Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,502
- 22,355
Yanga na Simba mwaka 1974 Uwanja wa Nyamagana Mwanza.
Mechi ya Yanga na Simba ambayo itakumbukwa kwa simulizi zake za kusisimua ni ile ilochezwa uwanja wa Nyamagana mkoani mwanza mwaka 1974.
Ilikuwa ni fainali ya kombe la FA ambapo miamba hii ilipambana kwa dakika zaidi ya 90.
Kwa mujibu wa msimulizi wangu Mzee Abdalah Juma Zungo, ilikuwa ni mechi ya kukata na shoka.
Simba iliundwa na wachezaji kama Haidari Abeid, Khalid Abeid, Martin Kikwa, Hamis Askari, Mohamed Kajole, Abdalah Hussein, Athumani Juma, Ismail Mwarabu, Yussuf Kaungu, Adam Sabu na Aluu Ally.
Yanga nao kama kawaida walikuwa na Muhidin Fadhili, beki wa kulia Athumani Kilambo (baba watoto), beki kushoto Suleiman Saidi, mabeki wa kati walikuwa ni Hassan Gobos na Omari Kapera. Namba 6 alikuwa ni Abadulrahman Juma, na namba 8 ni Sunday Manara (computer).
Washambuliaji wa pembeni namba 7 alikuwa ni Godfrey Nguruko na namba 11 alikuwa ni Maulidi Dilunga, namba 10 ni Gibson Sembuli na mshambuliaji mwenyewe namba 9 alikuwa ni Kitwana Manara "Popat".
Mechi ilikuwa ni ya kusisimua huku wachezaji wa kiungo wa Simba Aluu Ally akiwa anapambana vilivyo na Sunday Manara, Omari Kapera alikuwa akimchunga vilivyo Adam Sabu.
Dakika ya 16 Aluu Ally akamtoka Omari Kapera na kumpasia mpira Adam Sabu, nae bla hiana akafunga goli la kwanza kistadi hasa maana lilikuwa ni shuti la mbali mguu wa kulia liitwalo kwa kiingereza "volley".Uwanja mzima ilirindima kwa yowe na vifijo na Yanga wakawa nyuma kwa goli 1-0.
Uwanja mzima ilirindima kwa yowe na vifijo na Yanga wakawa nyuma kwa goli 1-0.
Yanga walijaribu kujibu mapigo lakini ngome ya Simba ikiwa chini ya Haidari Abeid haikulala na mpaka timu zinaenda mapumziko Simba 1 Yanga 0.
Itaendelea.