Simulizi za sasa

Simulizi za sasa

Japhet Lufungulo

New Member
Joined
Sep 2, 2025
Posts
4
Reaction score
3
SIMULIZI-JAYLAN
MTUNZI-JAPHET LUFUNGULO
SEHEMU-01
Nø-+255680113178
MWANZO
Ni majira ya jioni angani ambapo katika ndege moja ya kijeshi ndani yake walionekana wanajeshi wakiwa katika purukushani za kuvaa parachuti zao kwa ajiri ya kuruka chini,kwa maana ndege ile upande wa kushoto wa injini ile ilikua ikiwaka moto mkubwa na kusababisha ndege ile kukoswa uelekeo.

Ndipo sasa anaonekana binti mmoja ambae mda huo ndio alikua anazinduka toka alipopoteza fahamu,maana kumbukumbu za mwisho zilimjia akikumbuka alizimishwa na kitako cha bunduki na kumfanya azirai.basi binti huyo alitizama ndani ya ndege ile na kuona wanjeshi wengi wakiruka kwa kuachiana nafasi kidogo ndipo sasa aligundua ndege ile ilikua imepata hitilafu kwa kushambuliwa injini maana mda ule ilikua ikiyumba yumba sana bila hata ya kukoma.

Hata wale wanajeshi hawakua na mda na binti huyo ambae mpaka sasa hivi mimi na wewe bado hatujamjua ni nani na anafanya nini kwenye ndege ile.ndipo sauti ya mwanajeshi mmoja ambae alikua wa mwisho ukiachana na pilot ( yaani dereva wa ndege ile )alimfata pilot na kumwambia kwa sauti ya juu kua hakuna mda wanatakiwa kuruka na alitakiwa kuielekeza ndege ile kwenye mlima mkubwa uliokua mbele ili baada ya wao kuruka basi ndege ikajibamize kwenye mlima ule.

Taarifa zile zilimfikia huyo binti ambae mikono na miguu yake ilikua imefubgwa na kamba maalumu na kujua mara moja ni kitu gani kilichokua kinafatia maana kilikua ni kifo maana alijua lazima walipanga kumuacha ili afe na ndege ile.

Basi mwanajeshi yule aliruka na kumuacha pilot nae akianza kutembea lilipo boksi kubwa la kuhifadhia parachuti lililokua limening'inizwa kwenye ukuta wa ndege ile.

"Mungu wangu limebaki moja tu" aliongea kwa sauti ndogo binti yule baada ya kushuhudia vile na kujua kama akifanya tu uzembe basi alikua anaenda kufa kifo kibaya sana, haraka sasa alikohoa kidogo hali iliyomfanya pilot yule kugeuka nyuma na kumtizama binti huyo
"Najua mda si mrefu nitakufa ila nilikua naomba ombi moja tu kabla hujaruka na kuniacha" aliongea vile binti huyo huku akimtizama pilot yule kwa macho malegevu kana kwamba alikua anataka kusinzia hali iliyomfanya pilot yule kuchomoa bastola yake huku akimsogelea na kichwani mwake alijua kabisa hakutakiwa kujisahau maana binti yule alikua mpiganaji mzuri ndio maana alichomoa bastola endapo kama ikitokea la kutokea pindi takapomsogelea basi amfyatulie risasi pale pale.

Ni kweli pilot yule alimsogelea binti yule huku mkono wake mmoja alianza mtomasa chuchu zake zilizokua zimesimama dede ndani ya tisheti ile nyeusi aliyokua amevaa pamoja na jinsi ya kubana vizuri mwili wake.

Lakini wajiwa wanaendelea na lile zoezi ilisikika alamu ikiwa inalia kuashiria mbele kulikua na hatari ya kugonga mlima na ndege ilikua inaelekea upande huo, haraka sasa pilot yule aliacha kuchezea chuchu za binti yule na kutaka kukimbulia mlangoni kwa ajili ya kujirusha ila ghafla alishtuka hasa baada ya kuona mikono ya binti yule ikitokea nyuma ya mgongo wake huku mkono wake wa kulia ukiwa umeshikilia kisu kidogo na haikuchukua sekunde pilot yule alianza kuhaha baada ya kisu kile kupita ndani ya koo lake huku damu nyingi zikiendelea tu kumtoka.

Haraka sana binti yule alikata kamba za mguuni na kuusukuma mwili wa pilot yule nje huku na yeye pale pale akijirusha ulipoelekea mwili ule na ni mita kadhaa tu kilisikika kishindo pamoja na mlipuko mkubwa sana baada ya ndege ile kugonga mlima uliokua mahala pale.

Binti yule aliufikia mwili wa pilot ambae mda huo alikua ametulia tu kuashiria alikua ameshakata roho akiwa angani kuelekea chini, basi binti yule alivuta kamba ndogo iliyokua kwenye begi lile alilokua nalo pilot na hapo hapo parachuti ilichomoka hali iliyofanya wao kurudi juu kidogo.

Sasa huku chini wale wanajeshi ambao walikua wamesharuka kwenye ndege ile waliona parachuti ile kwa mbali na moja kwa moja kujua alikua ni mwenzao pilot akishuka kwa hiyo moja kwa moja walianza kuelekea huko ili kukusanyana ili waijiwe na magari yao ya kijeshi kwa ajili ya kurejea kambini kwao na mda huo tayari ki giza kilikua kimeanza kushika hatamu kutfuta majira ya saa moja.

Binti yule baada ya kutua chini haraka alichomoa bastola iliyokua kwenye kifuko cha kombati ya pilot yule na kuishikilia huku haraka akianza kukimbilia msituni huko kwa sababu kwa mbali alianza kuona tochi nyingi zikija uelekeo wake.

TURUDI UPANDE MWINGINE
ikiwa ni majira ya saa moja na dakika zake alionekna kijana mmoja ambae mda huo alikua akitoka ndani ya supermarket moja katikati ya mji na moja kwa moja alielekea lilipokua gari lake aina ya toyota fortune nyeupe na kuingiza mizigo yake nyuma ya buti na n kuingia ndani ya gari lile na kutekenya funguo kuelekea kulia hali iliyofanya gari kuwaka mara moja na kuanza kuondoka maeneo yale kwa mwendo wa kawaida.

Huku nako wanajeshi wale baada ya kufika maeneo ya mbele waligundua kua pilot alikua ameshakufa na dalili zote za kua huenda binti yule waliemuacha ndani ya ndege ile tayari aliponea na atakua anatoroka,ndipo sasa wanajeshi wale walisogea mbele na kukuta magari yao yakiwa ndio yanafika na haraka waliingia huku target yao ilikua ni kumsaka binti yule ambae mimi na wewe bado hatujaweza mjua jina.

Binti yule alikimbia ndipo sasa kwa mbele kama mita 400 aliona kuna barabara na upande wa kulia wa ile barabara aliona mianga mingi ya taa na kujua moja kwa moja walikua wapita njia,hivyo haraka alianza kukimbia kuelekea kule barabarani ambapo baada ya kufika bastola yake aliichomeka nyuma na kushusha tisheti ile huku akianza kupungia mikono magari yale ambayo kutokana na mianga ya taa kua mikubwa binti yule alishindwa kuona vizuri mbele.

"Mkuu mbele kuna raia anapunga mikono nafikiri anaomba msaada" ilisikika sauti ya dereva yule akiielekeza sauti yake kwa mkuu wao ambae nae baada ya jusikia vile alitizama mbele kuangalia huyo mpungaji alikua ni nani na jumbe mkuu huyo ndio wale wanajeshi walioruka mda mfupi kwenye ile ndege na ndio waliokua wanamtafuta binti huyo.

Je itakuaje kwa binti huyo ambae bado hajajua kama magari yale ni ya wale waliokua wamemteka na kutaka kumuulia ndani ya ndege
Je atafanikiwa kuwakwepa maadui hao ?

Mimi na wewe hatujui ila cha kufanya
like
share na
comment

maoni yako juu ya mwanzo mzuri wa simulizi hii ya kijasusi mapigano pamoja na upelelezi

Ndio kwanza tuko mwanzo mambo mazuri yatakua katika sehemu ifuatayo ambayo hiyo itakua ni sehemu ya 2 bye
IMG_1755885495225.png
 
Usijali vipande vipo vya kutosha ila nachopenda ni komment zenu juu ya ulichokisoma na wapi nakosea basi unakua ni mwanzo mzuri wa kurekebishana mkuu
 
Usijali vipande vipo vya kutosha ila nachopenda ni komment zenu juu ya ulichokisoma na wapi nakosea basi unakua ni mwanzo mzuri wa kurekebishana mkuu
Moja tu then umeshaanza kusikilizia comments! Hutopata wadau kwq mwendo huu. Anyway keep it up
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom