Simu kutoka tume ya ajira.

deonova

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
742
Reaction score
420
Habari wadau,
Kuna kazi zilitangazwa na sekretariat ya ajira tukaomba wengi mwezi wa 5 mwaka 2012 then tukaitwa written interview mwezi wa 12 mwaka huo huo na baada ya siku 3 tukaenda kufanya Oral interview. Baada ya hapo mwezi wa 1 na wa 2 mwaka jana 2013 wakaitwa waliochaguliwa kuripoti kazini na baadae wameendelea kuitwa mmoja mmoja kila vacancy inapotokea mimi nikawa nimeshajikatia tamaa.
Sasa jana jioni around saa 18:20 kumbe kuna simu ilipigwa ya landline bwana mi sijasikia maana bado nilikuwa kibaruani, nimekuja kuona missed calls saa moja jioni, nikapiga ikaita bila kupokelewa.
Nikaona basi ngoja nitapiga leo asubuhi, so around saa tatu nikapiga akapokea mshua mmoja nikajieleza pale kuwa nilikuta missed calls jana. Wao walitaka kujua employment status yangu kwa sasa na niko wapi. Nikajieleza niko Dar kwa sasa na nafanya kazi ya muda (short term contract) kwenye private company moja. Jamaa kanambia watanipigia baadae. Baada ya kukata simu nikajistukia aaah kwa kusema nafanya kazi inaweza kuninyima hyo fursa kwa wao kuassume tayari nina kazi so wakanitupa kapuni ama? Ingawa nahisi kwa ambaye tayari ana kazi serikalini ndo inakuwa tatizo.
Je wadau hii ni sawa ama nimejibu wrong kwa kusema nafanya kazi? Nitoeni wasiwasi jamani Comrades.
 
Ingawa nahisi kwa ambaye tayari ana kazi serikalini ndo inakuwa tatizo.
Je wadau hii ni sawa ama nimejibu wrong kwa kusema nafanya kazi? Nitoeni wasiwasi jamani Comrades.

Mbona ushafanikiwa kujitoa wasiwasi comrade??????ni hakunaga jibu lingine tofauti na hilo
 
Asante Toria basi hebu ngoja niwasikilizie maana leo siku ya 2 bado hawajanicheki tena.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…