Sina moyo wa kukopa kabisa

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,431
Hello wana Jf ..Natumaini mpo wazima

Jamani mwenzenu Sina Tabia za Kukopa Kabisa ...hii roho ya Kukopa Kwangu Sijui ipo wapi ... Yaani Nipo ladhi ku fight kutafuta Hela Mwenyewe Kwa Njia Yeyote ile Na Ninaipata Hiyo hela na kumaliza jambo langu Nililokusudia ila Sina Roho ya Kukopa Kabisa

Na Hii hali nahisi Niliipata Kipindi nipo Primary kuna Jamaa yangu Nilishawahi Muazima/Kopa Tsh 100 (mia). Sasa Kila alipokuwa akiniona Naenda Kuchukua Barafu au wakati wa Mapumziko anakuja Ananikaba Nimrudishie hela yake kwahiyo akikuta na Sh 20 au 50 anaichukua .. Nabaki na Njaa Mpk sa 8 bila kula... Kuanzia Hapo nikachukia kukopa Mtu hela kabisa ...Bora Niitafute Mwenywe kuliko Kukopa Kwa mtu.. Kwahiyo hata kama nina Lengo la Kununua Kitu cha Milioni kadhaa .. Unakuta Nafanya Kazi Au kuanzisha Mradi ili mradi tu nipate hiyo Million kutoka kwenye Nguvu zangu kuliko kukopa Mtu halafu Tunaanza Kuzinguana baadae..

Sometimes Huwa nagombana mpk na Mchumba wangu kwa Tabia Zake za kukopa kopa sanaa hasa Vocha za Mitandao nipige tafu sijui.. Maana Sometimes ana hela Kabisa Ila Utashangaa mikono ya Kukopa Inamuwasha eti kisa Duka Lipo mbali....

Kuna Quote Moja Ya Reginald Mengi aliiweka Kipindi cha Nyuma kwenye Mtandao wa Twitter kwamba "Mtu hawezi Endelea kama Hatokopa" mpaka Leo nikiifikiria Hii Quote Nashindwa kupata Muafaka je Ni kweli Au Mm ndo na matatizo ya Kutoona Faida za Kukopa?


Na Ukizingatia Huku Kwetu Kuna Watu wamekopa Wanaishia kuja Kufilisiwa ..mtu kakopa Million 1 mara Jamaa Wanakuja kuuza Nyumba ... Mtu kakopa Kajenga Nyumba kubwa ya Kupanga Kesho kutwa Inapigwa Mnada... Yaan Hapo tu Moyo wangu Huwa Unasita Kabisa hasa Inapotokea Huna cha Kurudisha
 
kama unaona katika kupigana kwako na life unafanikiwa pasi na kukopa basi kwako haina haja ila kwa wengine kukopa kupo pale pale na hiyo ni kuongeza mtaji tu na sio kwamba pesa ya mkopo ndo uanze nayo.
 
wengi wanakopa bila malengo,wengine wanakopa kwa kuiga tu .
Kuna watumishi wana mishahara ya milioni ,.lakini unakuta amekopa zaidi ya Benki/taasisi 4,anabaki na take home ya laki moja,na cha maana halichokifanya hakuna.
Ni bora kutokukopa kuliko ,kukopa Vila malengo mazuri/faida
 
Ha ha ha! Umenifurahisha sana & kunikumbusha mbali hasa hapo kwenye kukabwa na jamaa anayekudai enzi za utotoni na kuchukua mpunga wote.
 
Kwa mtu binafsi na maisha yako ya kawaida, unachofanya ni kizuri na inaonesha una nidhamu katika matumizi ya pesa. Alichosema Mengi ni kibiashara zaidi, si rahisi kuwa na mtaji mkubwa ili ufanye biashara kubwa kama hutakopa.
 
Mkuu maisha yana njia nyingi sana za kupitia ili kufanikiwa. Kwako wewe hiyo njia uliyoichagua inakufaa sana lakini wengine inaweza isiwasaidie hivyo wakaamua kupita njia nyingine ikiwamo hiyo ya kukopa, ndiyo maana ya ule msemo kuwa "kila mtu kivyake" Kwa mfano ukitaka kwenda Dar kutokea Mwanza unaweza tumia njia zifuatazo;
1.Njia ya anga - Ndege.
2.Njia ya reli - Treni, Miguu.
3.Njia ya barabara - Gari, Baiskeli, Pikipiki, Miguu
Kwa hiyo ukichukulia maisha ni safari basi mtu anayo hiyari ya kutumia moja ya njia hizo 3 hapo juu kufikia malengo yake - Kufika Dar.
 
Kukopa ndo mpango mzima! Obama mwenyew anakopa sembuse miye Loh! Teh! Mwaya kama unaamini katika kutokopa USIKOPE! Utaishia kudaiwa tu! Alaf raha ya mkopo ufanyie kitu kwa maendeleo ,we kopa alaf katolee mahari! Teh!
 
Kukopa ndo mpango mzima! Obama mwenyew anakopa sembuse miye Loh! Teh! Mwaya kama unaamini katika kutokopa USIKOPE! Utaishia kudaiwa tu! Alaf raha ya mkopo ufanyie kitu kwa maendeleo ,we kopa alaf katolee mahari! Teh!
Hivi Munkari?......
 
Kukopa ndo mpango mzima! Obama mwenyew anakopa sembuse miye Loh! Teh! Mwaya kama unaamini katika kutokopa USIKOPE! Utaishia kudaiwa tu! Alaf raha ya mkopo ufanyie kitu kwa maendeleo ,we kopa alaf katolee mahari! Teh!
Sasa Hadi mahari unakopa ... Yaani hela ya Mwanaume mwenzio unaenda Kuolea..
 
Tatizo hapa ni moja, tofautisha kati ya:
a) deni na
b) mkopo

Mkopo huwa haudaiwi, kinachodaiwa ni deni ... deni ni utumwa 100% Ila mkopo ni jambo la kawaida kwa walio wengi ndo maana Mengi anasisitiza kukopa.
 
Back
Top Bottom