SEHEMU 3
Gaston; Kwa nini umeamua tukae hapa ili hali kigiza kimeshaingia na sehemu hii hamna taa?
Alice; Hapana sehemu hii nimepapenda tu siunajua room (hostel) sa hivi kila mtu yupo alafu kwa wewe mtoto wa kiume sio vizuri kuingia chumba cha watoto wa kike tupu usiku huu.
Gston; Ni kweli, lakini mimi nilikwambia uje gheto kwangu.
Alice; No, leo sijisikii kutoka nitakuja siku ingine, ebu nambie ulitaka kuniambia nini?
Gaston; Kwa mazingira haya siwezi kukuambia kitu, ila kwa kuwa huwezi kutoka nitakwambia hiyo siku ingine ukiweza kutoka nje ya chuo.
Alice; Sawa haina shida, tutatoka wikiendi uniambie.
Hayo ni baadhi ya mazungumzo mafupi baina ya Alice na Gaston mtu na shemeji yake wakiwa juu ya kimbweta cha chuo.kwa wale wasiojua kimbweta ni viti vilivyotengenezwa kwa sumenti kwa ajili ya kujisomea na vinapatikana nje ya madarasa mara nyingi huwa vipo vyuoni na vina majina mbalimbali kulingana na chuo husika.
Wakati wakiendelea na stori za hapa na pale kwenye sehemu hiyo yenye kigiza na mbu wasumbufu mara kuna watu wawili walikuja tena wa jinsia mbili tofauti hapa namaanisha wa kike na wa kiume. Gaston akamwambia shemeji yake ebu tujifiche tuone sinema maana kila siku nasimuliwaga eti kuna wanachuo waliochizika wanakuja huku kufanya mapenzi. Wale watu wawili wa kike na kiume wakaenda kwenye Vimbweta vilivyojificha zaidi na kutulia hapo. Walikuwa wanaongea kwa sauti ya chini sana hali ambayo iliwafanya Alice na Gaston wasogee zaidi kujua nini kinaendelea.
Kwa mbali walisikia wale watu wakibishana kuhusu bei,
Wa kike; Tatizo lenu nyie wanafunzi wa secondary mnataka vitu vizuri wakati hamna hela. Mtu huwezi kulipia hata hela ya guest bado mnanisumbua hamuoni kuwa mnazalilisha kazi yangu?