#SimuliziZa116: Akutwa akimlawiti nduguye mwenye ulemavu wa macho

Sema Tanzania

JF-Expert Member
May 18, 2016
251
465
Mwezi Februari mwaka huu tulipokea simu toka shehia moja (jina tunalihifadhi) ambapo jirani alitueleza kisa cha kijana kumlawiti mwenziye mwenye ulemavu wa macho ilihali yeye ndiye muangalizi wake wa karibu. Anasema majirani walisikia kilio cha maumivu toka nyumbani kwa jamaa huyo na hivyo kuhamasishana hatimaye wakafika nyumbani hapo. Mtuhumiwa baada ya kusikia makelele ya majirani alitimka lakini alikimbizwa na hatimaye kukamatwa na majirani.

Walimfikisha kituo cha polisi jirani na ndipo tukapigiwa simu kwani hawakuridhika na huduma. Baada ya kuwasiliana na OCD na Afisa Ustawi wa Jamii wa eneo hilo tulifanikiwa kufungua jalada na kumpeleka ndugu allolawitiwa hospitali kwa vipimo. Hata sasa jalada la kesi hii lipo katika mahakama kwa kupata haki.

Amini usiamini, tafiti zinaonesha nyumbani ni sehemu inayoongoza kwa ukatili katika jamii zetu. Ukatili unaotendeka majumbani mara nyingi hufunikwa na ndugu, jamaa na majirani. Usikubali kukaa kimya. Tupigie namba 116 nasi tutafuatilia.
 
It's a scary world out there. Mkuu asante sana kwa mada mbalimbali za malezi katika jamii ila mimi nilichojifunza ni kwamba kazi kubwa ya mzazi ni kusugua goti mbele za Mungu linapokuja suala la malezi.
 
Back
Top Bottom