hussein boxer
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 832
- 335
Pes,pesa pesa, tatizo noti mkuu
Kaoge na magadi utapata kama njugu
hauko serious mbona wako bwerereree hivyo, mi kila siku nakutana nao tena wao ndo wananililia mm..
ha haa jaribu kuwa serious.
Habari zenu wakuu, kwa ufupi ni kwamba tangu wazo la kutaka kuoa linijie nakosa mchumba ambaye yupo siriazi na maisha, umri wangu ni miaka 32 nimeona umri unaenda nami nahitaji kuwa na familia kama vijana wengine,.
Tangu mwaka 2012 wazo la kuoa lilinijia na mpaka sasa nilishapata wachumba 9 ni mmoja tu ndio nilisex nae. Wapenzi hao wote waliniacha kwa sababu mbali mbali kama umri, kwenda kusoma, usaliti n.k .
Kwa sasa nahitaji mke ila sipati na nikipata ni wale wasio na malengo yani wachunaji.
Nifanyeje wakuu au kuna mahali nakosea?
tatizo lako upo desperate unataka ndoa mkuu...
tengeneza foundation ya mahusiano kwanza afu ndoa itafata.. umri haujalishi ndoa ni mikiki mikiki mkuu ko tafuta mtu anae match na wewe anzia step ya chin kabisa urafiki msome mtu afu ndo ivyo vya mapenzi vianze la si ivyo we utaangukia pua kila siku
Kama ndo hivyo hama chama ulichopo kwani yawezekana
ndi kinaweza kuwa kinakupa hilo gundu lililokuganda ka ruba.
Pole sana mkuu, lakn usikate tamaa kwan Mungu bado anakuandalia yule atakekufaa daima, Mutumainie bwana naye atakutafutia wakufanana nae, hakika bwana hajakuacha,
Nashukuru sana kwa ushauri wako mkuu.
Huwa nasikia umri wa wanaume kuoa hauendi kwa hiyo usitie shaka. halafu unavyosema katika "wachumba" 9 mmoja tu ndo ulisex nae unamaanisha nini? unauelewa vipi uchumba yani. una uhakika uko tayari kuoa au unataka kuoa kwa sababu vijana wenzio wa umri wako wana familia? Umesema huna bahati ya kupendwa? Wewe mwenyewe unajipenda? una amani? huna msongo? huna upweke? Hangaika na wewe mwenyewe kwanza. Ukishakaa vizuri kimwili, kiakili na kiroho utanunurisha upendo, furaha na amani kwa hiyo utapendwa labda na kutamaniwa mpaka ushindwe kuchagua.
Pole sana mkuu, lakn usikate tamaa kwan Mungu bado anakuandalia yule atakekufaa daima, Mutumainie bwana naye atakutafutia wakufanana nae, hakika bwana hajakuacha,