Simulizi, "Mwacheni aishi"

Simulizi, "Mwacheni aishi"

JJ FORMAR

Member
Joined
May 29, 2025
Posts
34
Reaction score
32
Karibuni sana wapenzi wa simulizi, Leo naitambulisha kwenu simulizi hii iitwayo "MWACHENI AISHI." Ndani ya simulizi hii utakutana na visa, mikasa na matukio ya maisha kwa ujumla, vimbwenga, mapenzi wivu, usalitu, chuki, mauaji, na kadharika. Mwandishi anakukaribisheni kutoa maoni ushauri na mapendekezo usomapo simulizi hii.

Simulizi, "MWACHENI AISHI"

SEHEMU YA KWANZA.

Amini Usiamini lakini hali ilikuwa tofauti na vile wahenga walivyouaminisha ulimwengu ya kwamba "usiku wa deni haukawii kucha" maana licha ya kwamba haukua usiku wa deni lakini kwa maoni yake ni kwamba usiku huu ulikuwa mfupi mno, yaani ni kama jana yake giza lilichelewa kuifukuza nuru duniani, na sasa limeharakisha kuikimbia dunia.
"Aisee, yaani leo ni kama vile sijalala kabisa, yaani kujiegesha kidogo tu tayali kumekucha" aliongea mwanaume mmoja wakati akijiinua kivivu toka kwenye godoro lake ambalo limetandikwa sakafuni pasipo uwepo wa kitanda.

Alijinyanyua taratibu huku akijinyoosha na kupiga miayo kwa mkupuo, aliyafumbua macho yake na kuanza kuangaza huku na kule akitafuta ni wapi simu yake ilipo, kwa hasira aliitazama simu hiyo ambayo mda mchache uliopita ilitoa mlio mkali ulimuamsha mwanaume huyu. Hakuwa na shaka kuhusu muda, kwani ni yeye mwenyewe aliyetega alamu kwenye simu hiyo, hivyo aliamka na kuchukua taulo na baadhi ya zana zake za usafi, akatoka mle ndani kuelekea maliwato ambako angejifanyia usafi wa mwili.

Mawazo mengi yalikuwa yakipita kuchwani mwake, alilikumbuka vema tukio la jana yake usiku lilopelekea mpaka akachelewa kulala, tukio ambalo kwake lilikuwa zaidi senema za kihindi ziaminikazo kuwa na matukio mengi ya uongo. Alipomaliza kuoga aliingia ndani kujiandaa, muda mwingi alikuwa akiitazama simu yake akionekana kutegemea jambo fulani kutoka kwenye simu hiyo. Naam, haukupita mda mrefu simu yake ilitoa mwanga hafifu uliofuatiwa na mlio mkali wa kumfanya mwenyewe aisikie hata awapo katika mazingira ya fujo, aliichukua kisha akabofya kitufe cha kupokea "Vipi jamaa, nimekaribia hapo, fanya haraka, nikukute tayali tuondoke maana mda umeenda sana," ,,,"sawa, " yalikuwa ni maongezi mafupi aliyoyafanya na mtu wa upande wa pili aliyeonekana kuwa mtu wake wa karibu.

Haukupita mda, ulisikika mrio wa pikipiki nje ya nyumba, mwanaume huyu akachukua begi lake dogo la mgongoni na kutokanalo nje ambako alifika na kupanda pikipiki hiyo ya rafiki yake ambaye aliitoa kwa kasi, " Oya Nemes vipi huko utokako, kwema?"> "kunakuwaje kwema jamaa yangu, yaani hapa nangojea leo jioni ifike, lazima yule dogo aondoke, kama kazi imemshinda bora arudi kijijini asijeniletea matatizo mjini hapa" aliongea dereva yule wa pikipiki ajulikanae kwa jina la Nemes. "

Ndiyo mmeafikiana hivyo?" Aliuliza mwanaume huyu ambaye mda huo alikuwa akihangaika kushikilia vizuri pikipiki ile iliyokuwa ikikimbia kwa mwendo wa kasi sana. "Lazima aondoke hilo halihitaji majadiliano yoyote, maana naona kabisa huu ni mchezo ananifanyia, hembu angalia, hii ni wiki ya pili sasa, na bado hali yake ni ileile haibadiliki, wewe unafikiri ni nini kinafatia hapa kama siyo mimi kuanza kumlea kama mtoto mdogo? Hafanyi kazi yoyote, yeye wa kula tu, hata hela aliyokujanayo imeisha kabisa." Nemes alitao maelezo hayo ambayo yalilenga kumshawishi mwenzake "Shida yako unajifanya kutokuelewa nini kinamsumbua bwanamdogo, yule ni mgonjwa kaka, sasa kwanini ulazimishe awe anashiriki kazini, ungekuwa wewe ungeweza? haya ni maisha tu kaka." Yule mwanaume alimjibu Nemes akionesha kutakubaliana na mpango wake.

Safari yao ilikuwa ya kwenda nje kidogo ya mji kwani hata walipofika njia panda ya Chiwangu waliiacha balabala ya kuingia soko kuu la mkoa na kuifata Ile ilekeayo nje ya mji huku wakizidi kuzozana katika mazungumzo yao. Nemes anaonekana kukasilishwa na kutokubaliana na hali ya mwenzao waliyemtaja kuwa ni mgonjwa. "Oya haijalishi na wala sitajari ni undugu gani uliopo kati yetu, yaani kwa hali hii, sioni kama tutawezana tena, kesho lazima dogo aondoke, siwezi kuendelea kulea ujinga" aliongea Nemis kwa sauti ya juu ili mwenzake aweze kumsikia "lakini ukumbuke wewe ndiye uliyemshawishi mpaka akakubali ", " nakumbuka, lakini mpango si ilikuwa aje tupige kazi? "

Nemesi aliendelea kuhoji, huku akionesha kushikilia msimamo wake na kutokubaliana na mwenzake huyu."sawa, hili suala ni lakwako, Mimi nafikiri halinihusu saana, lakini katika yote utakayoamua ukumbuke ni ndugu yako yule, niwewe unapaswa kumsaidia kwanza kabla ya wengine." Mazungumzo yao yaliendelea wakiwa tayari walishauacha mji.

Ilikua ni safari ya takribani nusu saa, kutoka mjini mpaka huku waliko sasa, lilikuwa ni eneo kubwa la wazi ambapo kulionekana kuwapo baadhi ya majengo ambayo bado hayakuwa yamekamilika, hapa ndipo safari ya Nemes na mwenzake ilipoishia. Waliipaki pikipiki yao katika eneo maaaluma ambako kulikuwepo magari kadhaa na pikipiki, waliingia ndani ya jengo moja ambako hawakukaa sana, walitoka wakiwa wamevaa sare kama walizovaa baadhi ya watu waliokuwepo hapo. Walikua ni mafundi ujenzi(waashi) na hapo ndipo walipokuwa wakifanyia kazi ya ujenzi.

Yapata saa tatu za asubuhi sasa, ni ndani ya nyumba moja ndogo anaonekana Kijana mmoja, amelala sebuleni juu ya kochi, haukupita muda kijana yule aliamka akionekana kutokuwa sawa hata kidogo, sura yake ilikosa nuru kutokana ina le hali ya kutoka usingizini, alijiinua pale alipokuwa amelala na kwenda maliwato ambako alijifanyia usafi wa mwili. Kichwani alikuwa akiwaza mengi, alitamani walau angekua na uwezo, wa kubadirisha mfumo wake wote wa maisha lakini alijua kitu hicho hangekiweza kamwe.

Baada ya kumaliza kunawa alirudi tena sebuleni ambapo kwa sasa hakulala kama mwanzo, alikaa kwenye kochi ambalo bila kupenda lilibonyea kutokana na uzito wake. "Siamini kama kweli haya yanayonikuta ndiyo mpango wa Mungu juu ya maisha yangu" alijisemea kijana huyu. " Kwahiyo jamaa anataka niondoke?, du! sijui itakuwaje, yaani nirudi kule tena!, hii itakuwa hatari sana kwangu, siwezi, siwezi kabisa kufanya kitu kama hiki." Alikuwa katikati ya dimbwi la mawazo ambayo yalimchanganya sana, hakukubaliana na mchakato uliokuwa ukifanywa juu yake, "eti anasema atanipa nauli nirudi niondoke, hii ni sawa kweli! na vipi kuhusu pesa? Au ndiyo anataka anizulumu" alipowaza kuhusu kuzulumiwa mawazo yake yalimpeleka mbali sana, alikumbuka namna alivyohangaika mpaka kupata pesa ambazo yeye aliamini kuwa zingekuwa mwanzo wa kuishi maisha mazuri, maisha ambayo yangemuweka mbali na shida alizozipitia huko nyuma.

Hakuamini kabisa kwamba leo hii ilitakiwa iwe siku yake ya mwisho kukaa mbali na shida, ambapo kesho yake alipaswa kuondoka, "Hapana, haiwezekani, yaani niondoke mikono mitupu" akili yake iligoma, iligoma kabisa kukubaliana na mpango uliokuwepo. "Lazima nitafute namna ya kufanya, lazima nibaki" aliwaza hivyo, lakini uso wake ulipatwa masikitiko baada ya kukumbuka hali yake ya ugonjwa uliomsumbua. "du! Sijui itakuwaje, lakini siondoki, bora nifie hukuhuku" ni kauli ya kishujaa ambayo aliitoa, akionekana kuwa na mengi moyoni mwake yaliyokwisha uumiza moyo wake. Hakuwa na usingizi ambao ungemfanya kulala tena hivyo alipanga kwenda mgahawani akapate kifunguakinywa kuiganga njaa aliyokuwanayo.

Alitumia zaidi ya dakika kumi kufika mgahawani, "KWA MAMA ZABI VYAKULA VITAMU" ndivyo lilivyosomeka bango kubwa lililowekwa juu ya mgahawa huo, ulikuwa mgahawa maarufu sana maeneo hayo, umaarufu wake ulitokana na huduma bora iliyotolewa mahali hapo. Huu ndio mgahawa pekee uliopo jirani na makazi ya kijana huyo, na hapa ndipo amekuwa akifika mara nyingi kupata chakula, "karibu Tena Morisi" sauti hii lilipenya kwa namna yake ndani ya Ngoma za masikio ya kijana huyu ambaye tunamjua sasa kwa jina la Morisi, ilikuwa ni sauti ya binti Nasma mfanyakazi wa mgahawani hapo iliyokuwa ikimkaribisha kwa bashasha kubwa kijana Morisi.

"Ahsante" alijibu Morisi kwa sauti ambayo haikuonekana kujari wala kuendana na lile bashasha alilokuwa nalo binti mhudumu ambaye alionesha kutopendezwa na jibu hilo, "Chai Moja, Chapati mbili" aliongea Morisi kuagiza kifungua kinywa hicho ambacho hukipendelea sana. Binti huyo alimuandalia mteja wake kile alichokiagiza lakini badala ya kuweka chapati mbili aliweka nne na kupeleka pale mezani alipokaa Morisi. Morisi alishangaa kuona ameletewa zaidi ya alivyoagiza, "labda atakuwa amechanganya, chakwangu kampatia yule jamaa" alijisemea moyoni huku akitarajia kumwona jamaa yule akiulizia ziada yake jambo ambalo halikutokea kwani jamaa yule alianza kula chakula chale bila kuuliza. Morisi hakuwa mjinga kula zaidi ya vile alivyoagiza kwa maana alilijua balaa la mamant'ilie namna wanavyokuwa watata sana kudai pesa zao ni kwasababu pesa ya kulipia alikuwa nayo ndiyo maana aliamua kula zile chapati zote maana alizimudu,,,,,,,,,,,,ITAENDELEA.
 
TULIPOISHIA,,,Morisi hakuwa mjinga kula zaidi ya vile alivyoagiza kwa maana alilijua balaa la mamant'ilie namna wanavyokuwa watata sana kudai pesa zao ni kwasababu pesa ya kulipia alikuwa nayo ndiyo maana aliamua kula zile chapati zote maana alizimudu,,,,,,,,,,,,ENDELEA
Kitendo hicho hakikumpendeza Nasma kwani ilikuwa kinyume na mpango wake, ukimya wa Morisi ndio ulimfanya Nasma kuhisi labda alichanganya sahani wakati wa kuzipeleka, maana walikuwepo wateja wengine aliowahudumia kwa mda ule, hivyo alipanga akajipitishe tena karibu na alipokaa Morisi ajifanye kusafisha baadhi ya meza zilizokuwa pembeni, lengo lake ilikuwa aone na kuhakikisha kama kweli ile sahani yenye chapati nne aliyempatia ni Morisi. Alichukua kitambaa na kwenda kuutekeleza mpango wake, mapigo ya moyo wake yalidunda mbiombio sana kiasi cha kumfanya mikono yake kuanza ketetemeka kwa mbali, hali hiyo haikumfanya kuacha kutekeleza kile alichopanga, alipiga moyo konde akaendelea kufanya alichokusudia.
Huenda hiyo ingekuwa kazi nyepesi sana kwa mabinti wengi wa mjini, ambao uchangamfu ndiyo sifa yao kubwa, lakini hali haikuwa hivo kwa binti huyu ambaye alinekana kuwa mzito sana kufanya maamuzi hayo. Nasma hakuwa msichana wa kupapalikia wanaume, hakua yule ambaye angejirahisisha kwa wanaume wampatie vichenchi kadhaa na kuishia kuutumia mwili wake watakavyo, wala hakuwa msichana yule ambaye angelainishwa haraka kwa maneno matamu yaaliyosheheni ushawishi toka kwa wanaume wachokozi. Ungewauliza watu wengi hasa vijana wa kiume waliowahi kumtongoza binti huyu basi wasingesita kukwambia "huyu demu ni kauzu kinoma", kutokana na misimamo yake.
Harakati za Nasma kumfatiria Morisi hazikuanza leo, kinachofanyika leo ni matokeo ya kile ambacho mwanzoni Nasma alikipuuzia sana. Ilikuwa hivi, Kutokana na ukarimu wake kwa wateja wa rika zote, Nasma alitokea kukubalika na kupendwa sana na wateja wengi, jambo hilo lilimfurahisha sana mwajili wake kwani mauzo ya mgahawa wake yaliongezeka mala dufu, mpaka akafikiria kuuacha mgahawa mikononi mwa binti huyo yeye awe anakuja kuchukua fedha za mauzo. Kuna wale waliovutiwa zaidi na urembo wa sura na umbo matata alilokuwa nalo binti huyu ambao ndio hao waliokuwa wakipisha Kila mmoja akitaka kujaribu bahati yake kwa binti huyo.
Nasma amekuwa akisumbulia na wanaume wengi wakijaribu kumtongoza hasa vijana mabodaboda ambao walishindana kuhitaji kumnasa binti huyo kimapenzi, hata hivyo waliishia kukataliwa na binti huyo ambaye asingeacha kuwatishia kuwa angemweleza mwajili wake endapo wangeendelea kumfatilia, hayo yakawa ndiyo maisha yake, alishazoea kusumbuliwa na wanaume watu wazima wenye familia zao, wenye wanawake wao ambao yeye huwaita mama. Asilimia kubwa ya vijana wakazi wa eneo hilo walishawahi kumtongoza, hivyo mpaka kufika wakati huo alishajenga imani potofu juu ya wanaume, aliamini wanaume wote wanatamaa yamapenzi, warafi na wasioridhika hata wangepewa nini, Imani hiyo ndiyo ilimfanya kuwa msichana katili wa hisia asiyetaka masihara na mwanaume yeyote walimwita kauzu maana hakutaka mazoea nao, "alikuwa bingwa wa kuchomoa pale ambapo angechomekewa vishawishi vya mahaba"
Yapata wiki mbili sasa tokea Nasma amjue Morisi ambaye ni ghafla amekuwa mteja wake wa uhakika, mwanzoni alimuona kuwa kijana mhuni tu kama walivyo vijana wengine hivyo hata wakati Morisi alipomsalimia hakumchangamkia kwani alijua mwisho wa uchangamfu wake nini kingetokea. Baadae uhalisia uliiisariti vibaya imani ya binti huyo maana Morisi hakuwa mtu wahivyo, licha ya kuwa hufika mgahawani hapo mala kwa mala, lakini hakuwahi kuonesha hata dalili za kumtamani Nasma, yeye angekuja mgahawani hapo kupata chakula kisha kuondoka, hakuwa muongeaji sana na mala zote afikapo angeongea aidha wakati akiwa anasalimia au kuagiza chakula, akishamaliza kula hulipa na kuondoka.
Huenda tabia ya ukimya wa kijana huyu ndiyo iliyomvutia Nasma ambaye sasa alihitaji kujenga ukaribu na kijana huyo, jambo hilo halikuwa jepesi kwake, maana mbali na ukauzu wake, Nasma hakuwahi kupata hata dakika moja ya kuongea na kijana huyo kwani malazote Morisi hufika mgahawani hapo mida ya asubuhi ambapo angemkuta Mama Zabi maeneo hayo. Uwepo wa mwajili wake ulimnyima nafasi ya kuongea na kijana huyo. Leo hii ndiyo imetokea nafasi ambayo Nasma aliona ni kama "zari la menteli" lililomfikia, Morisi amefika na kumkuta akiwa peke yake, hii kwake ilikuwa zaidi ya fursa, hivyo aliwaza namna gani angemuanza kijana huyu ambaye hakuwa na mazoea naye, ndipo aliamua afanye kitu ambacho kingemfanya Morisi mwenyewe kuanza kumuongelesha. Alivizidisha vitafunwa vile makusudi kabisa akipanga kuvitumia kama kete yake ya ushindi dhidi ya kijana huyo.
Morisi ambaye hakuwa akitambua mpango wa Nasma aliendelea kunywa chai yake taratibu, huku akiwa bize na kisimu chake cha mchina, alimuona Nasma akizunguka kusafisha baadhi ya meza, hapo akajipapasa mfukoni na kuiandaa hela ili mhudumu huyo akimfikia aweze kumpatia. Nasma baada ya kutimiza lengo lake hakuwa na sababu ya kuendelea kusafisha meza zile ambazo kiuhalisia hazikuwa zimechafuka, hivyo akaondoka mle ndani na kurudi eneo la jikoni, "Sasa mbona hajaniongelesha" aliwaza Nasma kwani alishajiridjisha kuwa aliyekuwa amempatia sahani ile ni Morisi "au atakuwa anasubili amalize kwanza kula ndipo anieleze, au,,, ngoja nimsubili akija tu kunipa hela nitamwongelesha." Aliongea binti huyu ambaye ungedhani kuna mtu alikuwa akishauriana naye, hakukaa sana kutafakari hilo ndipo alisikia sauti ya vishindo vya miguu ikisogea upande wake, aligeuka ghafla na hapo ndipo alipomwona mfanyakazi mwenzake wa kiume akija upande ule, "vipi, Kuna jamaa kanipatia hii hela na,," hakumsubili amalize kauli yake "kwahiyo ndio unaniletea Mimi, kwani wewe ukikaa nayo Kuna shida gani" Nasma aliongea kisha akaichukua ile hela na kuondoka, hakutaka kuendeleza maongezi yale kwani alikuwa na mpango wake aliohitaji kuukamilisha sasa.
Haukupita mda Nasma alirudi tena kule jikoni awamu hii alikuwa ni mwenye haraka,"wewe, ni nani kwani kakupatia hiyo hela?" Alimuuliza mwenzake ambaye alimjibu kuwa kuna kijana mrefumrefu mweusi ndiye aliyekuwa amempatia ile hela. Baada ya kusikia vile Nasma alitoka pale kwa haraka kuelekea barabarani, kilikuwa ni kitendi cha haraka ambacho kilimwacha mwenzeke akishangaa, huko balabalani Nasma aliishia kuangaza kulia na kushoto kama vile kuna mtu alikuwa akimtafuta bila mafanikio,"aghhhhh" alilalama binti huyu kwa hasira, hakumuona yule aliyemtafuta wala hakujua alikoelekea ni wapi. Kwa unyonge aliaanza kurudi kule mgahawani huku akijifinyafinya vidole vya mikono yake, alijilaumu sana kushindwa kuwa makini mpaka Morisi kuondoka akiwa hajaongea nae. Kunakitu aliwaza na kuanza kutabasamu mwenyewe,"kwanini nilishindwa kuongea nae mda wote, aah ningeongea naye tu" aliwaza hayo wakati akiwa anaitazama ile hela aliyopewa akiwa alishajua aliyeilipa ni Morisi, "kwahiyo amelipia mpaka zile nilizomuongezea, du! Si itakuwa nimemtia hasara kaka wa waitu,,,lakini anaonekana anaroho nzuri, kesho akija lazima niongee nae,,..na nitaongea nae Nini?" alikatisha mawazo yake baada ya kugundua kuwa hakuwa hata na kitu chochote cha maana alichohitaji kumwambia kijana yule, kilichobakia usoni mwake ni tabasamu mwanana lililoacha vishimo kwenye mashavu yake, hakuelewaka lilikuwa tabasamu la kufurahia nini. "Mambo vipi mrembo" ilisikika sauti nzito ya mwanaume mmoja aliyeingia mgahawani mda ule, Nasma alikuwa akimtambua mtu huyo kwani ni miongoni mwa wale waliokuwa wakimsumbua sana, ijapokuwa alikuwa akimchukia mwanaume huyo ambaye kwa umri alikuwa ni zaidi ya baba yake, hakuwa na namna ilibidi amsikilize kwa ukarimu "ndiyo wateja wenyewe hawa" alijiongelesha Nasma huku akiinuka kwenda kutekeleza maagizo ya mteja wake......
ITAENDELEA,
 
Tukutane jioni kwaajili ya mwendelezo, sehemu ya pili ipo njiani kukufika,
Karibu sana, ✍️✍️✍️✍️✍️✍️
 
🤝🤝
 
TULIPOISHIA. Nasma alikuwa akimtambua mtu huyo kwani ni miongoni mwa wale waliokuwa wakimsumbua sana, ijapokuwa alikuwa akimchukia mwanaume huyo ambaye kwa umri alikuwa ni zaidi ya baba yake, hakuwa na namna ilibidi amsikilize kwa ukarimu "ndiyo wateja wenyewe hawa" alijiongelesha Nasma huku akiinuka kwenda kutekeleza maagizo ya mteja wake......
ITAENDELEA,
Mithili ya Simba mwendapole, ndivyo alivyokuwa akiikatasha mitaa, alikiinamisha kichwa chake akitafakari hatma wa maisha yake ndani ya mji huu,"ngoja nisubili nione atanipatiia nauli kiasi gani, akinilipa na ile pesa yangu nitaongea na baba Sesi anisaidie kutafuta chumba nipange, sitaondoka mjini kwa sasa,,,lakin,,,.." ghafla alishtushwa na mlio wa Joni ya bajaji nyuma yake"we dogo vipi, acha ujinga mjini hapa, utakuja kugongwa fala wewe" ilikuwa sauti ya dereva bajaji akimwongelesha kwa hasira kijana huyo aliyeonekana kuwa mshamba mjini "yaani unatembea kiboya boya tu kum,,,," alifoka tena dereva yule awamu hii akimtukania mama yake na kuondoka. Maneno Yale yalimuumiza sana Morisi, hasa lile tusi, alitamani japo angemkamata yule dereva amshikishe adabu kidogo lakini uwezo huo hakuwa nao. Ndani ya gari moja lililokuwa karibu na eneo la tukio zilisikika sauti za watu wakiteta "Hawa vijana wakishavuta bangi akili zinawaruka kabisa," " Siyo bange hiyo, huyo ana stress(msongo wa mawazo) atakuwa kaachawa huyo" maneno yalipenya vema masikioni mwa Morisi ambaye hakujishughulisha nayo kwani kauli kama hizo alishazizoea, kauli za watu ambao humwelezea mtu hata wasiyemjua. Wakati huu Morisi alijitahidi kutembea kwa umakini sana kuepukana na matusi ya madereva wasio na staha hata kwa yule wasiyemjua.
Alipofika myumbani, alianza kufanya usafi wa baadhi ya nguo zake, alijiandaa ili hata akitimuliwa basi aende na nguo safi, akiwa anaendelea na shughuli hiyo mala simu yake ikaanza kuita kwa fujo, aliitazama kisha akabonyeza kitufe cha kupokea, "haloo" ilisikika sauti ya upande wa pili ambayo bilashaka Morisi aliifahamu vema. Zaidi ya dakika nne zilikatika akiwa bado anaongea na simu, alikuwa akiongea kwa uchangafu sana akionekana kufurahia maongezi yale. Mda huo kwaharaka ungemuona Morisi mwenye uso wa furaha akitabasamu na kucheka, lakini ukiongeza umakini na kumwangalia vizuri, basi ungegundua haikuwa furaha ya kweli, ni tabasamu bandia liliojengeka usoni mwake. Ili kuakisi uhalisia wa mazungumzo aliyokuwa akiyafanya, ilimlazimu kuigiza tabasamu na sauti yenye bashasha ingawaje macho yalimsaliti, hakulijali hilo, alilenga kutimiza kile alichokuwa akifanya, kuchekesha, ndiyo aliigiza furaha kumhamdaa mtu wa upande wa pili.
Baada ya simu ile kukatwa, Morisi alihema kwa nguvu mithili ya mkimbiza upepo, aliirudisha simu mfikoni na kuendelea na kazi yake, kichwani aliwaza kuhusu mtu aliyetoka kuongea nae "nipo salama, ndiyo, anapaswa ajue hivo tu". Hakukaa tena kuendelea kufua, alinyanyuka na kuingia ndani, lakini baada ya muda kidogo alitoka akiwa amelishikilia begi dogo la mgongoni, alipanga kulisafisha pia hivyo akaanza kutoa humo baadhi ya vitu vyake ambavyo huvitunza humo.
Baada ya kuvitoa vyote alilikung'uta begi like ili kutoa vumbi lililokuwa kwa ndani, hapo ndipo kilidondoka kimfuko fulani ivi cha karatasi nyeupe, yawezekana alijua nini kimo ndani yake ndiyo maana alikiokota kwa haraka sana akihofia kisilowanishwe na maiji yaliyozagaa mahali pale, alikifungua na kutoa humo kipande kidogo cha kalatasi ngumu. Haikuwa karatasi ya kawaida bali ilikuwa ni picha yenye taswira ya watu sita wenye nyuso za furaha, aliikodolea macho picha ile kwa kitambo kidogo akioneka kutafakari kitu kuhusiana na picha ile, mawazo yalimrudisha nyuma mpaka siku ilipopigwa picha ile . Ilikuwa ni siku ya furaha, siku ya mahafari ya mdogo wake aliyekuwa akihitimu darasa la saba, Morisi alikuwa msitali wa mbele kuhakikisha furaha hiuo ya mdogo wake, alihusika katika kila tukio la siku ile, ilikuwa baada ya sherehe kuisha ndipo walipopata wasaa wa kupiga picha ya pamoja ya familia. Kwenye picha hiyo alionekana Morisi na wadogo zake watatu pamoja na wazazi wao.
Kilichomfanya aitazame sana picha ile lilikuwa ni tabasamu la kipekee la mama yake, "atakuwa amefurahi sana kusikia nipo salama na ninaendelea vizuri na kazi" alijisemea huku akimwangalia mama yake huyo aliyetoka kuongea nae kwa simu mda mchache uliopita. Ilimlazimu amdanganye mama yake kuhusu hali yake, alishindwa kabisa kumweleza uhalisia wa maisha yake mjini, aliijari sana furaha ya mama yake ndiyo maana hakuwa tayali kumpa taarifa mbaya za magumu yanayomkabili kwasasa, "haya ni maisha tu" alimtoka kauli hii ya kujifariji ambayo isinge msaidia chochote baadaye.
Ni ndani ya jumba moja la kifahari sana lililojengwa katika eneo lililojitenga na makazi ya watu, anaonekana mwanamke mmoja umri wa makamo akihangaika kusafisha vyombo vya chakula na kuvipanga ndani ya kabati, aliifanya kazi hiyo kwa mda kidogo, baada ya kumaliza aliingia chumbani ambako alimkuta kijana mmoja aaliyekaa juu ya kochi dogo lllilokuwemo humo ndani. Alikuwa akifanya mawasiliano kwa njia ya video(video call) kupitia kompyuta yake ndogo. Huenda hayakuwa mawasiliano ya kawaida ndiyo maana hata baada ya kijana huyo kugundua uwepo wa mtu mwingine mle ndani, hakujisumbua kumwangalia mpaka pale alipohakikisha amemaliza kuwasiliana, hapo ndipo alipogeuka na kumtazama meanamke yule, "vipi wamekubali" aliuliza yule mwanamke akionekana kujua kilichokuwa kinaendelea, "naona bado wanakuwa wazito kunikubalia" alijibu kijana yule huku akinyanyuka na kumfata yule mwanamke, "kwa sasa tujipe mda kwanza, wale si watu wepesi, hawawezi kumkubalia mtu yeyote kirahisirahisi hivi" aliongea na mda huo tayali alishamfikia na kumkumbatia kwa nyuma mwanamke yule. Zilipita dakika mbili wakiwa bado wamekumbatiana, na tayali walishaanza kupapasana maungoni "mhhhhh!!, Mmewangu, unajua unaponishika huko utasababisha ni,,,", hakumaliza kauli yake kwani mdomo wake ulikutanishwa na ule wa kijana yule na hapo wakaanza kunyonyana wakibadirishana juisi ya mdomoni. Dakika chache baadae kilichokuwa kikisikika humo ndani ilikuwa ni miguno na sauti za mahaba, wawili hawa walikuwa wakiufaidi utamu uliofichwa ndani ya maungo yao ya uzazi.
Ulikuwa ni mtanange mkali uliodumu kwa zaidi ya lisaa limoja na nusu, mpaka wanamaliza kila mmoja alikuwa amechoka sana na walihitaji kupumzika, ghafla wakasikia sauti ya makofi "pa! pa! pa! pa!". "Kazi nzuri sana, unaonekana bado uko vizuri kijana wangu, licha ya umri kwenda lakini bado unaihimili vizuri mikikimiki ya vijana" yalikuwa ni maneno ya mtu ambaye bila shaka ndiye aliyekuwa akipiga makofi yale. Sauti aliyoisikia ndiyo iliyamfanya kushtuka sana "wew, imewezekanaje?"
ITAENDELEA.
 
Kazi nzuri.
 
ILIPOISHIA
"Kazi nzuri sana, unaonekana bado uko vizuri kijana wangu, licha ya umri kwenda lakini bado unaihimili vizuri mikikimiki ya vijana" yalikuwa ni maneno ya mtu ambaye bila shaka ndiye aliyekuwa akipiga makofi yale. Sauti aliyoisikia ndiyo iliyamfanya kushtuka sana "wew! Imewezekanaje"
ENDELEA.
alionge mwanamke yule kwa sauti ambayo haikuelezeka kama ni uoga au hasira. "Imewezekana kwasababu inawazekana, vipi nikuache kwanza umalizie "ugwadu" wako" aliuliza mwanaume mgeni ambaye sasa tunaweza kumuona vizuri, alikuwa ni mwaname mweusi, mfupi kiasi mwenye mwili ulioonekana kuwa imara sana licha ya uzee ulioanza kumyemelea. Mkononi alikuwa kashikilia bunduki, huenda hii ndiyo iliyomfanya mwanamke yule kuogopa, "No! haiwezekani, umepajuaje hapa?" Alihoji mwanamke yule ambaye sasa alikuwa akirudi nyuma kwa hofu, "Sina haja ya kukueleza nimefikaje hapa, chamsingi unapaswa unyanyanyuke hapo ulipo, uongozane na mimi," aliongea mwanaume yule mzee ambaye sasa alishamfikia yule mwanamke, aliinama kuokota nguo ili ampatie yule mwanamke aweze kujistiri kwani alikuwa bado yupo uchi. Hopo ndipo alipofanya ambalo lilikuwa lighalimu maisha yake, ghafla alipigwa teke kali sana mgongoni lililomwacha na maumivu makali sana, hakuwa mzembe hivyo akataka kuinuka haraka lakini alikutanishwa na ngumi mbili nzito za mbavuni zikisindikizwa na teke la nguvu lililomsomba na kumtupa chini mita kadhaa mbele, haraka alijibetua na kusimama hapo ndipo hakuamini macho yake kwa kile alichokishuhudia. Mbele yake alisimama yule kijana lakini katika hali ya kushangaza zaidi kijana yule alikuwa ameyatoa macho pima akitokwa damu tumboni na mdomoni "nini kimetokea" aliongea akimuuliza kijana yule ambaye mpaka dakika hiyo hakuwa hai tena, mwili wake ulidondoka chini kama gunia la viazi. Aligeuka kuangalia kule alipokuwepo yule mwanamke lakini hakona mtu yeyote mahali pale. Mwili wake ulimsisimka sana na hali hiyo ilimshangaza sana mwanaume huyo, alianza kuzunguka mle ndani kwa umakini sana akiwa ameishikilia vizuri bunduki yake, alipekua na kuzunguka kila mahali ndani ya nyumba ile lakini hakuambulia chochoche, hakukuwa na dalili ya uwepo wa mtu mahali pale. Hali hiyo ilizidi kumshangaza na alijionya kutokaa kizembe kwani mtu aliyekutana nae sahivi alikuwa hatari sana, hakuwa mtu wa kawaida kama alivyomzoea. Jambo ambalo alishindwa kuelewa ni namnagani alishambuliwa, na ni mtu gani huyo mwenye Kasi ya ajabu kuweza kufanya mambo yote kwa mda usiozidi sekunde hamsini. Mwanzoni yule bwanamdogo aliyemkuta ndiye aliyemshambulia lakini wazo Hilo lilifutika baada ya kugundua aliyeshambuliwa kwanza ni yule kijana kabla yake. "Atakuwa nani huyu" aliwaza mda ambao alikuwa akirudi kule chumbani, hakuna kitu cha ziada alichokipata maana hata ile kompyuta ndogo ilishachukuliwa, "lnamaana huyu mwanamke anamiliki watu hatari namna hii" aliwaza mzee yule huku akiukagua mwili wa yule kijana kuona kama atapata chochote cha kumsaidia. Baada ya kujiridhisha kuhusu hali ya mle ndani, aliamua kuondoka kupitia dirisha lililoluwa wazi.
Umbali wa kama mita hamsini nje ya nyumba ile wanaonekana watu wawili ,wanamme mmoja akiwa na mwanamke aliyekuwa akihema kwa nguvu, "Bosi, inabidi nifanye mpango uongezewe ulinzi" aliongea mwanaume yule ambaye mda wote alikuwa akimwangalia kwa kumkagua bosi wake huyo kuona kama Kuna sehemu atakuwa kadhurika, " ulinzi siyo shida Kan,, kinachonichanganya ni kivipi huyu mpuuzi amepajua mahali hapa kiurahisi hivi" alifoka kwa hasira mwanamke yule " siku hizi mmeanza kuwa wazembe sana, kunahaja ya kurudi shimoni, naona nitakuwa na wakati mgumu kama mambo yakiendelea hivi" aliendelea kufoka ,wanamke yule. Hapo Kan akataka kujitetea, " lakini boss siyo,,," alikatishwa kwa kupigwa na kofi zito la uso " hivi bado unapata nguvu ya kutetea uzembe wa watu wako, huoni ni kwa namna gani sasa hivi tumekuwa wepesi, hembu tazama kani" yule mwanamke aliongea akiwa anamonesha Kani kule kwenye nyumba yake ambapo alionekana yule mzee akiruka tokea dirishani kuja nje. Hapo Kan akataka kwenda kumdhibiti Mzee yule lakini alizuiwa na boss wake "sikiliza Kan, kabla hujafanya huo ujinga wako unatakiwa ujiulize kwanza, Mzee Mombo amewezaje kupajua hapa? amejuaje kama mda huu ningekuwepo? na kwa ujio wake huo ni wazi kabisa alijua mahali hapa hakuna ulinzi wa kumpa shida ndiyo maana akaamua kuja mwenyewe akijua kabisa angenipata bila shida yeyote," aliongea kwa kina mwanamke yule akionesha siyo muumini wa kufanya mambo kwa kukurupuka. "Sasa sikia Kan, mfatilie huyo mzee, mpaka kufika jioni niwe nimeshajua anaishi maeneo gani ndani ya mji huu, yupo na kina nani na taarifa zangu amezipataje, ongea na King atume vijana wakasafishe mle ndani, mwambie awaandae WAKINZI, usikuu huu lazima nikamtembelee huyo Mzee". Aliongea yule mwanamke akitoa maelekezo kwa kijana wake kisha akatoka ndani ya maficho yale na kuelekea kule nyumbani kwake. Kan hakuwa na mda wa kupoteza, haraka alianza kumfatilia mzee yule ambaye tayali alishapotelea vichakani, alitembea kwa haraka huku akiichomoa simu yake mfukoni na kupiga mahali. Haukupita mda alimuona mzee Mombo aliyekuwa alitembea kwa tahadhari kubwa ndani ya vichaka vile, alitamani kumshambulia Mzee yule ambaye amesababisha leo hii yeye amekaripiwa na bosi wake, alitamani amvamie amuoneshe yeye ni nani katika ulimwengu wa mapigano, lakini alijionya, kufanya vile kungeharibu mpango mzima alioupanga bosi.
Upande wa Morisi, jioni hiyo alikuwa mwenye hofu sana, hofu ambayo ilimuondolea hamu ya chakula, jioni hiyo illikuwa tofauti na siku nyingine ambapo mda kama huo ungemkuta ameshaandaa chakula chake cha usiku. Jioni hii alikuwa ameketi kibalazani nje ya nyumba, tayali ameshaandaa vitu vyake na hapo alimsubili mwenyeji wake afike ili akaijue hatima yake, "Ndio mda wake huu" alijisemea baada ya kuiangalia saa yake mkononi. "Sijui bado atataka niondoke!", aliwaza Morisi ambaye licha ya kuwa alishaelezwa leo hii angepewa nauli ili aondoke, bado hakuamini kabisa kama ndugu yake yule angemfukuza, hivyo hata mawazo yake hayakuwa kuwaza namna ya kuondoka, aliamini huenda leo mwenyeji wake angebadili msimamo wake.
Tokea upande wa mashariki mwa nyumba ile ilisikika sauti ya muungrumo wa pikipiki ambayo Morisi aliitambua haraka kuwa ni pikipiki ya mwenyeji wake, haukupita mda mrefu pikipiki ile ilifika mahali pale juu yake alionekana Nemes akiwa na yule rafiki yake tunayemfahamu kama baba Sesi wakirudi toka kazini. Nemes hakujisumbua hata kumsalimia Morisi, baada ya kuipaki pikipiki yake aliingia ndani, huku nje alibaki yule mwenzake ambaye alienda kukaa mahali pale alipokuwepo morisi. "Vipi hali yako dogo, unaendeleaje?" yule nwanaume aliuuliza " siyo mbaya kaka, naona kadli siku zinavyoenda afya yangu inazidi kuimarika" alijibu Morisi muda huo akiwaza kumweleza mwanaume huyo mpango wake wa kutafuta chumba cha kupanga endapo angetimuliwa na mwenyeji wake. "Ok,itakuwa vizuri ukipona ukachukue nafasi yako kabla hajawekwa mtu mwingine". Maneno hayo yalipenya kama msumari ndani ya moyo wake kiasi cha kutamani kulia, Morisi alikumbuka namna alivyohangaika kuipata nafasi hiyo, ilikuwa ni nafasi ya kufanya kazi kama mwajiliwa wa kudumu kwenye mradi wa ujenzi wa selikari kule wanakofanyia kazi ndugu zake hao. Kutokana na kwamba hakuwa na elimu hata ya kidato cha nne, alimtegemea ndugu yake Nemes amfanyie mpango wa kupata kazi, hata hivyo haikuwa rahisi kwani waliopaswa kuajiliwa kama vibarua saidia fundi katika mradi ule walitakiwa kuwa wazawa wenyeji wa mahali pale. Moris hakuwa mwenyeji wa mahali pale hivyo ikamlazimu kuongea na kiongozi wa eneo lile ambaye baada ya kulambishwa asali(kupewa hongo) alikubali kumuandikia barua ya utambulisho kama mwenyeji wa eneo lile. Ugumu haukuishia hapo, maana alilazimika kutoa hongo kwa maafisa wahusika wa mambo ya vibarua katika mradi ule. "ndiyo malengo yangu, nikishapona lazima nirudi kazini" alijibu Morisi kabla ya kumuuliza mwanaume yule "Hivi maeneo haya chumba wanapangisha kwa bei gani" inaonekana hakutegemea kuulizwa swali kama hilo, hivyo akajikuta naye akiuliza "kwanini unaulizia chumba bwanamdogo, vipi unataka ukapange?". Kwakuwa Morisi hakuwa mtu mrahisi keleza shida zake kwa watu wengine, aliamua kudanganya pasipo kujua tayali mwanaume yule ameshaugundua mpango wake, "hamna, nilikuwa nawaza kwa wakati ujao, maana najua sitoendelee kukaa kwa ndugu yangu siku zote" alijibu Morisi asielewe uongo wake umekwishajulikana, "vyumba vipo tena vizuri lakini bei hutofautiana eneo kwa eneo, mfano kwa pale,,," maelezo yake yalikatishwa na sauti ya Nemes tokea ndani "we Morisi wewe!" Morisi aliinuka na kwenda kumsikiliza ndugu yake huyo, "Chukua hii hela ukatuletee msosi, maana leo hatujapita mgahawani". Morisi baada ya kupewa maelekezo yale aliingia chumbani ambako aliivua kaptula yake ambayo huivaa akiwa maeneo ya nyumbani, alivaa suruali ndefu ili aende mgahawani kuchukua chakula kama alivyoagizwa.
Baba Sesi alibaki akiwa anatafakari kuhusu kile alichoambiwa na Morisi, "inaonekana bwanamdogo hataki kuondoka" aliwaza na wakati huo alimuona Morisi akitokea ndani, mkononi alishikilia mfuko ambao bila shaka ulikuwa wa kubebea chakula, Morisi aliaga na kuondoka. "Dogo yupo sahihi, hata ningekuwa mimi nisingeondoka yaani nihangaike kutafuta kazi, nimeipata hata malipo ya mwezi mmoja sijapata atokee mtu aniambie niachane na kazi niondoke wee!! Pangechimbika mjini hapa." Alijisemea baba Sesi akijaribu kujivika uhusika wa kile anachopitia Morisi. "Ngoja nisubilie, kama akiniambia nimtafutie chumba nitafanya hivyo, kwani nini bwana! Yaani unamfukuza ndugu yako kisa ugonjwa, eti amekaa wiki mbili bila kuingiza chochote?." Mwanaume huyu alionekana kutokubaliana na rafiki yake Nemes, aliamini ni mjinga pekee anayeweza kufanya kitu kama hicho hasa kwa ndugu yake, hata hivyo hakuwa na chakufanya maana hata alivyojaribu kushauri hakusikilizwa hivyo aliamua kuwaacha wenyewe.
Morisi alikuwa akitembea haraka haraka sana, alipanga atumie mda mchache kufika mgahawani ambako angechukua chakula awahi kurudi akaendeleze mazungumzo yake na baba Sesi. Hazikupita hata dakika tano akawa ameliona lile bango kubwa "KWA MAMA ZABI, VYAKULA VITAMU" aliyasoma maneno hayo ambayo yeye huwa anakiri kuwa ni ya kweli. Alikuwa tayalii amefika mgahawani na kama bahati, mbele yake alimuona Mama zabi mwenyewe hapo alitabasamu maana alijua angehudumiwa haraka kisha angeondoka..
ITAENDELEA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom