Asaelofficial
Member
- Sep 5, 2017
- 30
- 35
[9/16, 11:27]
: NICE GUY OF CENTURY
SEHEMU YA 01
Ni katika supermarket moja alionekana Baba akiwa mke wake pamoja na mtoto wao mdogo wa mwisho katika uzao wao,mke alikuwa alilalamika kuwa hela hawana halafu mmewe amemleta sehemu ya gharama supermarket kununua keki ya birthday ya mtoto wao mkubwa wa kiume Asael,mtoto ambaye hana hata kazi tangu amalize masomo yake hakuwa ameajiriwa mpaka muda huo bado tegemezi nyumbani,
Baba alichukulia busara hakutaka kubishana na mke wake alimwambia...
"Mke wangu huyu ni mtoto wetu hata kama kwa sasa hana kazi ni tegemezi kwetu itafika tu wakati naye atapata kazi,na kuhusu kutumia pesa hata iliyobaki ya matumizi yetu nyumbani kumnunulia keki ya gharama mtoto wetu ambaye hana hata msaada kwetu kwa sasa sioni kama ni tatizo huyo ni mwanawetu hivyo ikiwa leo ni siku ya kuzaliwa kwake acha tutumie hata kidogo tulichonacho kuhakikisha mtoto wetu anapata furaha,ikiwa sisi tupo hai ni jukumu letu hili"
Hayo yalikuwa maneno ya mzee baada ya mkewe kulalamika kuhusu kijana wake kukosa kazi ya msingi tangu amalize masomo yake kutokana na tatizo la ajira kwa sasa.
Mkewe alimuangalia mmewe kisha akasema...
"nilijua tu utamtetea tu kijana wako,haya nunua hiyo keki twende"
aliongea mkewe,
mzee akajua huyu tayari nimeshamshinda ujanja,hayo yalikuwa ni maneno ya hapa na pale ya familia wakati wakiwa katika supermarket...
mara mtoto akaona mkate akamunyoshea mkono baba ake amnunulie...
Baba akawa anataka kumnunulia mtoto wake kwa siri ili mkewe asijue maana alijua tu lazima mkewe angemsema tena kuwa kawadekeza watoto wake....
Mzee alikuwa na tabia ya kutokukubali mtoto wake apate shida au ateseke ikiwa yeye anauwezo wa kumsaidia...
Walifika nyumbani walianza maandalizi ya kuandaa siku ya kuzaliwa ya kijana wao mpendwa walipanga kumfanyia surprise/mshitukizo hawakumpa taarifa,yeye mwenyewe haikuwa rahisi hata kuikumbuka hata siku yake ya kuzaliwa maana muda mwingi alikuwa akiutumia kufanya kazi ndogondogo mtaani akisubiri ajira kiufupi maisha hayakuwa sawa kabisa yalikuwa ya dhiki mtindo mmoja...
Wakati wao wakiandaa surprise aliyekuwa akiandaliwa hiyo surprise ndio kwanza wakati huo alikuwa akikabidhi guta alilokuwa akitumia kujiingizia kipato kwa boss wake,alikabidhi akapewa ujira wake kutokana na kazi aliyoifanya kwa siku hiyo,maana alikuwa akilipwa kwa kutwa,sasa alishangaa siku hiyo kulipwa nusu ya mapato yake alipohoji akaambiwa nusu ingine ilikuwa ibaki ili kukarabati guta alilokuwa akitumia,
Hakuwa na jinsi ilibidi tu akubaliane na matokeo alinishauri boss wake akaondoka....
Taratibu alikuwa akitembea kurejea nyumbani moyoni alijiuliza mateso na unyanyasaji huo uliokuwa ukimkumba ungeisha lini kazi ngumu mshahara mdogo,mtaani anadhaurika kuwa kasoma bure kaishia kuuza maji hakika hizo ndio zilikuwa changamoto kubwa kwake...
Aliingiza mkono mfukoni akatoa simu yake,alipotazama saa ilikuwa saa mbili usiku kama na dakika tano hivi alijiona amechelewa aliongeza mwendo akaendelea kukatiza katika vichochoro....
Nyumbani maandalizi yalikuwa tayari familia ilikuwa na furaha tele licha ya hali ya uchumi kutokuwa nzuri tangu Baba mwenye nyumba afukuzwe kazi katika kampuni alikuwa akifanya kazi kutokana na kuongoza wafanyakazi katika kudai haki zao kampuni lilichukua uamuzi wa kumfuta kazi na kumpa haki zake zote ili kuepusha asisambaze sumu iliyokuwa katika moyo wake ya kutetea wafanyakazi wenzake ili wapate haki zao za msingi hivyo alijikuta alifukuzwa kazi akarudi katika kazi yake ya kilimo cha mbogamboga za majani mpaka wakati huu....
Mama alianza kupata hofu akasema mbona kijana wake hakuwa na tabia ya kuchelewa nyumbani hivyo labda huko alipo alikumbwa na matatizo,
Mme akamsihi asiwe na hofu kijana wao angefika tu muda sio mrefu hivyo waendelee tu kumsubiri....
Upande wa pili ni kweli kijana wao Asael hakuwa kabisa na kumbukumbu kuhusu siku yake ya kuzaliwa,aliendelea kutembea ili awahi nyumbani....
Sasa wakati akiwa anatembea katika jengo moja alisikia kama kuna watu walikuwa wakiongea na vishindo vya hapa na pale ilimuwia vigumu kupita hilo eneo tena la mtaani kwake asijue nini hasa kiliendelea wakati huo,,,
Taratibu alijisogeza katika jengo hilo,aliamini wazi alikuwa sahihi kwa alichokusudia kuchunguza wakati huo kwa yeye alisomea masuala ya uwandishi wa habari sasa alitaka kujigeuza naye kama mwandishi halisi wa habari aliyekuwa akipeleleza habari kwa kina!
Rahasha kumbe haikuwa hivyo yeye akitokea katika kazi za guta hakuwa ameajiriwa kwa wakati huo licha ya kuwa kweli alikuwa na ujuzi huo...
Taratibu kabisa alipata upenyo akapenyeza jicho lake la kushoto bado ilionekana hajaridhika,alizidi kupepesa macho kwa harakaharaka aligundua kulikuwepo na makundi mawili ya watu ambayo yalisimamiana wima,alipotazama kwa umakini zaidi kiongozi mmoja wa kundi alimtambua,alikuwa ni Mr chalima mfanyabiashara mkubwa kabisa wa madini aliyejulikana sana hakuelewa kwa harakaharaka nini walikuwa wakikifanya usiku ule...
Baada ya muda gari iliingia mpaka eneo hilo gari ilikuwa imefunikwa turubai juu,Taratibu Mr chalima alisogea katika gari hilo akatoa amri vijana wafungue aone kilichokuwa ndani vijana walifanya hivyo...
Zilikuwa ni pembe za Ndovu aise!!!
Moyo wa Asael ulijawa na hofu sana kwa muda huo,hakuwahi kufikiria kuwa mtu kama mr chalima alikuwa akisifika kwa kutoa misaada katika jamii angesubutu kufanya biashara ya hatari kiasi kile tena wakishirikiana na maafisa wa polisi!!
mr chalima kwa wakati huo alikuwa na furaha sana hakuwa na wasiwasi kwa alitendalo...
ni wazi alikuwa ni mwenyeji na biashara hiyo,
Taratibu mwili ulimsisimka Asael akaitoa simu yake mfukoni aliona ni bora angebaki na ushahidi yeye kama mwandishi wa habari...
Alirekodi tukio hilo kwa simu yake ya mkono wakati mr chalima akikabidhi pesa kwa maafisa wale wa jeshi la polisi...
akajiona mshindi hakuta kuishia hapo alitaka apige na picha!!!
Nyumbani Bado alikuwa akisubiliwa
na familia yake ili waje kusherehekea siku yake ya kuzaliwa
mdogo wao wa mwisho alianza kulilia ile keki mama akaamua kumkatia kidogo..
Huku Asael akafanikiwa kupiga picha mbili za mwanzo,ila tayari alishaonekana mwanga wa simu ulimponza!!!
Akashangaa anaguswa kwa nyuma,akageuka mapema sana akafanikiwa kumtoroka huyo mtu ila aligundua ameshafamika alilaumu kimbelembele chake alijiona tayari ameiongoza familia yake matatani kwa muda wowote yule mtu angeweza kufika nyumbani....
akazunguka upande mwingine kusikia nini kingejili baada ya yeye kuonekana....
Alisikia kabisa mr chalima akitoa amri kwa kujiamini kabisa....
"kama amesikia haina budi sisi kumfunga mdomo asiongee mpaka mwisho,
na njia sahihi zaidi ya yeye kutunza siri ni kufa tu kabla hajafika nyumbani aeleze hili akiwatangulia kufika basi mmalize familia nzima siri izidi kuwa siri"
hii sauti Asael Alijisikia waziwazi kabisa kifo chake na cha familia yake kikipangwa na mr chalima....
Moyoni aliona ni bora awahi nyumbani akaiondoe familia yake mapema kabla wauaji hawajafika....
Wazazi wakiwa wamezubaa zubaa ghafla mwanao alifika akiwa na hofu iliyopitiliza
"baba,mama yatupasa tuondoke eneo hili mara moja wauaji wanakuja muda sio mrefu sitaki mniulize maswali kwa sasa nitawaeleza mbele ya safari"
Aliongea huku jasho likimtoka kama alitokea katika riadha marathon...
fataki zilianza kufyatuka picha yake mbele ndipo akakumbuka ilikuwa siku yake ya kuzaliwa!!
Alijilaumu sana kuwa na kiherehere...
walitoka akawasindikiza yeye akawahaidi kukutana mbele amalizie kuchukua vitu ndani....
Wakati tu anarudi kabla hajafika alishuhudia wauaji wakiingia ndani katika nyumba walipoishi wao....
Huu ni utangulizi tu wa mkasa huu...
[9/16, 11:35]
: SEHEMU YA 02
...ilipofika
Baada ya kijana mdogo Asael kuingilia mambo ya wakubwa kwa kujitia mwandishi wa habari na kuamua kupiga picha biashara za watu,anajikuta katika wakati mgumu hata familia yake kuitia matatani
Sasa endelea....
Baada ya wale wauaji kuingia ndani na kukosa mtu walijua moja kwa moja walizidiwa akili,walijilaumu kuchelewa kufika hapo,
wakapiga simu kwa mr chalima kumjulisha habari hizo...
Baada tu ya watu hao kuondoka katika nyumba ya akina Asael,kwa umakini mkubwa Asael akaingia ndani naye akapita mpaka katika chumba alichokuwa akilala akainama katika uvungu wa kitanda akatoa kisanduku kidogo,akaamua kukivunja,kilikuwa ni kibubu chake alichokuwa akihifadhi pesa,baada ya kukipasua akazitia zile pesa mfukoni kwa upesi upesi akatoka....
Sasa familia yake baba,mama na wadogo zake wawili wakiume na wakike walifanikiwa kufikia kwa ndugu,baba mdogo wa Asael/mdogo wake na baba wa Asael(Mr kiwila).
Cha ajabu Ndugu akakataa hata kuwaruhusu kulala akidai hawezi kukaribisha matatizo kwake,wakabaki nje wasijue hatima yao ni nini usiku ule hakika usemi wa ndugu ni ndugu wakati wa raha tu au unapokuwa umefanikiwa tu na kuja kuomba misaada ukiwa na shida unapambana na hali yako ukiwa peke yako ama na familia yako...
Waliendelea kukaa hapo kwa muda baadae mtoto wao,
Asael akafika naye,alijisikia mkosaji kila alipowaangalia wazazi wake katika hali ile wakati muda mchache tu uliopita familia ilikuwa katika furaha tele chanzo cha matatizo yote alikuwa yeye....
Hawakuwa na jinsi waliingia jikoni hapohapo kwa ndugu yao,Asael aliwaomba radhi wazazi wake kwa kilichokuwa kimetokea,mwisho aliamua kuwaeleza nini kilitokea mpaka wao wakafikia katika hali ile...
Mr chalima akiwa amelala na mke wake nyumbani usingizi haukuwa karibu kwake kwani alikuwa anahisi usalama wake ulikuwa mdogo tayari ushahidi kuhusu biashara zake haramu sasa ulikuwa mikononi mwa mtu fulani!!
Mkewe alimuuliza kuhusu hilo ila hakuweza kumuweka wazi alisema hakuwa na usingizi tu...
Hakutaka kuzungusha kichwa sana kwa mara zote alikuwa akiamini hakuna linaloshindikana mbele ya pesa,sheria aliishikilia mkononi kila alilotatizwa alimwaga pesa na kulifukia bila shida...
iweje leo kijana mdogo mwenye kiherehere tu eti amnyime usingizi??
kakijana tu ambacho hakajafunzwa vyema nyumbani kanaingilia vitu vya wakubwa,Mr chalima alimbeza Kijana mdogo Asael aliyejitia kimbelembele mbele ya biashara zake...
Alijiuliza Ni mara ngapi nimekuwa nikipambana na wanasheria waliosomea na wanaujuzi nawashinda??
Hizo ni rekodi zake alikuwa akizikumbuka....
Alipiga simu katika kituo cha polisi na kuwataarifu familia ya mr kiwira iangaliwe kwa umakini popote itakapoonekana ajulishwe...
mpaka hapo aliamini ameua mchezo.
Asael baada ya kueleza kilichotokea ,walimshauri tu asiumie sana kuwa amewaingiza matatani yote hiyo ni mipango ya mungu tu,
aliwambia wajiandae kusafiri kesho tayari alishaanda usafiri watoke kabisa katika mji wa Arusha waende Morogoro wakaishi huko, aliwambia asingependa aendelee kuitia doa familia na kuhatarisha usalama wao yeye ageenda sehemu nyingine akaanze maisha mapya...
Asubuhi na mapema gari ilifika,Waliagana mama alimsihi mwanaye awe makini na anapoenda Asael alihaidi kufanya hivyo mzee alimkumbatia mwanaye akampiga piga mgongoni kumfariji "take care my son" mzee aliongea...
Gari iliondoka,Asael aliishuhudia tu gari kwa mbali ikipotelea,
moyoni alipatwa na furaha familia kuondoka bila kudhurika yeye aliona kwa upande wake ilikuwa rahisi kujiokoa...
Mr Chalima leo alifika katika kanisa kubwa ambalo pia lilikuwa likijihusisha na kulea watoto yatima,mr chawala alikuwa anatumia nafasi hiyo kila alipokuwa akitoa misaada katika kituo hicho cha kulelea watoto yatima aliita wandishi wa habari,
Habari zilikuwa zinatangazwa na yeye kuzidi kujizolea sifa kuwa ni mfanyabiashara mwema,kumbe nyuma ya pazia ni nyoka....
Hivyo kupambana na mtu kama yule aliyekuwa akikubalika na wengi haikuwa rahisi,
Aliongea machache na kiongozi wa kituo kile,hata father alikuwa chini ya mamlaka ya Mr chalima,
Waliongea mengi kuhusu malezi ya watoto,
Mwisho Mr Chalima akamuuliza "vipi wangapi wamekomaa kutuingizia pesa kwa kipindi hiki nimetumia pesa nyingi sana hadi sasa kuwagharamia hawa watoto"
Father aliangalia kulia na kushoto kuhakiki kama hakuna alikuwa akiwasikiliza....
ilikuwa ni kauli tata sana ya mr chalima haikuwa rahisi kuielewa kwa upesi...
je anamaanisha nini usikose sehemu 03
[9/16, 11:36]
: NICE GUY OF CENTURY
SEHEMU YA 03
Mtunzi Asael Samwel
...ilipofika
Familia ya Mr kiwila imefanikiwa kuondoka salama mji wa Arusha,kuepuka unyama uliopangwa na Mr chalima Mfanyabiashara mkubwa jiji la Arusha,Asael bado hajaondoka bado yupo Katika jiji moja na hasimu wa Mr Chalima....
Sasa endelea...
Baada ya mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima kuulizwa swali ni Mr Chalima,kuwa ni wangapi walikuwa wamekomaa kuwaingizia pesa kwa kipindi hicho mkuu wa kituo,
Mkuu wa kituo akiangalia huku na kule kuhakikisha hakuna aliyekuwa akiwasikia alimnong'oneza...
"Mkuu kwa sasa kuna mabinti kama watatu tu ambao wanafaa kuuzika katika soko letu subiri kwa muda waongezeke...
Aliongea mtu huyo kwa utulivu kabisa,
Mr Chalima akamwambia....
"nimeshatumia kiasi kikubwa cha pesa kuwekeza katika kituo hiki cha kulelea hawa watoto hivyo kwa sasa nataka nipate faida pia wakifika angalau 10 unijulishe"
Aliongea Mr Chalima akainuka na kuanza kutoka kutoka katika kanisa hilo walipokutana kufanya mazungumzo yao...
Ni kwa muda mrefu sasa Mr chalima alikuwa akitumia mgongo wa kutoa misaada katika kituo hicho kama msamalia mwema,kumbe alikuwa anatumia nafasi hiyo kama kuwekeza kwa watoto hao kila walipofikia umri fulani hasahasa mabinti alikuwa akiwachukua na kuwauza nchi za nje hasahasa huko uarabuni na kujipatia pesa wakishirikiana na mkuu wa kituo hicho cha kulelea watoto yatima...
Asael hakuwa mbali na eneo hilo,ni wazi kwa sasa alishaamua kumfuatilia hatua kwa hatu Mr Chalima,Mara tu baada ya kugundua huyo mtu hakuwa mwema licha ya kujivika ngozi ya kondoo kwa kujifanya msamalia mwema ili kuficha uhalisia wa unyama wake,
Aliyasikia mazungumzo hayo,lakini hakufanikiwa kuyaelewa hasa yalilenga nini maana walizungumza kwa ufupi sana na kwa mafumbo mengi,aliamini kuna wakati ungefika angeelewa tu hakuwa na shaka alitoweka hilo eneo...
Nyumbani kwa Mr Chalima
Mke wake alikuwa na Mama yake (mama mkwe wa Mr chalima)
Mama alikuwa anamlalamikia mtoto wake ni kwa muda gani angeendelea kumdanganya mmewe kuwa anaujauzito wakati hakuwa na ujauzito...
Mke wa Mr chalima alimtazama mama yake akamwambia,
"mama usijali kila kitu kitakuwa sawa tu mtoto atapatikana na mimi nitatoa haya matambara nitamfanya huyo mtoto ni wangu na mchezo utaishia hapo"
Aliongea mke wa Mr chalima kwa kujiamini sasa...
Mke wa Mr chalima tangu aolewe hakuwahi kupata mtoto,na mmewe kila mara alikuwa akimpigia kelele kuwa anataka mtoto atakayekuwa mrithi wa mali zake hivyo ikamlazimu yeye kutengeneza ujauzito feki ili kulinda ndoa yake na kumlizisha mmewe...
Mama aliendelea kuhoji,
je huyo mtoto utamtoa wapi?
Hujui kama hii ni hatari siku moja mmeo akija ajue ukweli?
Mama aliuliza maswali kwa mfululizo sana kuonyesha alikuwa na wasiwasi sana kwa alichokuwa akikitenda binti yake...
Bintiye(Mke wa mr chalima)
Alimwambia asihofu hayo yote yasingetokea.
Upande wa pili Asael aliamua kurudi katikati kazi yake ya guta ili kudunduliza pesa zimsaidie kuondoka katika mji huo kama alivyokuwa amemhaidi mama yake hataishi hapo te ataondoka,
Akiwa amekaribia kufika kazini kwake,akaangalia kwa umakini eneo hilo aligundua Vijana wa Mr chalima bado walikuwa wakimtafta hivyo walijitega makusudi katika eneo lake la kazi wakitambua wazi lazima tu angerudi kazini na wao wangempata kiurahisi...
Alijua tayari eneo hilo halikuwa salama tena kwake,alihairisha kwenda...
Ulikuwa ni wakati wa kupata chakula cha mchana,familia nzima ya Mr chalima ilikuwa pamoja mezani wakipata chakula cha mchana...
Mr chalima alikuwa anakula huku akiendelea kupiga story za hapa na pale..
"mke wangu mimi huwa napenda sana kula nyama ya paja iliyo kaushwa vizuri hasahasa na mke wangu"
Mr chalima aliongea kwa masihara,
familia yote ikaishia kumcheka...
akaendelea kuongea,
"mke wangu natumaini hata mtoto wangu junior alizaliwa atakuwa anapenda kula kama baba yake nilivyo"
Mamamkwe akashituka sana baada ya kusikia maneno hayo kwani alijua wazi kilichokuwa kikiongelewa halikuwepo kabisa,mke wa mr chalima hakuwa na ujauzito...
akajifanya amepaliwa na chakula ili kuipotezea ile hali ya yeye kushituka...
"ooh samahani jama tatizo dogo nakuja"
Aliongea Mama akatoka nje...
Asael sasa aligeuka mtu wa kujificha ficha tu sehemu ya kula hakuna kazi hana,pesa zote za akiba alishatumia kuisafirisha familia yake alibaki akizurura tu mtaani...
Aliingiza mkono akatoka na 2000 pesa ya kitanzania pesa ambayo isingemtosha hata kwa siku mbili mbele,Giza lilianza kushika hatamu hakuwa na sehemu ya kulala...
Aliwaza angefika vipi hata kama angeamua kuondoka mji Wa Arusha wakati hakuwa na pesa wakati huo kula kwenyewe ulikuwa mtihani?
Alijisogeza uchochoroni kwa bahati akaona walalahoi hoi wamejipumzisha kwenye uvungu wa gari bovu bovu,naye akaona ingemfaa kulala kwa siku hiyo ili kesho aone pakuelekea....
Alivuta usingizi wa bila shuka,Sasa kipindi akiwa amelala kumbe aliingilia dili za watu aisee...
Kumbe katika wale walalahoi waliolala pale,mmoja hakuwa mlalahoi alitumia tu njia ya kujifanya mlalahoi kumbe moyoni alikuwa akiwaza vingine,
Aliamka kipindi wenzake wakiwa wamelala fofofo taratibu,akashika begi lake dogo akalifungua kwa umakini mkubwa alitoa sindano akaiweka sawa akaitia dawa aliyoijua yeye taratibu alianza kumwendea Asael lengo amdunge hiyo sindano katika bega lake....
2017 Asael Samwel
Sijui huyo mtu analenga nini kuamua kumdunga sindano Asael,
Je atafanikiwa kutimiza???
[9/16, 11:37]
: SEHEMU YA 04
...ilipofika
John anajikuta katika wakati mgumu hana kazi,pesa,mji mzima anatafutwa hana makazi anaamua kujumuika na walalahoi wa mtaani ili angalau alale siku ipite anangukia katika mikono ya mtu anayetaka kumdunga sindano...
Sasa endelea....
Mtu huyo alikuwa tayari kabisa kudunga sindano lakini bahati haikuwa ya kwake siku hiyo,ghafla Asael akajigeuza kujikinga na baridi maana alilala bila hata kujifunika kitu cha kumkinga na baridi ya usiku...
Hicho ndio kilimsaidia ila akapata wasiwasi juu ya mtu huyo japo hakuiona sindano,alijifanya hakuelewa chochote alihitaji kujua lengo hasa la mtu yule aliendelea kulala...
Huyo aliyeshika sindano akajua hakuonekana,akashukuru lahasha hakujua kuwa tayari alishaonekana akaona huo ndio muda mwafaka wa kutimiza lengo lake akamuendea Asael kwa mara nyingine tena,
Taratibu akaiangalia sindano yake ilikuwa sahihi,Asael aliogopa baada ya kugundua huyo mtu alikuwa na lengo la kuwadunga sindano....
Alimvizia wakati anapeleka tu mkono begani akaudaka!!
Wakaanza kinyang'anyana sindano wakiwa humo uvunguni mwa gari hilo bovu...
Walisumbuana sana mwisho,Asael akafanikiwa kumdhibiti huyu mpuuzi...
Akamtoa nje ya uvungu akamvuta katika uchochoro uliokuwa karibu...
Akaamua kumhoji kwa amani kwanza kabla ya shuruti,
"hizi sindano zilikuwa za kazi gani"
Asael aliuliza...
akarudia swali mara kadhaa bila ya majibu kutoka kwa mtu yule,
akafikiri huenda alitumwa
"nani amekutuma hii kazi?"
bado kimya kiliendelea,
Asael aliwaza kwa sekunde chake,
akajisemea moyoni...
"nikiendelea kumbembeleza huyu mtu hatutafika popote mimi sina ofisi ya mahojiano mimi mwenyewe sina hata sehemu ya kulala...
alimpa onyo huyo mtu,
"nahesabu mpaka tatu usipojibu tutajua cha kufanya"
Aliongea Asael kama alikuwa na masihara vile...
Kwa mwili wa Asael ulivyoonekana mdogo yule bwana alijua huyu hana cha kunifanya cha msingi ananitisha tu hakujua udogo wa mwili haukuwa sababu ya yeye kujiamini,
Asael alianza kuhesabu...
1......
2......
3.......
mpaka alifika tatu bila ya kusikia yule bwana akinyanyua kinywa chake...
Hasira ilimshika aligundua alidharaulika....
Alimpiga goti akamkandamiza kwa kiwiko,
akaugulia maumivu
"nitakueleza"
kauli ilimtoka yule bwana
"sawa ongea"
Asael aliongea..
"Mimi nimetumwa na boss wangu wa gang fulani na siko peke yangu kuja huku mtaani kupanua soko la biashara yetu ya madawa ya kulevya"
kupanua soko kivipi?
Asael aliuliza
Nyumbani kwa Mr Chalima,
usiku akiwa amelala aliota ndoto Mtu amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kutoboa kila aina ya biashara na vitu vyake haramu"
Ghafla akaamka kwa mshituko...
Hapana!!
alipiga kelele akisema "hapana"
mpaka mke wake akaamka
"nini mme wangu"
mkewe akamhoji
"usijali mke wangu ni ndoto tu lala"
Mr chalima alimsihi mkewe asiwe na hofu wakalala...
Moyoni Mr chalima alijiapia "lazima nimkamate kijana huyu lasivyo atanitia kizuizini kabla sijamtia mimi ili nibaki salama"
aliweka nadhiri ya kumkamata Asael ili aishi kwa amani...
upande wa pili yule mtu akaendelea kumweleza Asael,
"Tunapanua soko kwa kuwadunga watu hasa vijana madawa ya kulevya,baada ya hapo wanaathiriwa,wanageuka mateja basi sisi tunapata soko la kuuza madawa yetu ya kulevya,
hata leo ningefanikiwa kujifunga ile sindano lazima ungenitafta tu ili nikuuzie madawa ungekuwa mtumwa wetu moja kwa moja"
Asael alijikuta akinyong'onyea baada ya kusikia hayo maneno...
yule mtu alipata upenyo akakimbia...
Asael akarejea katika uvungu akachukua kile kibegi,ndani akakuta mabomba kibao na sindano vichupa vya madawa ya kulevya na pesa,akachukua pesa maana alikuwa na tatizo la pesa akatokomea kutoka hilo eneo....
Mke wa Mr Chalima alifika hospitali akashuka kutoka katika Gari yake akiwa na mama yake,moja kwa moja akaingia katika hosipitali,alikuta wagonjwa wakisubiri huduma,
kwa kiburi na dharau yeye akaingia moja kwa moja....
Alifika mpaka ndani,akaongea na nesi mkuu kwa muda mchache,mwisho akaulizwa vipi umekuja kiliniki mama?
"hamna ninamaongezi na wewe naomba wamasiliano na wewe"
aliongea mke wa mr chalima,
nesi hakuwa na neno akampa namba ya simu ya mkononi....
Asael alifika kituo cha mabasi,alikuwa anatafuta tiketi mwisho alipata lengo lilikuwa ni kwenda mwanza,Aliambiwa gari itaondoka jioni aliondoka akasubiri muda ufike...
Alitazama mkononi alikuwa bado amebaki na pesa kiasi flani alizozipata jana katika begi lile la mtu yule aliyemweleza kuwa anapanua soko alikimbilia kwa mama ntilie ili apate angalau hata chai....
Mke wa Mr chalima leo alimuita yule nesi ili wapate chakula cha mchana pamoja apate nafasi ya kueleza shida yake,
Wakiwa wanaendelea kupata chakula Mrs chalima aliona huo ndio wakati mwafaka wa kueleza shida yake...
"nesi mimi nashida....
nataka unitaftie mtoto"
Nesi alishituka "nikutafutie mtoto kivipi?"
Nesi alihoji kwa mshituko mkubwa
"usijali nesi wewe huwa unahusika na uzalishaji hapo hospitali hivyo sioni kama ni kazi kupata mtoto"
aliongea kwa kujiamini
Nesi alisema...
"sipo tayari kwa ujinga kama huo mtafute mtu mwingine"
Aliongea Nesi kwa kwa kujiamini na kuanza kuondoka...
"Subiri"
Aliongea mke wa Mr Chalima,
Nesi akageuka,
"unajua kuwa mme wangu anaasilimia 60 ya umiliki wa hiyo hospitali,ukifanya mchezo kazi utakosa tunza hili akilini Nesi,kazi lazima ufanye"
Aliongea mke wa mr chalima kwa vitisho na kujiamini
Akaitaka mhudumu akamlipa pesa ya aliyotumia kupata huduma hapo akaondoka....
Asael alikuwa katika basi tayari kwa safari ya kwenda Mwanza, Haikuchukua muda safari ikaanza taratibu alianza kuuacha miji aliokulia,
moyoni hakuwa na kinyongo aliamini kule alipokusudia kwenda angeishi kwa amani huku akiendelea na mipango yake...
2017 Asael Samwel
je Asael atafika salama?
vipi kuhusu mipango ya mke wa Mr chalima?
Usikose sehemu ya 05
: NICE GUY OF CENTURY SEHEMU YA 01

: SEHEMU YA 02...ilipofika

: NICE GUY OF CENTURYSEHEMU YA 03

2017 Asael SamwelSijui huyo mtu analenga nini kuamua kumdunga sindano Asael,
Je atafanikiwa kutimiza???
[9/16, 11:37]
: SEHEMU YA 04...ilipofika

2017 Asael Samwelje Asael atafika salama?