehemu ya kuangushia mzigo ulioubeba kwa hiari yako mwenyewe....
 
Hakuna mtu aliyechagua kuwa single mom, it just happens na hakuna jinsi. Hawa single moms mimi nawaheshimu sana, they're stronger than us all, they are fighers, breadwinners kwa watoto wao, mara nyingi wanakuwa bullied lkn still they keep going.

You need an iron chest kuwa single mama. Ni watu kamwe siwezi kuwasimanga.

Hats off to all single mama who are disrupting status quo. Salute!

Wapo wengi nowadays anaamua hataki kuolewa
anazaa tu na mtu but hataki ndoa

tembea uone

na wapo ambao anazaa na mtu kwa uamuzi wake tu binafsi
bila kumshirikisha anaetaka kuzaa nae
 
Inabidi ifikike kipindi jamii yetu iondoe dhana mbovu iliyojengeka mwanamke asipoolewa anakuwa na tatizo fulani nadhani inaweza kupunguza mihemko ya ndoa kwa dada zetu inaweza kusaidia kupunguza tatizo hili.

Hili lina ukweli

But usisahau hata hao single moms wengine wanachagua sana pia wachumba
na sio kwamba wote hawapati wachumba
na single mama wengine wako single by choice na still wanalia kama wanaonewa..
kuolewa hawataki....
 
Back
Top Bottom