barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,865
Diwani kata ya Siuyu (CHADEMA), Jared Jastin ahukumiwa kifungo cha miezi 6 jela kwa kumzuia mkusanya ushuru na kuikosesha serikali mapato.
Hukumu hiyo imetolewa ili kukomesha tabia ya diwani huyo ambaye alikuwa anapinga ushuru wa mageti ya mazao ya misitu na mazao ya chakula ambayo yalionekana kuwa kero kwa wananchi na wanakijiji kwa ujumla.
Serikali ya Kata ya Siuyu imekuwa ikitoza ushuru hata wa kuni za kupikia ugali huku ikiwaachia wafanyabiashara wakubwa wanaotoka nje ya kijiji hicho wanaobeba mkaa kwa malori na kuusafirisha mkoani Mwanza na Arusha.
Kata hii ipo katika Jimbo la Mh.Tundu Lissu Singida Mashariki ambaye naye amekuwa akipinga ushuru mdogo mdogo kwa wananchi wake.Vipi Mh.Tundu Lissu Wakili,diwani wako mpaka anafungwa hakupata msaada wa kisheria?
================
Singida. Mahakama ya Mwanzo ya Ikungi mkoani Singida leo imemuhukumu Diwani wa kata ya Siuyu tarafa Mungaa (Chadema), Jared Mahami Jastin (34) kifungo cha miezi sita jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuikosesha serikali mapato.
Imedaiwa mahakamani hapo kwamba mnamo Februari mbili mwaka huu saa tatu asubuhi huko katika mnada wa kijiji cha njiapanda wilaya ya Singida, mshitakiwa kwa makusudi alimzuia afisa mwidhiniwa Amina Abdallah wa kampuni ya Abada Care Investment, kufanya kazi ya kukusanya ushuru wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Mapema ilidaiwa katika Mahakama hiyo iliyokuwa chini ya hakimu Simon Jiwawa Kayinga, kuwa katika siku ya tukio, alitenda makosa mawili ikiwa ni kumuzuia afisa Amina kufanya kazi yake ya kukusanya mapato ya halmashauri kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 12 para ya (e) sheria ndogo ndogo ya halmashauri ya Ikungi.
Aidha, mshitakiwa pia alituhumiwa kutenda kosa la kushawishi wananchi waache kuchangia mapato kwa halmashauri yao kinyume na sheria ndogo ndogo kifungu cha 12 (1) (c).
Hata hivyo, hakimu alitupilia mbali tuhuma ya kosa la pili kwa madai kukosekana kwa ushahidi wa kutosha kumtia hatiani mshitakiwa diwani Jared.
"Kwa kosa la kwanza la kumuzuia afisa wa kukusanya mapato yaliyobainishwa na halmashauri ya wilaya ya Ikungi,ushahidi wa upande wa mlalamikaji,umethibitisha bila kuacha shaka yo yote kwamba una hatia kama ulivyoshitakiwa",alisema hakimu huyo na kuongeza;
'Kwa hali hiyo,mshitakiwa Jared utaenda mahabusu ya gerezani kutumikia jela miezi sita,ili iwe fundisho kwako na kuogopesha madiwani wengine wanaotarajia kufanya kosa la kuzuia kufanyika kazi halali".
Chanzo: Mwananchi