SIMULIZI : PETE YA MVUVI

SIMULIZI : PETE YA MVUVI

Abdallahking

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2018
Posts
3,985
Reaction score
10,843
0.jpg


SIMULIZI HII IMEKAMILIKA
IMEANDIKWA NA : LEICESTER PETRON
CHANZO : BURE SERIES


SEHEMU YA KWANZA

Kawaida kwenye maisha tunakumbushwa kupenda kujituma kwa bidii zetu zote pale tufanyapo kazi zetu, Lakini pia tunahamasishwa kupenda kazi tunazozifanya, haijarishi ziwe ni za kipato cha chini au juu bila kujali ni kazi ya kuketi ofisini ukiwa umezungukwa na vitendea kazi vya kisasa kama Kompyuta, (Printer) kifaa cha kutolea kazi iliyoomo kwenye kompyuta na kuifanya ionekane kwenye karatasi n.k, Pia usijali kama kazi yako ni yakuzunguka mtaa kwa mtaa ukitembeza bidhaa zako au kazi ya kibandani kama kuuza genge, saluni, mgahawa n.k, Ndugu zangu wapendwa zote hizi ni kazi na inabidi tuzipende kwa moyo mmoja, Usidharau kazi yako kwani hata wateja wako na jamii yako kiujumla watakudharau. Kwa maisha ya hapa nchini kwetu Tanzania sidhani kama kuna mtu mwenye uelewa wa jinsi gani maisha yanavyoenda atakayeweza kuchagua au kubagua kazi fualni, Japokua kumekua na tabia ya kuchagua au kubagua kazi, Tabia hii imewaadhiri vijana wengi hususani vijana wa mijini kwa kuwa na msemo unaotamkwa na wengi wao ukisema, “Aaaaah!!!! Bwana eeeeh!!! Kijana mtanashati kama mimi (Au binti mrembo kama mimi) Kazi hii ni ya kike (Au kazi hii ni ya kiume) hivyo siwezi kufanya mimi yani bora nilale njaa, Jamii yangu nitaiyonea aibu au nitachekwa” Msemo huu umekua maarufu sana hususani maeneo ya mijini kwani vijana wengi wamekua ni Mabrazameni na Masistaduu hivyo kazi za kutembeza bidhaa au kazi za vibandani hawawezi kufanya kwani watajishusha thamani na pia wanaamini jamii yao itawacheka, Kazi wazipendazo wao ni zile za kuvaa Suti kali na tai huku mkononi wakiwa na funguo za magari mazuri tena ya kifahari. Kwa uwelewa wa kawaida vijana kama hao ndio wanaorudisha nyuma maendeleo ya taifa letu kwani endapo wangejitolea kufanya kazi kwa wingi na kwa nguvu zao zote nina imani Tanzania yetu ingesonga mbele kwa kasi zaidi, ila badala yake utakuta vijana hao kwa upande wa mabinti utawakuta wapo teyari kuuza miili yao ili wapate pesa nyingi bila kufanya kazi yoyote ya msingi, huku upande wa wanaume wengi wao hujiiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya kutokana na kukosa kazi za kuwafanya wafikiri vitu vya maendeleo na badala yake wanaanza kuwa vibaka ili wapate pesa ya kwenda kununua Kete (Unga) au Ganja (Bangi). Hali hii inasikitisha sana kwani huwa tunapoteza vijana wengi kwenye umri ambao tunaamini wangeweza kusaidia kukuza uchumi wa nchi yetu. Mnamo mwaka 1995, Katika kijiji cha “Luvile” yakiwa ni majira ya asubuhi sana nikiwa nimeketi na babu yangu nje ya nyumba yetu nzuriii!! ya udongo, Babu alinisimulia hadithi nzuri sana ambayo ilinifanya nipende kazi yake ya uvuvi kwani babu yangu alipenda sana kazi yake na hivyo alinisihi nijisikie wa bahati sana kujifunza kazi ile ya uvuvi kwani babu yangu alikua mvuvi mkongwe sana kwenye ziwa lilipo kijijini kwetu, kwa kuwa nilikua na umri mdogo (Miaka 15) Babu hakuwahi kunielezea historia ya wazazi wangu kwani sikuwahi kuwajua Baba na Mama yangu japo hata kwa sura na kila nilipokua nikimuuliza Babu hakuwa teyari kuniambia ila alichokua ananiambia ni, “Joshua mjukuu wangu wazazi wako walikua watu wema sana na walikupenda sana ila ni mipango ya Mungu walikuacha ukiwa mdogo sana, naomba uwaombee wapumzike mahali pema peponi”, Kauli ile ilikua ikinifanya niwe mwenye mawazo sana kwani nilitamani japo nikaone makaburi yao ila babu hakuwahi kuniambia walizikwa wapi wala sababu ya kifo chao. Nilijijengea tabia ya kabla ya kulala na kila niamkapo lazima nipige magoti mbele ya kitanda changu na kuwaombea marehemu Baba na Mama yangu. Siku moja, Ikiwa ni mida ya jioni saa 12 Babu alinituma niende ziwani nikaangalie kama rafiki zake walishaandaa nyavu za kwenda kuvulia samaki, Niliondoka huku nikikimbia na nikiimba nyimbo zangu za kuwinda ndege, kwakua muda ulikua umeshakwenda na ziwa lile lipo mbali na makazi ya watu niliongeza mbio. Nikiwa njiani niliona mfuko mweusi ukiwa umetupwa kati kati ya njia ile niliyokua nikipita, nilisimama na kuutizama mfuko ule kwani niliona kuna kitu kinacheza cheza ndani yake, nilivuta pumzi na kisha niliufata mfuko na nilijaribu kuufungua……… Loooooooh!!!!! Mungu wangu!!! Sikuamini macho yangu kwani niliona katoto kachanga kakiwa kamefumba macho yake na kwa haraka nilimtoa ndani ya mfuko ule na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Nilipokua njiani kachanga kale kalianza kulia na nilisimama na kutoa shati nililokua nimevaa na kumfunika kwani nilihisi mtoto yule anapigwa na upepo ndio maaana alikua analia, wakati namfunika mvua kubwa sanaa! Ilianza kupiga huku radi nazo zikigangamaa…

Niliogopa sana na nilimuonea huruma mtoto yule aliyekua hana kosa lolote la kumfanya apitie shida zote zile lakini kwa roho ya kijasili niliendelea kuongeza mbio na hatimaye nilifanikiwa kufika nyumbani huku nikiwa nimembeba mtoto yule na mwili wangu ukiwa umeloa chapa chapa!!!!. Nilipoingia ndani ya nyumba nilimkuta babu akiwa anakoka moto kwajili ya chakula cha jioni ambacho huwa alikua anapika kwanza ndio aelekee ziwani kuvua samaki, Babu alinishangaa sana kwani aliona nimebeba kitu kinachovuja damu ndipo babu aliinuka alipokua ameketi na kwa kuogopa aliniuliza, “Joshua mjukuu wangu umeiba wapi hako kachanga ka mbuzi?” Babu hakujua kuwa yule ni binadamu na sio kachanga ka mbuzi, Babu alinisogelea na alipofunua shati langu nililomfunika mtoto yule, Sauti nzuri ya furaha ilitoka ikilia, Ngaaa!! Ngaaa!!! Ngaaa!!! Ngaaa!!! Mtoto yule alitoa kilio kile ambacho kilimfanya babu anipokonye na kumsogeza karibu na moto. Kwakua sikua na uelewa wowpte juu ya kitendo kile nilimwambia babu, “Babuuuu!!!! Usimuue huyo ni malaika wa Mungu usimchome moto” Babu alinijibu, “Joshua huyu mtoto anahitaji joto hivyo namuweka karibu na huu moto apate joto kwani mwili wake una baridi, tena nahisi atakua na homa” Babu aliniomba nielekee nyuma ya nyumba yetu nikamchumie dawa iliyokua ni majani ya Roswa yaliokua yakipatikana kwa nadra sana, nilitoka nje na kumletea dawa ile ambayo aliitwanga kwenye kinu na kisha kuchuja maji yake na kumnywesha mtoto yule huku majani yake akimpakaa mwilini mwake. Babu yangu siku zote alipenda kuamini sana dawa za asili kwani hakuwahi kutumia hata Panadol, Na mtoto yule kupitia dawa zile za asili alianza kuendelea vizuri. Ilipokua asubuhi sana baada ya muda wa miezi 6 kupita babu aliniamsha na kuniambia, “Mjukuu wangu mimi natoka naelekea ziwani kutafuta riziki hivyo nakuomba ubaki na mdogo wako Neema na uhakikishe unanywesha uji na anashiba , Usimuache peke yake kitandani ataanguka na kuumia vibaya, Sawa babu?” Nilimjibu, “Sawa babu usijali pia naomba Mungu akuongoze uende salama na urudi salama” Babu alifurahi sana na ndipo aliondoka kuelekea ziwani. Nilimpenda sana mdogo wangu (Neema) kwani nilihakikisha tangu nilipomuokota mpaka asubuhi ile aendelee kuishi vizuri na pale atakapokua mtu mzima nilipanga kumueleza ukweli wa kila kitu. Majirani zetu hawakujua Neema ni mtoto wa nani wala kafika vipi pale kijijini na kila nilipokua naulizwa niliwajibu, “Neema ni mtoto wa Shangazi yangu yupo mjini kapatwa na tatizo kidogo hivyo kaniomba mimi na babu yangu tumsaidie kulea”. Kawaida ya Babu kurudi nyumbani ilizoeleka kuwa ni saa 10 jioni ila alipokua akichelewa sana pale alipokua akipitia kilabuni kupata chupa mbili tatu za kilevi alikua akifika nyumbani saa 12, Ila leo tangu alipoondoka asubuhi ile na mapema ikiwa ni saa 2 usiku hakuwa amerudi nyumbani, Niliogopa sana kwani muda ule upepo mkali na mvua kubwa Sanaa!! Ilianza kunyesha huku Neema akiwa analia njaa kwani tangu nimpe uji wa asubuhi nilikosa cha kupika kwani nilikuwa nikimsubiri babu arudi na unga nimpikie uji mdogo wangu. Hali ya hewa ilizidi kuwa mbaya ila nilijaribu kumbembeleza Neema alale na alipolala nilitoka na kuelekea kwa jirani yetu wa karibu Mzee Magori ili nimuombe baiskeli yake nielekee ziwani kumuangalia babu yangu kwani nilihisi kuna kitu kibaya kimemtokea…

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA PILI

Kila nilipojaribu kugonga mlango wa Mzee Magori sikupata majibu kwani ndani kwake kulikua na giza lililoashiria mlango ule umefungwa nay eye pamoja na familia yake walikua wameshalala, Hivyo nilizunguka uwani kwake ndipo kwa bahati nzuri baiskeli yake aliisahau nje. Niliichukua na kuanza safari ya kuelekea ziwani kumuangalia babu yangu, Mvua kubwa iliendelea kunyesha lakini sikukata tamaa niliendelea kuendesha baiskeli ile kwa haraka mno. Nikiwa njiani kwa bahati mbaya tairi ya mbele ya ile baiskeli ilipasuka, Hivyo ilinilazimu nishuke na kuikokota baiskeli huku nikitembea kwa haraka na moyo wangu ulijawa na wasi wasi mno kwani nilianza kuhisi mikosi hii inawezekana ikawa babu yangu amepatwa na matatizo. Mvua iliendelea kuongezeka kila baada ya dakika huku radi kali zikipiga na kufanya miti kuanguka, Nilizidi kuogopa sana kwani nilikua katikati ya pori ambalo ni lazima upite pindi uendapo ziwani na pori lile lilijulikana kwa kuwa na wanyama na viumbe wa ajabu ajabu pindi tu ifikapo usiku. Nikiwa natembea huku nikikokota baiskeli ghafla nilimkanyaga nyoka aliyekua na rangi nyekundu huku kichwa chake kikiwa na pembe mbili kama za mbuzi, Nyoka yule alinirukia kiunoni na alipojaribu kuningata tumboni nilimshika kichwa chake na kumtupa chini kisha niliitupa ile baiskeli na kuanza kukimbia, Nilipokua nikikimbia nilijiuliza sana ujasiri ule wa kumshika mnyama hatari kama yule niliutolea wapi!? Ila niliamini ni Mungu tu! aliniepusha na balaa lile. Pori lile lilikua ni kubwa sanaaa!! Hivyo juhudi zangu za kukimbia zilifika ukingoni kwani pumzi iliniishia huku pia miguu iliishiwa nguvu kwani nilikua nikikimbia kwenye matope na madimbwi makubwa ya maji huku nikitobolewa na miiba, Nilisimama kwa dakika chache nikiwa nafuta pumzi na kutafuta nguvu za kuendelea na safari ya ziwani, Nilisikia sauti za fisi na vishindo vyao na kwa mbali niliwaona fisi wawili wakiwa wananifata kimya kimya na waliponiona tu! walianza kunikimbiza. Nilianza kukimbia na uchovu ule huku nikiwa nikimuomba Mungu na kwa sauti nilisema, “Mungu weeeeee!!! Mungu!!!! Niokoe mimiiii!!!” nilitamka maneno yale huku nikiendelea kukimbia mara ghafla sikusikia sauti wala vishindo vya fisi wale hivyo nilisimama na nilipojaribu kukohoa nilikohoa damu nzito huku pua zangu nazo zilianza kutokwa na damu, Maskini!!! Hali yangu ilikua mbayaaa mnoo…Nilikumbuka msemo wa babu uliosema, “Mwanaume ni shujaa na kila apatapo majaribu basi hana budi kupambana kuyashinda” Hivyo msemo ule ulinipa nguvu ya kuendelea kutembea na baada ya muda wa dakika 10 nilifanikiwa kufika ziwani. Nilitazama huku na kule nikitafuta mtumbwi wa babu ila sikufanikiwa kuuona japo kwa mbali, Machozi yalianza kunitoka taratibu taratibu na kadri nilipokua nikiangalia ziwa lile bila kuona dalili yoyote ya babu yangu kurudi nilianza kulia kwa nguvu kwani nilihisi kuna kitu kibaya kimemtokea babu. Ghafla kuna kitu kiliugusa moyo wangu na nilinyamaza, nilikumbuka nimeacha mlango wa nyumba yetu wazi na huku ndani nilimuacha mdogo wangu Neema, Nilishtuka sana na kusema, “Mungu wangu kumbe nimeacha mlango wazi?” Niliogopa sana kwani kawaida ya kijijini kwetu pindi mvua kubwa inyeshapo huwa kuna wanyama na wadudu kama nyoka na nge huwa na tabia ya kuingia ndani ya nyumba za watu kutafuta joto. Nilizidi kuogopa kwani ni lazima nipite tena kati kati ya lile pori lakini kutokana na upendo wa dhati niliokua nao kwa mdogo wangu (Neema) nilijikaza kiume na nilifanikiwa kupita bila kufukuzwa na mnyama yeyote. Nilipofika karibu na nyumba yetu nilimuona nyoka mkubwaaa!!! Akiwa anatoka ndani ya nyumba yetu huku tumbo lake likiwa limejaa. Daaaah!!!! Niliishiwa nguvu kabisaaa!! Kwani nyoka yule alikua mkubwa sana na alitoka huku akionekana amekula kitu na nilihisi atakua amemmeza Neema, Nilimsubiri nyoka yule apotee kabisa na ndipo kwa haraka sana nilikimbilia ndani na moja kwa moja nilielekea chumbani nilipokua nimemuacha Neema. Kwa bahati nzuri nilimkuta neema akiwa ameamka huku akicheza cheza na shuka, Nilihema kwa nguvu na kusema, “Ooooooh!! Asante Mungu”. Nyoka yule alimeza kiroba kilichokua na mabaki ya samaki na nyama ya mbuzi. Nilirudishia mlango wa nyumba yetu na kisha nilipanda kitandani kulala, Nikiwa ndotoni niliota ndoto mbaya sana kwani niliota nipo msituni nikizungukwa na watu waliokua na sura za wafu huku shangazi yangu aishio mjini akiwa na kisu kikali kilichotapakaa damu ya babu. Sikuweza kuendelea na ndoto ile kwani Neema alishtuka na kuanza kulia……

na kwa uwelewa nilijua ana kiu cha maji, Hivyo nilitoka kitandani kumfatia maji na kumnywesha baada ya muda kidogo alilala. Baada ya kuota ile ndoto sikupata usingizi kabisa kwani nilianza kuitafakari ile ndoto huku nikitokwa jasho na mikono yangu kutetemeka, Nilizidi kuogopa na nilikua nikitamani asubuhi ifike mapema. Asubuhi ilifika na mlango wa nyumba yetu uligongwa kwa nguvu, Mimi nilikua bado usingizini ila kwa mbali sana nilisikia sauti za watu zikisema, "Joshuaaaa!!! Weweee!!! Amkaaaa!! Babu yako ana hali mbaya sanaaa!! Fungua mlango" Mhhhh!!! Niliposikia jina la babu yangu limetajwa nilishtuka mara moja na nilitoka nje kuona ni nini kiliendelea. Maskiniiii!!!! Nilimuona babu yangu akiwa amelazwa chini huku anatokwa na damu za pajani na kifuani huku sura yake ikijawa na uchungu kwa kuvumilia majeraha yale, Babu aliniambia,"Joshua baba naomba uniletee maji kwenye kikombe changu cha kahawa" Nilinyanyuka haraka na nilimletea maji, Babu alikunywa yale maji na yalipofika nusu kikombe aliniangalia kwa huruma na kisha alisema,"Mjukuu wangu kikombe hiki na maji haya nakukabidhi yawe baraka zangu kwako na mdogo wako, Pia nakuomba uzisimamie mali zangu vizuri ukiwemo mtumbwi wa kuvulia samaki na hili shamba lililopo hapa nyumbani, Babu yako sidaiwi chochote na mtu yeyote yule hivyo asije mtu akakudanganya, Joshua Mungu akusimamie, Kwaheri mjukuu wangu" Kabla hata sijaanza kumuuliza kwanini ananiambia maneno yote yale, Babu yangu alifumba macho huku pumzi yake ikikata, Maskini babu alifariki akiwa mikononi mwangu....Kifo cha babu yangu kilisababishwa na majeraha makubwa aliyoyapata baada ya kungatwa na fisi alipokua akirejea nyumbani usiku ule ambao masaa machache kabla ya tukio lile nilienda kumtafuta eneo zima la pale ziwani lakini sikumuona. Kuchelewa kwa babu yangu kurudi nyumbani kulisababishwa na upepo mkali uliokua ziwani huku zile mvua zilizopiga kwa nguvu mno zilimfanya babu pamoja na rafiki zake kusubiri mpaka upepo na mvua ile kubwa ipungue, Na usiku huo walirudi wakiwa na furaha mno kwani walivua samaki wakubwa na wengi sana hivyo kwa furaha ile babu pamoja na rafiki zake walielekea moja kwa moja kilabuni japo kujipongeza na chupa kadhaa za pombe aina ya BALIMI, Babu yangu hakutaka kunywa pombe hivyo aliwaacha rafiki zake yeye alianza safari ya kurudi nyumbani, Kumbe alipokua kati kati ya lile pori alikua amebeba mfuko mkubwa uliojaa samaki huku alikua akiimba nyimbo zake kwa kupiga miruzi. Harufu ya samaki wale na mlio ule wa mruzi uliwakurupusha fisi na hivyo walitafuta harufu hiyo ipo wapi na walipomuona babu akiwa na mfuko mkubwa wa samaki, Kwa nguvu walimshambulia babu na kumjeruhi sehemu kubwa sana mwilini mwake. Maagizo yake yote aliyoniachia marehemu babu nilianza kuyatimiza pale tu! tulipomaliza kumzika,lakini kwa kuwa nilikua mdogo kujua nini hatma zile mali zake niliona ni vizuri nimshirikishe Shangazi yangu kwani yeye ndiye aliyekua mtoto wa pekee aliyebaki kwa babu yangu. Nilimueleza Shangazi kila kitu nilichoambiwa na babu huku nilimpa zile karatasi ambazo sikujua maana yake ni nini?, Shangazi alishtuka sana kwani aliona jina langu kwenye kila karatasi zile ambazo ni hati za mali za marehemu babu yangu. Shangazi yangu kwa hasira alisema, “Niniiiiiii!!!!? Eboooo!!? Joshua? Yani wewe ndio mrithi wa mali za baba yangu? Thubutuuu!!! Labda mimi sio binti wa marehemu” Niliogopa sanaaa!! Kwani aliongea kwa hasira huku macho yake yalianza kubadilika na kuwa myekundu, Kwa uwoga ule niliondoka eneo lile na kukimbilia ndani kumuangalia mdogo wangu (Neema) asiyejua lolote lilokua linaendelea. Enzi za uhai wa babu yangu alipenda sana kunisihi nisije nikamuamini Shangazi yangu hata chembe lakini nilikua sina wa kumuomba msaada kwa mzigo ule mzito wa kusiamamia mali niliokua nimekabidhiwa na marehemu baba kwani umri wangu ulikua ni mdogo kuweza kuhimiri jukumu lile peke yangu……

ITAENDELEA

CHANZO : BURE SERIES
 
SEHEMU YA TATU

Baada ya muda wa siku tatu kupita Shangazi aliniomba nikaishi nae mjini huku akinilazimisha nimuache mdogo wangu Neema kwa jirani kwani aliniahidi atanipeleka shule ya ufundi nikasomee Umeme, Nilikataa katu katu!! Kumuacha mdogo wangu kwa jirani kwani Neema alikua mdogo sana kuachwa mikononi mwa watu asiowajua. Niliendelea kusimamia msimamo wangu ule ule na ndipo Shangazi alikubali niondoke na mdogo wangu kuelekea mjini alipokua anaishi na familia yake. Nilimfunga Neema mgogoni na kipande cha msuli wa marehemu babu na tulipofika stendi ya magari Shangazi aliniambia, “Sasa wewe mtoto naomba unisikie tena unisikilize haswaaaa!!! Huyo mtoto wa kuokota uliyengangania uende nae kwangu!! Mimi sina hela ya kumlisha hivyo basi sitaki nisikie unaniomba ela ya uji sijui maziwa!! Hilo kwangu hapana, Umenielewaaa!!??” Shangazi aliongea kwa hasira sana huku akimfinya Neema mashavuni na mimi akinibamiza kofi la shavuni. Maskiniii!!! niliumia sana kuona maisha yetu yanabadilika na kuwa maisha ya kuteseka kwani enzi za uhai wa babu tulikua tukiishi kwa upendo na Amani licha ya kuwa na kipato cha chini lakini sasa nilienda kuanza maisha ya mateso na manyanyaso huku nikiwa na mtoto mdogo asiyejua kinachoendelea. Safari ya kuelekea mjini ilianza na tulipokua njiani Neema alianza kulia na kwa kuwa nilishamzoea mdogo wangu nilihisi itakua ni njaa, niliogopa sana kumwambia Shangazi kwani alishanionya nisimwambie habari zozote kuhusu Neema. Kila dakika iliyosogea mbele Neema alizidi kulia kiasi cha kuwafanya abiria wote kuamka kwani alilia sana na niliposhika kichwa chake kilikua ni cha moto, Nilinyanyuka na kuomba abiria wanisikilize japo nipate msaada, nilisema, “Shikamooni wote, Mimi naitwa Joshua na huyu ni mdogo wangu anaitwa Neema tunasafiri kuelekea mjini na hatuna msaada wowote ule, Mdogo wangu analia kwasababu ya njaa kwani hajala tangu asubuhi na sasa ni saa 12 jioni, Baba na mama zangu naomba msaada japo mdogo wangu ale tu! Mimi nitavumilia”. Macho ya Shangazi yaliniangalia vibaya mno huku yakianza kubadilika na kuwa myekundu, Kwakua sikusema tulikua tunasafiri na Shangazi yangu hivyo Shangazi alijifanya kama mtu mwema alinyanyuka na kunifata kisha alininongoneza akisema, “Wewe mtoto hunuji eeeh?? Yani unataka kunihaibisha mbele za watu sasa subiri uone, mlete huyo paka wako” Shangazi alionyesha tabasamu la kinafki na kunipokonya Neema huku akiwaambia abiria wale waliokua wakinisikiliza huku wakionyesha sura za huruma, “Msijali ndugu zangu nitamsaidia huyu mtoto, nimeguswa Sanaa na alichotuambia” Abiria wale hawakujua kilichokua kinaendelea hivyo walimpigia makofi shangazi na kumsifu kwa moyo wake wa huruma. Neema alikunywa uji baada ya kupata msaada kwa mama mmoja aliyekua na mtoto mdogo umri sawa kidogo na Neema, Ilipofika usiku wa saa 4 nikiwa ndotoni niliota ndoto mbaya sana kwani niliota sauti ya shangazi ikiniambia “Joshua nisikilize vizuri huyu mtoto hana faida yoyote kwako ni mzigo tu! Giza litakapoingia nitakusaidia kumtupa nje ya basi hili bila mtu yoyote kujua, Sawaaa Joshuaaaaa!!!” Nilishtuka!! Na nilipojaribu kupapasa mapajani mwangu nilipokua nimemlaza Neema sikubahatika kumgusa huku nikiangalia alipokua amekaa shangazi yangu sikumuona, Mapigo yangu ya moyo yalienda mbio sanaa……Nilisema moyoni mwangu, “Neema yupo wapi Mungu wangu, au shangazi kashamtupa dirishani? Maana hii ndoto si bureee!!” Niliendelea kumtafuta mdogo wangu na kwa bahati nzuri kumbe yule mama aliyenisidia uji wa mwanae nikamnywesha mdogo wangu (Neema) alimchukua ili acheze na mtoto wake. Niliporudi kuketi nilijikutta nikikalia kifuu kilichokua na maji ya moto, Ghafla nilinyanyuka na nilipojaribu kukitoa maji yale yalikauka mara moja huku kifuu kikipotea bila kuelewa nini kinaendelea. Shangazi yangu alikua amelala huku akikoroma kama shetani na ghafla niliona vitu vya ajabu kama funza wa chooni wakimtoka shangazi puani, mdomoni na masikioni, Mungu wangu!!! Nilijisemea moyoni, “Shangazi mbona anatoa funza mwilini mwake? Ameoza au macho yangu hayaoni vizuri? Eeeh Mungu ni balaa gani tena hili?” Kwakua abiria wengi walikua wamelala pemebeni yangu nilikaa na mzee mmoja wa kitanga (Msambaa) nilishindwa kuvumilia kwani niliogopa sana na ndipo nilimuamsha mzee yule na alipoamka nilimuonyeshea maajabu yale, Mzee hakusema chochote aliangalia funza wale na kisha alicheka kidogo na kurudi usingizini. Nilizidi kupatwa na maswali juu ya hatma yangu na mdogo wangu pindi tufikapo mjini kwa shangazi, Nikiwa nawaza ghafla nilipojaribu kumuangalia tena shangazi tulikutana macho kwa macho huku funza zile zikiwa zinarudi mwilini mwake, Nilipiga kelele kwa nguvu nikisema, “Jamaniii!! Eeeeeh!!! Nakufa mimi!!!” Abiria wa basi lile hawakuamka hata mmoja, kilichonishangaza zaidi hadi wale waliokua macho walipata usingizi wa ghafla na kulifanya basi lile kuwa kimya huku dereva wa basi lile akiwa anapiga miyayo ya usingizi na baada ya sekunde chache basi lile lilisimamishwa na dereva alilala. Shangazi yangu alikua na nguvu kali sana za kichawi na niliamini hilo baada ya kuamua kuchukua watoto wote wa kwenye gari lile na kuondoka nao bila mtu yeyote kujua zaidi ya mimi na yeye tu!. Shangazi aliwachukua watoto wale akiwemo Neema na kuwakabidhi wachawi wenza waliokua wamalizunguka basi lile kama sadaka yake kwao, Niliishia nguvu ya kujaribu kumpokonya mdogo wangu na kila nilichokua naongea kilikua hakisikiki wala hakitoi sauti. Maskinii!! Shangazi alinichukulia mdogo wangu kipenzi pamoja na watoto wengine wa abiria wa basi lile bila kujua anaenda kuwafanyia nini yeye pamoja na wachawi wenzake…

Nilimkumbuka sana marehemu babu kwani alipenda kunisihi kila jaribu huja kwa maana yake na linaweza likaja kwa nia ya kukujenga au kukubomoa, hivyo niliichukilia hali ile kama sehemu ya maisha yangu ambayo niliamini Mungu ana makusudi yake ya mimi kupitia wakati ule mgumu. Asubuhi ilifika huku sauti za abiria wengi zikilalamika kuwa wamechoka sana huku wengi wao wakiumwa na viungo vya miili yao na uchovu ule ni kama walifanya kazi ya kulima usiku kucha, Kumbe uchawi wa Shangazi uliowafanya walale ndio uliwachosha na kuwaumiza viungo vya miili yao. Mama mmoja aliyekua ameketi mwisho kabisa wa basi lile alianza kupiga kelele akisema, “Jamani dereva hebu simamisha gari tafadhali” Dereva alisimamisha gari na mama yule aliendelea kuongea, “Jamani abiria wenzangu nimepotelewa na watoto wangu mapacha wawili wa kike siwaoni, naomba mnirudishie watoto wangu” mama yule alianza kulia na baada kumaliza kuongea mama wengine waliokua na watoto pia walishtuka kwani hakukua na mtoto hata mmoja. Mzozo wa kelele na vilio vya kina mama vilianza kwani watoto wote walipotea katika mazingira ya kutatanisha, Lakini mimi nilikua najua kila kitu ila sasa Shangazi alinitupia ububu wa muda hivyo sikuweza kuongea chochote ila nilitamani niseme ukweli kwani tukio lile nililiona na lilikua la kinyama sana kwani watoto wale akiwemo mdogo wangu (Neema) walifungashwa kwenye kiroba cha mkaa bila kujali kuwa wengine ni vichanga na wengine kidogo viungo vyao vimekomaa na kusafirishwa hadi makao makuu ya uchawi wao. Yule mzee wa kitanga aliyekua ameketi pembeni yangu alihisi kuna kitu nafahamu juu ya kupotea kwa watoto wale kwani nilipomuamsha aone wale funza waliokua wakimtoka shangazi yangu puani, mdomoni na masikioni mzee yule aliona kama ni ndoto ivyo hakuitilia maanani lakini mzee yule alinisikia nikiongea na nikitaja jina la shangazi yangu hivyo alishangaa sana kuona nimekua bubu ghafla. Mzozo ukiwa unaendelea huku basi likiendelea na safari, Mzee yule alinipa kalamu na karatasi japo nimuandikie tukio zima lilivyokua kwa bahati mbaya nilishindwa kwani sikuwahi kwenda shule hivyo sikujua kuandika wala kusoma. Wakati safari ikiendelea huku vilio na kelele zikishamiri, Ghafla!!! mbele ya kioo cha basi tulilokuwemo nyama za mikono, miguu, kichwa cha mtoto zikiwa zimekatwakatwa zilitupwa mbele ya basi letu huku damu zikiwa na maandishi yaliyosema, “BADO DAMU YA MTOTO MMOJA”. Dereva alisimamisha basi kwa haraka mno na abiria wote tulishuka kushuhudia tukio lile ndipo mama mmoja aligundua mtoto yule aliyekatwakatwa alikua ni mwanae kwani alikua na alama ya kuungua kwenye eneo kubwa la paja lake, Vilio vilianza huku maombi ya kumkemea shetani yakishamiri kwa kasi ya hatari na nilipomuangalia Shangazi sikumuona eneo lile wakati abiria wote tulikua eneo lile. Yule mzee wa kitanga alitoa msaafu wake na kuomba apewe muda wa nusu saa afanye swala zake kisha tuendelee na safari, Abiria wote tulikubaliana nae na aliomba kisha tukaanza safari, Ilipofika mida ya saa 2 usiku nilianza kuogopa sana kwani mtoto niliyebaki kwenye basi lile ni mimi tu! Na ujumbe ule wa kishirikina ulitaka damu ya mtoto mmoja. Nikiwa nashangaa nje ghafla niliona shangazi akishushwa kwenye mbawa ya mnyama wa ajabu ambaye alifanania na mwewe mkubwaaa!! Na sekunde chache nilimuona Shangazi karejea kwenye siti yake huku akiniangalia kwa hasiraaa……

ITAENDELEA

CHANZO : BURE SERIES
 
SEHEMU YA NNE

Nilishindwa kuendelea kumuangalia shangazi kwani sura yake ilitisha sana na alipojaribu kuinuka na kunifata alijikuta akiishia nguvu kwani Mzee wa kitanga alinipa kitabu kitakatifu (MSAAFU) nilioukumbatia kifuani mwangu. Nguvu zake za giza hazikuweza kunifikia kwani nilikua nikilindwa na nguvu za Mungu hivyo kutokana na kuishia nguvu, Shangazi alirudi kuketi kwenye siti yake akiwa na uchovu kwani nguvu za Mungu kupitia MSAAFU ulimfanya aishiwe nguvu zote. Wakati tukio lile likitokea Mzee wa kitanga alikua amelala fofofo na abiria wengi pia walikua wameshalala hivyo tukio lile nililishuhudia peke yangu, Nilikumbuka kuna dawa babu alinipa inilinde na nguvu zozote za giza niliichukua dawa ile na kujipaka mikononi na kisha nilimfata shangazi na kumuuliza, “Shangazi naomba uniambie wale watoto umewapeleka wapi? Niambie haraka kabla sijatangaza ukweli wako mbele ya hawa abiria, Semaaa!! Neema na wenzake wapo wapi?” Niliongea kwa hasira na ujasiri wa hali ya juu kwani dawa ile ilinibadilisha na kunifanya niwe na ujasiri wa kuzungumza chochote kile, Shangazi kwa kuwa aliishiwa nguvu hakuwa na msaada wowote na hivyo kuepuka aibu ile alinijibu, “Nenda msitu wa mashetani uliopo CHANIKA utamkuta Neema tena inabidi uwahi maana damu ya Neema imependwa na mizimu yetu na kabla jua kutoka watamfanya sadaka yao” Nilikosa cha kumjibu shangazi Zaidi ya kumwambia, “ Unasema nini!!! Neema anatolewa sadaka? Kwenye msitu wa mashetani uliopo CHANIKA? Sasa nisikilize wewe mwanga mguu wako mguu wangu mpaka huko msitu wa washenzi wenzako,nyanyuka twendeee!!” Dawa ile niliopewa na babu ilinipa nguvu nyingi sana za kupambana na uchawi wowote ule hivyo nilimchukua shangazi na kupotea nae hadi tulipofika msituni pale. Niliona vitu vya ajabu sanaaa, kwani kulikua na vichwa vya watoto vikipikwa kama supu na huku miguu yao ikichomwa kama nyama choma. Mungu wangu!!! Kwa mbali nilimuona mdogo wangu Neema akiwa anapakwa unga mweupe akiwa uchi wa mnyama wakimwandaa kwajili ya kumtoa sadaka, kwa nguvu ya ile dawa niliyojipaka nilikimbia kwa haraka sana mpaka pale alipokua Neema na nilimnyanyua bila wachawi wale kuona ni nani au nini kimemnyakua mtoto yule. Tukiwa njiani kurudi kwenye basi lile tulihisi harufu ya damu za binadamu zilizomwagika muda si mrefu, Kumbe tulipofika msituni pale nikiwa na shangazi, Shangazi aliweza kunitoroka bila mimi kujua na kumfata mkuu wa kikosi kile cha wachawi na kumuelezea ukweli wote na ndipo mkuu yule aliondoka haraka kuelekea kwenye basi lile ambapo alilisababishia ajali na abiria wote akiwemo Mzee wa kitanga walifariki. Tulifika eneo lile la ajali mimi nikiwa sijui lolote lile nilibahatika kumuona mzee wa kitanga akikaribia kukata roho na ndipo aliniambia maneno machache, “Kijana Mungu akulinde, chukua MSAAFU huu uwe kiongozi wako” Mzee yule alikata roho papo hapo. Niliamini ni ajali ya kawaida, hivyo nilimchukua mdogo wangu (Neema) na kuanza nae safari ya kutafuta usafiri wa kurudi kijijini kwetu “Luvile”. Kabla ya kuondoka nilimwambia shangazi, “Naomba sana ukae mbali na maisha yetu tena usijaribu kutufata na nguvu zako za kichawi kwani umeona jinsi gani nguvu za Mungu zinaweza kuzishinda nguvu za giza, na kwa kuwa nakupenda Shangazi yangu naomba uache tabia ya uchawi na umrudie Mungu wako, Kwaheri Shangazi sisi tunarudi kijijini kuendeleza biashara (UVUVI WA SAMAKI) ya marehemu babu yetu”…

Safari ya kurudi kijijini haikuwa ngumu kwani tulipata bahati ya kupanda gari la mizigo lililokua lilikisafirisha mahindi na maharage hadi kijijini kwetu. Safari ile ilichukua muda wa siku tatu mpaka kufika Luvile kwani gari lile lilipatwa na itilafu za kiufundi hivyo tulifika kijijini pale ikiwa ni mishale ya saa 4 usiku nikiwa na Neema aliyekua begani amelala fofofo!!. Niliangalia huku na kule japo nipate sehemu ya kujilaza mimi na mdogo wangu mpaka itakapokuwa ikikaribia asubuhi ndio tuanze safari ya kuelekea nyumbani kwani kwa muda ule na umbali wake nilishindwa kuvumilia kwani nilikua na mdogo wangu begani ambaye uzito wake pia ulichangia mimi kukosa nguvu za kutembea mpaka nyumbani. Kwa bahati nzuri nilibahatika kuona nyasi zilizokua zimetengenezwa kama kiota cha ndege na bila kujiuliza mara mbili nilijitupa kwenye nyasi zile huku mdogo wangu nikimlaza pembeni kidogo na mimi, Usingizi ulinoga sana kwani nyasi zile hazikua zikiwasha wala kuchoma na hivyo sikuweza kuwaza chochote zaidi ya kulala tu, Nilishtuka usingizini kwani kiu cha maji kilikua kimenibana huku Neema nae akishtuka kwajili ya maji, Hivyo nilitoka kwenye kile kiota na kuanza kutembea huku na kule nikitafuta maji ya kunywa ila kabla ya kuondoka nilimfunika mdogo wangu na zile nyasi ili nimlinde na wadudu wakali wasijekumshambulia, Kumbe kiota kile kilikua ni cha nyoka aina ya kobra na hivyo baadhi ya wanakijiji walikua wameshamchoka nyoka yule mwenye sumu kali kwani alishaua watoto zaidi ya watatu ndani ya wiki moja hivyo nilipokua kuwa nikitembea kutafuta maji nilipishana na kundi lile wa wanakijiji wenye hasira za kumuua nyoka yule akiwa kwenye kiota chake, Mimi sikufahamu chochote hivyo niliendelea na kazi yangu ya kutafuta maji ya kunywa nimpelekee Neema niliyemuacha kwenye kiota na yatakayobaki ninywe mimi. Wanakijiji wale walipofika kwenye kiota kile na kuona kitu kikijigusa gusa bila kutoa sauti walihisi moja kwa moja atakua ni yule nyoka, hivyo walimwaga mafuta ya petroli kwenye kiota kile na kisha waliwasha moto, Sikufanikiwa kupata maji hata tone moja hivyo nilianza safari ya kurudi kwenye kile kiota, kwa mbali niliona moshi na moto mkali ukitokea eneo lile lile nililomuacha mdogo wangu, Nilikimbia kama mwehu na nilipofika eneo lile palipokuepo na kile kiota nilichukua nimemuacha Neema sikuamini macho yangu kwani kiota kile kiliteketea chote kwa moto ule mkali wa mafuta ya Petroli……Sikuweza kuendelea kuangalia tukio lile kwani roho iliniuma sana kuona kiota kile alichokuewpo mdogo wangu kikiteketea na moto ule mkali, Hivyo niliondoka eneo lile na kuelekea nyumbani. Maisha bila ya Babu na Neema yalikuwa magumu sana kwangu kwani nilikua mpweke sana, Na kila nilipokua nawakumbuka niliishia kulia bila kupata wa kunifuta machozi yangu.........
Nilipiga moyo konde na nilianza maisha yale mapya nikiwa peke yangu, Muda wa miaka 10 ulipita, Kipindi hicho nikiwa mtu mzima na Mvuvi mwenye uzoefu na umakini wa kiwango cha juu kiasi ambacho wavuvi wenzangu walipenda kufanya kazi na mimi kwani niliipenda sana kazi yangu. Wanakijiji wengi walinipa jina la “JOSHUA NYOTA YA LUVILE” Kwa jinsi nilivyokua nikijitolea kwenye shughuli za kuisaidia na kuendeleza jamii yangu, Nilipewa wadhifa wa kuongoza wavuvi wenzangu huku pia nikiwa kiongozi wa vijana wa kijiji changu. Nilipendwa na wengi kwa jinsi nilivyokua nikiwaongoza wenzangu wa ziwani huku nikiwa mshauri mzuri wa vijana ambapo nilifanikiwa kuwawezesha vijana wengi wa kila jinsia wa kijiji kile kwa kuwapa elimu ya uvuvi ambayo hapo awali ilikua ikitolewa na marehemu babu yangu. Maisha ya Luvile yalibadilika sana kwani nguvu kazi za vijana wenzangu zilishamiri kwa kasi na kufanya kijiji chetu kuwa na chakula cha kutosha huku mazao mengi tulianza kuyalima kwenye ardhi yetu na kuepekua gharama za kununua na kusafirisha chakula kutoka mikoani kuleta kijijini kwetu na badala yake mazao yetu ndio tuliyokua tukiwauzia watu wa mijini. Mali za marehemu babu zilichukuliwa na Shangazi tangu nikiwa mdogo na hivyo sikubahatika kufaidi jasho la babu yangu, ila nilikua nikijisemea moyoni mwangu kwamba, “Ipo siku waliodhurumu mali za marehemu babu yangu, Mungu atawaadhibu kwa mabaya yao”. Siku moja nilipokua njiani kuelekea ziwani ikiwa ni mida ya jioni nilibahatika kuonana na binti mrembo aliyejulikana kwa jina la Bahati, Bahati alikua ni binti mrembo sana aliyekua akiishi nje kidogo ya kijiji chetu na nilikua nikilisikia jina lake mara kwa mara kwa rafiki zangu ila sikuwahi kupata nafasi ya kuonana nae ila leo hii nilibahatika kuonana nae. Kwa sura bado mdogo ila umbile lake alionekana mkubwa kwani alikua ni mrefu mwenye shepu ya kumfanya kila mwanaume amtamani, Nilimsimamisha na tulianza kufahamiana kwa majina na aliposikia mimi ndio Joshua alifurahi sana kwani sifa zangu zilienea kila kona. Mazungumzo yetu hayakua marefu kwani mrembo yule aliniambia ana haraka mno kwani bibi yake ni mgonjwa sana na hakua na pesa ya kununua dawa kwani kwa bahati mbaya alidondosha fedha zile alizopewa na bibi yake, Kwa roho ya huruma niliyojaliwa na Mungu nilizama mfukoni na kumpa kiasi chote cha pesa nilichopanga nikawalipe vibarua wangu. Kawaida ya mapenzi huwa ni hisia za mtu kwa mtu na huwa hakuna sababu nyengine ya msingi Zaidi ya hisia. Hisia zangu zilitokea kumpenda sana bahati japokua ilikua ni siku yangu ya kwanza kuonana nae, Hivyo sikumuacha aende peke yake na badala yake niliongozana nae mpaka duka la madawa na kisha nilibahatika kwenda nae mpaka alipokua akiishi na bibi yake, Nilifurahi sana kwani bibi yule aliponiona tu na kujua jina langu alianza kucheka na hakika sifa zangu nzuri zilimfanya bibi yule kupata nguvu ya kushuka kitandani na kisha tuliongea vizuri mno. Nilipokua naaga kuondoka bibi yule hakuniruhusu mpaka pale alipomuomba Bahati apike haraka mno japo nile chochote kile kama ishara ya kuacha baraka zangu nyumbani pale, Chakula aina ya Roshoroo kipikwacho kwa mchanganyiko wa maziwa na mahindi kililetwa na Bahati jamvini nilipokua nimeketi na bibi yule, Nilifurahi sana kupata muda wa kukaa na bibi yule kwani nilikumbuka nilivyokua na marehemu babu yangu, licha ya yote nilifarijika sana nilipomuona bibi yule akipata nguvu hadi ya kuniimbia nyimbo zao za zamani enzi za ujana wao, Bahati alikua mwenye furaha mno kwani alinishukuru sana kutokana na bibi yake kugoma kula chakula ila kwa uwepo wangu pale alikula vizuri na kunywa dawa zake bila shida yeyote. Niliaga na kuanza safari ya kurudi nyumbani, Nilipokaribia na nyumbani ghafla nilivamiwa na kundi la vijana walionimulika na mwanga mkali wa tochi sikuweza kuwatambua kwa haraka na hivyo walinifunga mikono na miguu yangu kwa kutumia Kamba na kisha walinigonga kichwani kwa kitu kilichokua kama chuma na hivyo nilipoteza fahamu zangu.

ITAENDELEA

CHANZO : BURE SERIES
 
SEHEMU YA TANO ........MWISHO


Nilipokuja kushtuka na kurejesha fahamu zangu nilihisi upepo mkali sana huku mawimbi yakipiga mahala pale nilipokua, kwakua ilikua ni usiku mno sikuweza kujua nilipo ila baada ya kuhisi maji yakinilowesha miguuni nilishtuka sana na nilijikuta nikiwa ziwani peke yangu kwenye mtumbwi ambao ulishaanza kujaa maji. Mikono na miguu yangu ikiwa imefungwa na kamba ngumu, nilihangaika sana lakini sikuweza kujifungua kamba zile. Mtumbwi ulijaa maji na bila hata kupoteza muda mtumbwi ule ulianza kuzama………

Juhudi za kujifungua zile kamba nilizokua nimefungwa mkononi hazikufanikiwa na mtumbwi ule ulizima nikiwa chini ya maji pumzi iliniishia baada ya kunywa maji mengi, nilihisi nina sekunde chache mno kufika mwisho wa maisha yangu, Nilihema kwa tabu sana na baada ya sekunde chache nilipoteza nguvu zangu zote huku pumzi ikielekea ukingoni. Kwa chini kabisa niliona kipande cha chuma nilijitahidi kwa nguvu zangu zote huku moyoni nikisema, “Eeeh Mungu wangu naomba unijalie nguvu na pumzi japo kwa dakika chache niweze kujiokoa, nikishindwa basi nitaomba unichukue” Sikujua nguvu na pumzi zilitoka wapi papo hapo nilijikuta nikipata nguvu ya kukifata kile kipande cha chuma kilichokua chini kabisa ya ziwa lile, Nilifanikiwa kukifikia na niliweza kujifungua kamba za miguuni kwanza na kisha kamba za mikono. Mungu ni Mungu tu! kwani sikutegemea kama ningeweza kujiokoa ila kwa mapenzi yake niliweza. Niliogelea mpaka kufika ngambo ya ziwa lile, Watu wengi walinishangaa sana kwani nilikua uchi wa mnyama huku nikiwa nimeishiwa nguvu kabisa. Kwa msaada wa wavuvi wenzangu walionitoa ziwani pale mpaka hospitali kupata matibabu kwani nilikohoa damu huku nikitapika maji kila baada ya dakika, Daktari alinipa dawa na maelekezo ya vyakula vya moto huku niliambiwa nisiende ziwani kwa muda wa wiki tatu kwani hali yangu haikuniruhusu kufanya hivyo. Wiki ya kwanza ilipita salama na ilipofika wiki ya pili hali yangu ilianza kubadilika kwani nilianza kukohoa damu kila dakika, Wanakijiji wenzangu walianza kunitenga kwani habari zilizozagaa zilikua mimi ni muathirika wa virusi vya ukimwi kwa jinsi nilivyoanza kukonda huku nikitoka mabaka baka ya rangi ya kijani mwilini wangu. Kilichonisikitisha zaidi ni pale niliposikia Bahati karibuni angechumbiwa na kuwa mke wa mtu, Maisha yangu yalibadilika sana kwani nilikua ni mgonjwa nisiyekua na mtu wa kuniangalia na kuniuguza, Heshima yangu yote ilipotea huku uongozi niliyokua nao kwenye nyanza mbali mbali za kijiji kile zikichukuliwa na watu wengine kwani kila mwana kijiji alijua mimi sitopona tena na huku wakiniambia, “Joshua wewe sidhani kama utafika mwakani, Wewe ni wa kufa tu” maneno hayo yalikua yakiambatana na vicheko vya kejeli…Hakuna kitu kibaya kwenye maisha ya binadamu kama kutengwa na jamii yako, Afya yangu ilizidi kuwa mbaya mno kandri siku zilivyozidi kwenda mbele kwani sikua na mtu wa kunisaidia kupika wala kunisimamia ninywe dawa kwa muda sahihi. Siku moja nikiwa kitandani mida ya usiku nilikumbuka sana maneno ya marehemu babu kwani alikua akinisisitizia kuwa, “Joshua mjukuu wangu wewe ni jasiri kwani ulizaliwa kwenye mazingira magumu sana ambayo isingekua ujasiri wako usingefanikiwa kufika hapo ulipo, hivyo naomba ulitambue hilo” Palipokucha nilijitahidi kuamka na kisha kuanza safari ya kuelekea ziwani kutafuta chakula kwani sikua na chakula kabisa, Nilipokua njiani nilikutana na Bahati ambaye sikutegemea angenikimbia bila hata kuitikia salamu yangu. Niliumia sana kwani kitendo kile kilinifanya niishiwe nguvu ya kuendelea na safari yangu ya ziwani, nilipiga magoti na kisha kuziangalia mbingu huku nikitamka kwa sauti ya nguvu, “Baba Mungu mwanao napitia yote haya sina wakunipenda tena hapa duniani, Ewe Mwenyezi naomba unijalie afya njema” Nilipomaliza kuongea maneno yale machozi yalianza kunitoka na ghafla niliona mkono wa mwanamke ukinishika begani huku sauti ikiniambia, “Joshua usilie mwanangu nimekuja kukusaidia” Nilipomtazama mtu huyo sikuamini macho yangu kwani alikua Shangazi yangu. Shangazi aliniinua pale nilipokua nimeketi kwa huruma na kisha alinikumbatia huku akiniambia, “Joshua pole sana mwanangu, Niliota ndoto mbaya sana kuhusu wewe na kwa kuwa nilifata ushauri wako nimrudie Mungu wangu niache ushirikina naamini Mungu aliniotesha ndoto ile ili nije nikusaidie, Punguza kulia nimekuja kukusaidia, Nyanyuka twende nyumbani”. Tulipofika nyumbani Shangazi aliingia jikoni na kunipikia ndizi na samaki, Nilikula na kisha nilimeza dawa na kisha tulianza kuzungumza, Nilimwambia Shangazi, “Shangazi nashukuru sana kwa upendo wako pia nashukuru kwa kufata ushauri wangu, Naamini Mungu ameshakusamehe makosa yako yote” Shangazi alinijibu, “Joshua, Marehemu baba yako alikua mtu mwema sana na alipenda sana kumsaidia kila mtu bila kujali ni tajiri au maskini, Naona umerithi tabia zake, Joshua nitakuangalia mpaka upone kabisaa na kama utahitaji twende wote mjini basi sina shida na hilo, Sawa mwanangu kipenzi?” Nilimjibu kwa furaha, “Ndio Shangazi yangu kipenzi”…

Shangazi aliniangalia vizuri sana kiasi ambacho madonda yote ya mwilini yalianza kupotea huku hali yangu ya kukohoa damu ikitoweka kabisaaa!! Majirani wenye roho mbaya na chuki rohoni mwao hawakusita kuja nyumbani na misalaba huku wengine wakiwa na sanda bila kusahau rafiki zangu waliokuja na jeneza kwajili ya kunizika, Hali ile iliendelea kila siku lakini Shangazi yangu hakuchoka kuwafukuza na kunipa moyo kuwa yote hii ni mitihani ya maisha na ili kuyashinda ilibidi niwe jasiri. Baada ya Muda wa wiki 3 kupita nilitoka nje na kujiangalia kivuli changu sikuamini kwani afya yangu nzuri ilirudi huku madonda na mabaka baka ya kijani yakitoweka kabisaa! Nilirudi ndani na kumwambia Shangazi ," Shangazi yangu nakushukuru sana haya yote unayonifanyia ipo siku Mungu atakulipa, nakupenda sana shangazi" Shangazi alinijibu huku akitabasamu, "Joshua mimi ndio mzazi wako niliyebaki hivyo ni jukumu langu kuhakikisha upati tatizo lolote lile, Sawa baba?" Nilimuitikia Shangazi kisha nilitoka nje kuelekea ziwani kuangalia hali halisi ya uvivu inavyoendelea. Nilifika ziwani nikiwa nimevaa nguo za kujizuia na baridi ambazo zilinifanya kutojulikana na mtu yeyote yule kwani nilivaa mzula (boshori) uliofunika kichwa changu. Niliona fujo na maneno makali ambayo wananchi walikua wakilalamika Uongozi mpya wa ziwa lile ulijawa na ufisadi, niliposogea karibu na umati ule wa wavuvi na wauza samaki nilisikia kundi la vijana likisema, "Daah..! Yani bora ya Joshua naamini angeendelea kuwa kiongozi leo hii tusingekua na malalimiko ya kijinga jinga" Mara baada ya kijana mmoja wao wa kundi lile kumaliza kuongea maneno yale kundi lile kwa pamoja lilianza kuimba kwa sauti za hasira, " Tunamtaka Joshua, Tunamtaka Joshua, Tunamtaka Joshua, Tumechoshwa na ufisadi" Wimbo ule ulipokelewa na kila mtu aliyekuepo eneo lile. Nilitamani sana nionyeshe uso wangu ila roho yangu ilisita kwani usalama wangu ungekua hatarini, Hivyo niliondoka eneo lile na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Nilipokua nakaribia nyumbani nilikutana na yule bibi aliyekua akiishi na Bahati ambaye aliniomba tuketi na alinelezea historia ya Bahati, Mungu wangu!!! Sikuamini nilichoambiwa kumbe Bahati ni mdogo wangu Neema…

Simulizi ya bibi kuhusu historia ya Bahati ilikua hivi, “Joshua wewe ni kijana shupavu na mwarevu sana pia ninaelewa ni jinsi gani umetokea kumpenda Bahati lakini Bahati si mjukuu wangu wa damu moja, Siku moja miaka 15 iliyopita nikiwa kando ya ziwa nilimuona mtoto mmoja wa kiume akiwa na mdogo wake wa kike aliyekua amembeba begani na walihaha huku na kule kutafuta mahali pa kulala na ndipo mtoto yule wa kiume aliona kiota alichoshindwa kutambua ni cha mnyama gani na kujilaza yeye pamoja na mdogo wake, Mimi nilipoona amelala kwenye kile kiota ambacho wanakijiji wa hapa walikua wakimuwinda nyoka aliyetokea kuwa tishio sana kwa miaka ile na makazi yake yalikua kwenye kile kiota nilijificha pembeni ya mti mkubwa na kuwalinda watoto wale. Baada ya masaa kadhaa kusogea mbele nilimuona mtoto yule wa kiume akitoka na kuelekea barabarani niliposhindwa kutambua alikua akifata nini, Alimuacha mdogo wake kwenye kile kiota kwa mbali nilisikia sauti za wanakijiji zikiwa zinakaribia eneo lile na kutokana nilikua na sungura wangu ilinibidi nimfunge mdomo, miguu na mikono ili asijetoroka wala kupiga kelele kwani kuna mwanakijiji mmoja alikua ameshafika eneo lile la kile kiota na kuona kitu kikiwa kimejifunika kwenye manyasi huku kikijigusa gusa na ndipo aliondoka kuwaita wenzake waje kumteketeza nyoka yule bila kutambua alikua ni mtoto. Hivyo nilielekea kwenye kile kiota na kumtoa mtoto yule na kisha kumfunika Sungura wangu kwenye zile nyasi na wanakijiji walipofika na kukuta bado kuna kitu kinajigusa gusa waliwasha moto na kujua kuwa wamefanikiwa kumuua nyoka yule, kumbe walimchoma Sungura wangu. Hivyo Joshua Bahati si mjukuu wangu wa damu ila yeye hatambui ilo kabisaa!!” Nilivuta pumzi kwa nguvu huku macho yakinitoka kwani historia ile ilionyesha kuwa Bahati ni mdogo wangu Neema, Nilijikaza nisilie wala nisiongee chochote cha kumfanya bibi yule kujua ukweli kwamba mimi ndio kaka wa Bahati (Neema). Nilinyanyuka na kumwambia bibi, “Dah.. pole sana bibi, ila pia Mungu akubariki kwa kuweza kuokoa maisha ya Bahati” Tuliagana na niliendelea na safari yangu ya kuelekea nyumbani. Nilipofika nyumbani nilimkuta Shangazi akiwa ameketi chini kwenye jamvi na nilianza kumsimulia kila nilichoambiwa na yule bibi, Shangazi aliniambia, “Joshua unasemaaa..!!?”.

Muda wa wiki tatu ulipita na nilimuaga Shangazi kuwa naelekea mjini kumtafuta mdogo wangu, Nilitupilia mbali nafasi ya kurudi kwenye uongozi wa ziwani huku vijana wenzangu wakiandamana kuniomba nirudi kuongoza umoja wa wavuvi wa kisiwa kile ila yote yale hayakua na nguvu yeyote ya kunizuia nisiende mjini kumtafuta mdogo wangu (Neema). Nilianza safari ya kuelekea mjini Mazimbwe ambapo nilibahatika kufika majira ya usiku Sanaa, kutokana nilikua na kiasi cha fedha kilichoweza kunifanya nilipie chumba kwenye nyumba ya kulala wageni sikuwa na shida ya kutafuta pa kulala. Nyumba ile ya kulala wageni ilikua ni ya kizamani zamani hivyo huduma ya kujisaidia na kuoga ilikua ikipatikana kwenye vyoo vilivyokua nje ya vyumba, Nilishtuka saa 8 usiku baada ya jasho kali kunimiminika na hivyo niliamua niende bafuni japo nijimwagie maji nitoe jasho lile. Kwa bahati mbaya niliingia bafuni bila kubisha hodi na hivyo nilimkuta binti mmoja akiwa mtupu na kwa kuwa aliniona alishtuka na kuniambia, “Usiondoke na wala usiogope” Mhhh!!!!? Niliguna moyoni mwangu kwani binti yule alikua na rangi nzuri ya kuvutia huku sehemu ya nyuma ya mwili wake alionekana kama kafungasha virushi vya maembe La hasha!!! Mtoto alikua ameumbika walaaahi!! Dooh!!!. Aliniambia, “Sogea karibu basi mbona unaniogopa?? Kifua chako kimenisisimua sanaaa” niliogopa sana na nilimuuliza, “Samahani dada wewe ni nani? Na kwanini upo kwenye hii nyumba?” Yule binti alinijibu, “Mimi naitwa Nasra na hapa nipo na bwana wangu ila nimechoka kukaa nae ndani kwani hawezi kitu kabisa yani huwezi amini tuna masaa matatu chumbani mtarimbo wake umegoma kusimama na nina hamu ya kufanya mapenzi, naomba unisaidie japo mshindo mmoja tu nikalale vizuri maana kwa hali hii sitoweza kulala” Nilitazama mwili wake ule wenye umbo nambari 8 nilishindwa kukataa kwani mimi pia nilikua nina hamu sana, Hivyo tulisogeleana na nilifanikiwa kula tunda lake kwa ufundi zaidi kiasi kilichomfanya akalale na mimi chumbani kwangu na kumuacha bwana wake chumbani peke yake akiwa amelala akikoroma kama chura wa mtoni. Yote yali yalinifanya nisahau kilichonileta mjini na hivyo asubuhi ilifika Nasra aliniamsha na kuniomba nimpatie huduma ya asubuhi kwani hatopata tena akirudi kwa bwana wake na kwa vile mtoto yule alitaka name sikua na jinsi nilimpatia, Ila sasa wakati tunafanya mapenzi mlango wa chumbani kwangu nilisahau kuufunga na hivyo ulifungulia na tulikurupuka kuangalia ni nani anaingia.Tulibaki tukitoa macho kwani tulishindwa kuelewa kundi lile la polisi lililoingia chumbani bila hata kubisha hodi wala kusalimia, Polisi wale walianza kukagua mizigo yangu na kisha walikagua mkoba wa Nasra na kukuta akiwa na dawa za kulevya zikiwemo Bangi pamoja na Mirungi kwenye ule mkoba. Polisi hawakutaka maongezi na mtu yeyote walituchukua na kutupeleka kituo kikubwa cha polisi ambacho kilikua karibu na nyumba ile ya kulala wageni, Nilipokua kwenye gari ya polisi nikiwa natafakari mikosi yote hii niliyojitafutia kwa mbali kidogo nilimuona Bahati (Neema) akiwa anapakia mizigo kwenye gari ndogo ambayo ilionekana kuwa ya kwake huku tumbo lake likiwa limenona na bila fikra zangu kukosea Neema alikua mjamzito wa miezi 5. Nilimuita kwa nguvu zote, “Bahati Bahati Bahatiiii” kwa kuwa alikua anaongea na simu hakuweza kunisikia kabisa, Niliumia sana kwani nilikuja mjini kumtafuta yeye ila tamaa na roho za shetani zilinifanya nijiingize kwenye matatizo yote haya. Tulifikishwa kituoni na kila mtu alihojia maswali kwa muda tofauti, nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuwaelezea polisi ukweli bila kuwaficha chochote, Kamanda mkuu wa kituo kile alinielewa na aliniruhusu niondoke kwani mizigo yangu haikuwa na tatizo lolote. Niliondoka kituoni pale na kuanza kutanga tanga huku na kule nikiwauliza watu kama wanamfahamu Bahati japo kwa kuwaelezea jinsi alivyo, Siku tatu zilipita sikufanikiwa fedha zikiwa zimeniishia sikuwa na pa kula wala kulala, Siku iliyofata niliamua niende kituo cha polisi na kuwaomba wanitangaze kuwa nimepotea na nilikuja mjini kwa rafiki yangu Bahati, Polisi wale waliniomba pesa kidogo na kwa kuwa sikua nayo walishindwa kunisaidia, hivyo niliendelea kuzunguka bila kuwa na matumaini yoyote yale. Kadri siku zilivyozidi kusogea nilijikuta nikipoteza nguvu huku mwili wangu ukidhoofika kwa kukosa chakula lakini yote yale nilijisemea moyoni, “Sirudi Luvile bila mdogo wangu acha nife na njaa”. Kwa bahati nzuri siku moja nikiwa maeneo ya sokoni nilibahatika kumuona Bahati (Neema) akiwa ananunua bidhaa za nyumbani nilimkimbilia kwa furaha na kwa kuwa alikua amebeba mizigo mizito nilimpokonya mizigo ile bila hata kunijua vizuri, Bahati alikasirika sana kwani hakuweza kunitambua kwa urahisi kama nilivyodhani na hivyo alipiga kelele za mwizi, “Mwiiiziiii jamani mwiziiiiiii” kwakuwa nilikua mgeni maeneo yale watu walishindwa kunitambua na hivyo walinishambulia kwa mawe huku wengine walinipiga na mbao zilizokua na misumari mikubwa, Maskini!!! Nilijeruhiwa vibaya mno lakini kwani sehemu yangu ya kichwa ilipigwa sana na mawe na kutokana nilipoteza damu nyingi huku ubongo wangu ukichanganyika na damu sikuweza kuendelea kupumua, JOSHUA ALIFARIKI DUNIA. Bahati alipofika nyumbani alimsimulia mchumba wake kilichomtokea sokoni na alipokua akitoa mizigo yake kwenye mifuko aliiona PETE iliyokua na kidani cha rangi ya bluu iliyomkumbusha JOSHUA kwani pete ile alikua nayo Joshua na alipenda sana kuishika pale alipokua akionana na Joshua, Bahati alishtuka sana kwani alianza kurudisha fikra zake nyuma na kukumbuka tukio lile la yule kijana aliyemuitia mwizi na kwa msaada wa ile pete iliyodondokea kwenye moja ya mifuko ile wakati JOSHUA alipokua akimpokonya mizigo yake kwa nia ya kumsaidia. Bahati alimuomba Raheem (Mchumba wake) ampeleke sokoni kumuangalia yule mwizi kwani alihisi amefanya makosa kumuita mwizi, Walipofika walikuta mabaki ya majivu kwani JOSHUA alichomwa moto, Bahati alilia sanaaaa!! Kwani alisabibisha kifo cha Joshua bila yeye kutambua. Taarifa za kifo cha Joshua zilifika kijijini Luvile na kufanya kijiji kile kuwa na upweke wa hali ya juu huku vilio na maombolezo yaliochukua muda wa mwezi mzima kumuhenzi kwa sala na nyimbo za huruma na majonzi kwani hawakubahitika kuuona mwili wa Joshua kumbuka alichomwa moto. Shangazi wa Joshua alibahatika kuonana na Bahati na alimuuleza ukweli wote juu ya yeye kuokotwa na maisha yake yote mpaka pale alipofikia, Ukweli ule ulimfanya Bahati azidi kuumia na kumfanya mwenye majonzi kila kukicha.

Bahati ndiye Neema mtoto aliyetupwa njiani mara tu alipozaliwa na Joshua alimuokota na kumlea mpaka pale walipokuja kutengana, Juhudi za Joshua kwenda kumtafuta mdogo wake aliyekua amepotezana nae kwa muda mrefu zinamfanya apoteze maisha. Bahati (Neema) alijifungua mtoto wa kiume salama na alimpatia jina la JOSHUA. Wavuvi wa ziwa la Luvile walitumia gharama nyingi sana kuchonga sanamu ya Joshua huku wakibadili jina la ziwa lile ambalo hapo awali lilikua likijulikana kwa jina la FAHARI YA LUVILE na Kuliita SHUJAA WA LUVILE jina hilo liliambatana na ile sanamu kubwa ya Joshua.

MWISHO WA HADITHI.

UMEJIFUNZA NINI KWENYE HADITHI HII... NAOMBA MAONI YENU.

CHANZO : BURE SERIES
 
Ahsante......
Story unazoleta ni fupi, unazimaliza kwa wakati na zina mafundisho, hongera sana
 
Mwili ulinisisimka sana...stori nzuri mno imenifundisha kutokana na mafunzo yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom