Iko njema hii.. imenikumbusha mwaka jana mwishoni nilifikia uamuzi wa kuuza mradi wangu ambao ulikuwa haufanyi vizuri kwa miaka miwili sasa..
Mapato yote yalikuwa yanaishia kwenye uendeshaji wa mradi pamoja na kulipa vibarua,tena ilikuwa haitoshi ilinibid nitoe tena pesa yangu mfukoni kwa ajili ya uendeshaji...
Nikaona bora niuze tu,ndugu pamoja na wengine walio kuwa wananufaika kwa namna fulani kupitia mradi,walinikalia kooni wakipinga kuuzwa kwa mradi.
Japo walikuwa hawanidai chochote,maana walikuwa wanalipwa kama vibarua wengine kutokana na kazi walizo kuwa wanafanya.
Nilisimamia uamuzi wangu, juzi ilibid niuze japo kwa hasara 7mil..
Ila kwa tathmini yangu,naona nmetua mzigo mzito ulio ninyonya kwa 2 yrs...ambapo ningeendelea nao kwa mwaka mwingine ningepigwa sio chini ya 3mil katika uendeshaji.
Lakini ndugu pamoja na wote walio nufaika na mradi hawaangalii hayo..hivo tuwe makini na wanao tushauri.